Nahisi nimerogwa


Sijabisha ila nishaomba sana kama umenielewa.najua humu ndani muna magreat thinkers ndio maana nimeomba ushauri.
 
Kuwa na imana tu omba mungu wako hayo ni majaribu
 
Zaburi 127 : 1 Bwana asipoijenga
nyumba Waijengao
wafanya kazi bure. Bwana
asipoulinda mji Yeye
aulindaye akesha bure.
 
wahi haraka kwa manyaunyau
 
Binafsi yangu naomba nikuulize maswali yafuatayo;
1.je,umesha au ulikuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na binti wa huyo mama?
2.ilisha toke siku yoyote huko nyuma kumuahidi huyo mama ya kuwa utamuoa binti yake hata kama ni kwa utani?
3.Mahusiano yako na huyo mama ukiachana na biashara yakoje au yalikuwaje na kwainin ulimpa yeye kipaumbele sana badala ya ndugu zako wa karibu?
4.Na uhalali wa mali zako hizo ukoje,hii nikitilia maanani ya kuwa je ulirithishwa,ulitumia ndumbaa,ulisha wahi kudhulumu au kula viapo fulani kwa minajili ya kupata hizo mali?
5.wazazi wako au ndugu wa karibu wako wapi na umewashirikisha vipi au kwa kiasi gani katika hili?

JARIBU KUYATAFAKARI MASWALI HAYA ALAFU UTAPATA PICHA FULANI...KISHA CONNECT DOTS SASA KUONA TATIZO LIKO WAPI

MUNGU NA AKUPIGANIE KATIKA JINA LA YESU KRISTO.BARIKIWA.
 
Aliwazalo mjinga ndio linalo mtokea.Ashakum si matusi,sija kutukana hapo mleta uzi ila nataka kutoa uhalisia wa fikra zako,inaonekana tangu mwanzo ulisha weka fikira za kulogwa na huyo mama ndio maana badala ya kufikiria sababu za kibiashara zinazo kuyumbisha wewe unawaza kulogwa

Anza kwanza kujibu maswali ya mkuu Gibeath-Elohimu hapo juu then kama hizo biashara zako ni za halali na ulizipata kwa jasho lako bila dhuluma wala ndumba basi jichunguze tu mwenendo wako wa usimamizi wa hizo biashara na ukaribu wako na Mungu wako.

Kila la kheri
 
kijana pole sana ila unaonekana hujafilisika sana... emu nitumie 10,000 kwenye tigo pesa ili npate nguvu ya kukushauri
 
Huyo mama anaweza akawa chanzo cha hayo yote yanayokukuta au asiwe...ila kwa jinsi ulivyoelezea anaweza akawa anahusika...ingawa wewe ni muislam nakushauri rafiki nenda ukaombewe kwani case kama hizo nyingi sana zimepata ufumbuzi kwa njia ya maombi tu hamna haja ya mganga...wengine baada ya kuombewa mapepo yalilipuka na kusema yalitumwa na nani na kwa nini na kisha yakaondoka...fungua 98.1 FM kila jumapili SAA 4 usiku au jumatatu SAA 6 mchana usikilize au njo sabasaba maonyesho dar es salaam jumanne kuanzia saa nne asubuhi mpaka jioni utaonana na mtumishi na kama upo mbali sana tafuta sehemu wanayofanya maombi uende utafanyiwa maombi hayo yote yanayokusumbua yote yataisha kama kwengine ulipojarib palishindikana jaribu hii uone...karibu pia sabasaba kwa mchungaji Katunzi hicho kitatizo kitaondoka tu katika jina linalopita majina yote JINA LA YESU...kwa maelezo zaidi ni PM
 
sizani Kama kuna suluhisho jingine hapo zaidi ya Mungu nakuonea huruma maana shetani akimshambulia mtu ni sekunde itabakia story tuu ulikuwaga na hiki na kile nakwambia mdogowangu itabakia story utauza hadi nyumba, kuomba kupo ila sio kila maombi yatakusaidia ndio maana hata wewe mwenyewe umeomba sana na huoni matokeo hapo unatakiwa upate neno la maarifa kijana ukiwa huna maarifa kumshinda shetani story naatakumaliza naakisha maliza mali zako atahamia kwenye afya yako mwisho mauti ni pm nikusaidie faster kabla haujakwisha.
 

Mkuu.kama umeyaelewa maelezo yangu mwanzo utagundua kuwa mm sijarithi mali.nikiwa na umri Wa miaka 16 nilibahatika kufuga dola nikiwa bado ni kijana mdogo.maana kazi yangu ya kwanza ilikuwa ni kutembeza watalii.nilifanikiwa kupata dola elf 3.ndipo nilipoanzisha biashara zingine.Mkuu Huyu mama ni MTU Wang Wa karibu kwa Kuwa ni yy aliyeniambia nifanye biashara.
 
Enyi wana jf,ni lini mtaacha kuleta story za kutungwa na kupoteza muda wa kujadili vitu vya kufikirika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…