Waungwana,
Salaam za mwaka mpya! Pia poleni na majukumu ya January. Niwatie moyo kuwa uvumilivu ndio ngao imara katika vita ya maisha. Mdogo mdogo tutafika.
Nisiwachoshe!
Husika na kichwa cha habari.
Mimi ni kijana ambae nina shughuli zangu halali, kipato changu ni cha kati (middle class) lakini ninahitaji kuongeza kipato.
Fursa niliyoiona ni kumiliki gari ndogo ya biashara hapa mjini kama starlet, vitz, paso nk.. Changamoto ni pesa!
Bado sijawa na kipato kikubwa kuweza kununua gari kwa pesa moja kwa moja.
Najua kuna watu ambao huwa wanauza magari kwa malipo ya mkataba Ila tatizo ni connection. Na ndio maana nimeweka hapa hili bandiko nikitegemea kuwa litaonwa na watu wengi ili niweze kusaidiwa hitaji langu.
Hivyo basi. Kama wewe ni mtu wa magari na unafanya biashara kwa mtindo huu, au una mtu/watu unawafahamu, au kama labda una gari ndogo hapo nyumbani na halina matumizi, naomba uguswe na hili ombi langu ili tuwezeshane.
Nahitaji gari nzima tu hata ikiwa namba ni (A).
Nasisitiza kuwa, Nina shughuli zangu ambazo zinaniingizia kipato japo so kikubwa hivyo nina uhakika gari itaniongezea kipato zaidi na nitaweza kulipia hesabu yake kwa wakati.
Natanguliza shukrani.
N.B. NAHITAJI GARI KWA AJILI YA KUONGEZA KIPATO SIO STAREHE ZA MJINI.
Sent using
Jamii Forums mobile app