Nahisi nimerogwa


Ahsante kwa ushauri
 

Ahsante kwa ushauri
 
Ongea na wazee wako ili wakaongee n a huyo mama ili atengue kauli yake juu yako, na baada ya hapo uhame usionane nae na mambo yatarudi kama zamani
 
Kwa hio unanishauri VP.maana kwa sasa ninafanya biashara moja tu.nimefungua Bangalow kwa ajili ya watalii.Ila nimeshaichoka hii biashara maana Hawa jamaa wana mazarau sana.

Bungalow au Hotel? Vyovyote vile, Baniani mbaya kiatu chake dawa.
Mkuu hii ni biashara ya nne sasa ndani ya miaka 7 au pungufu. Bora ulivyobaki na moja. Isimamie kwa miaka kama mi5.

Ikiwa stori yako ni kweli, hapo ndo umerudi nyumbani maana ulikua unadili na watalii ndo ulipopata pesa na kuanza kuhangaika na kila kitu. Busara ya biashara ilikutaka kama ni magari, basi ununue ya utalii, boti la kubeba watalii, n.k. kwa kifupi ungekua na kuwa kampuni ya utalii. Usiwe kama yule Arawa alieimbwa miaka nenda rudi ye kubadilisha biashara tu.
 
katika habar hii hujataja wazazi asa sijui ushiriki wako na familia yako ukoje au uko pekeako kwenu?? mali nyingi kijana mdogo lazima kuna kitu
 

Ahsante Huu ndo miongoni mwa ushauri mzuri k uliko yote.nimeupenda sana.nakuahidi nitaufanyia kazi.Bila ya kusahau nitakupatia mrejesho
 
Unakaribishwa tena. Lakini SAGHIR ungeweza kushauriwa vema zaidi. Tatizo kuna maswali ya wadau huko juu hujayajibu. How come madhila yako uko tu wewe na huyo mmama 'mlogaji'? Elimu hujaizungumzia na mambo mengi. Ndo maana unaulizwa maswali kuliko kushauriwa.
 
Last edited by a moderator:
namuamini sana mungu,ilana pia najua uchawi upo.maana hata katika vitabu vya dini umezungumziwa.

ukimwamini mungu 100%, ukajitoa ufunge hata mwezi mmoja tuu!!
Soma maandiko na kufanya maombi kwa ratiba ifaayo hakika mungu muweza wa yote hakuna la kumshinda!!!
Mungu ni rafiki yetu tuwapo nyakati ngumu tuzungumze naye, wasamehe wote walokukwaza na ondoa vinyongo na chochote na omba omba omba omba mungu atakushindia kk!!!
God be with you
 
Hakuna mganga mkweli,nahisi ataenda kunilia hela zangu.

Shetani ana departments nyingi, mojawapo ni ya uchawi halafu nyingine ni ya uganga. Wote hao wanareport kwa shetani na wanapata resources za kutendea kazi toka kwa shetani.

Kukosa maarifa ni janga kubwa sana.
 

Ahsante sana.elimu yangu ni Degree ya Business Information Technology (BIT).
 
Last edited by a moderator:

Ahsante kwa ushauri mzuri
 
Shetani ana departments nyingi, mojawapo ni ya uchawi halafu nyingine ni ya uganga. Wote hao wanareport kwa shetani na wanapata resources za kutendea kazi toka kwa shetani.

Kukosa maarifa ni janga kubwa sana.

Ahsante kwa ushauri
 
katika habar hii hujataja wazazi asa sijui ushiriki wako na familia yako ukoje au uko pekeako kwenu?? mali nyingi kijana mdogo lazima kuna kitu

Kuhusu wazazi nipo nao.ila kwa sasa hawapo tz.wanaishi London pamoja na wadogo zangu wawili
 

Pole sana ila naomba uchunguze kwanza labda huyo mke mpya ndiye tatizo
 
Pole sana ila naomba uchunguze kwanza labda huyo mke mpya ndiye tatizo
kuhusu mke wangu mpya sijawa na uhakika bado,maana nimeshamchunguza vya kutosha kama ana imani za kishetani au laa, ni msikivu sana nawala sidhani kama anaweza kunienda kinyume,lakini kwa vile umenipa ushauri sitoudharau nitaendelea kuwa makini. ahsante.
 
Kukata mzizi wa fitna muoe huyo mama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…