Nahitaji kuandaa jambo hili naomba mwenye uelewa nalo anisaidie dondoo zake

Mcheza Viduku

JF-Expert Member
Jun 24, 2020
1,059
2,569
Umofia kwenu bandugu wote kwenye hiki kilinge chetu cha kujidai. Nina ombi kwenu wadau.

Nina mpango wa kuandaa tamasha la stand up comedy huku mkoa ninaoishi, nimeiona hiyo fursa naamini nitapiga hela.

Sasa ombi langu kwenu ni mwenye uzoefu wa uandaaji wa event za namna hii naomba anisaidie hatua kwa hatua za kupitia hadi kufikia siku ya show, ombi la pili show yangu nataka iwahusishe member wote wa CHEKA TU, sasa kwa mwenye connection ya kuniwezesha kuufikia uongozi wao pia anisaidie kwa hilo, na hata kama unaweza kuwa unajua gharama zao nisaidie Mtamzania mwenzangu, natanguliza shukrani kwenu 🙏🏻

NB: Niko serious kutaka kufanya hii ishu ndugu zangu.
 
Back
Top Bottom