Nina friji ya mtumba, nikiiunganisha kwenye umeme inafanya kazi vizuri ila umeme ukiyumba kidogo tu au ukikatika na kurudi hapo hapo inazimika na haiwaki tena mpaka baada ya muda mrefu.
Muuzaji kasema friji ni nzima na hiyo ni kawaida kwa friji zote za mitumba kutoka nchi za Ulaya ila nina kawaida ya kutowaamini wauzaji. Isipozimika inapoA vizuri. Kanishauri nitumie stabilizer. Kwa stabilizer umeme ukishake haizimiki ila ukikatika na kurudi inazimika kabisa. Nini hii??
Ni kawaida kwa compressor za German umeme ukishtuka ikiwa hot inazima na haiwezi kuwaka mpaka ipoe kabisa almost 45 min. Hilo si ubovu bali ni mfumo wake wa kuilinda ila kwa usalama wa fridge yako nakushauri nunua fridgeguard inauzwa kuanzia 25,000/= usiamini stabilizer hazina msaada sana kwa umeme wa fridge.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.