Nahisi nimeimbiliziwa (Nimerogwa) nisitoboe

Nahisi nimeimbiliziwa (Nimerogwa) nisitoboe

Mr Chromium

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2020
Posts
2,760
Reaction score
3,858
Aisee

Nalipwa 1.9M lakini ukiniangalia maisha yangu utacheka
  • Sina gari
  • Sina nyumba
  • Kiwanja ninacho
  • Sivai vizuri
  • Sili vizuri
  • Sipigi bata
Lakini katikati tu ya mwez nmeishiwa!!

Yaani najikuta hela inanitoka kwenye mazngira ya ajab ajab!! Sisemi inatoweka kama zile za chuma ulete NO but nikipata mshahara tu vishida na visababu vya kutumia hela vijatokea kusikojulikana!!

Mfano jana nimechelewa kuamka kwenda kazini ikabidi na kulikuwa na ugeni!! Na mimi ofisini ni mtu muhimu sana so ikabidi nikodi boda hadi kazini 13,000

Nilipofika nimesahau flash na ilikua na document muhimu ikabidi nirudi kwenda kurudi 26000
Bado sijala
Bado sijarudi jioni

Actually tuvitu twingi twingi tunasababisha hela itumike ili mradi iishe tu.

Nawaza kazi ikiisha ntaishije

Kuna shida gani hapa

We unaonaje? Share experience
 
Dunia haiko fair mpaka muda unaona kama wengine wanania ya kutambia watu, 26000 mimi nimetumia Week nzima tena Safari kibao nimepanda gari kibao hiyohiyo nimejikimu kula, vocha nk Mungu atupe na sisi kipato.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huna gari huna nyumba
Kwa ushauri wangu hamia karibu na kazi
Ila hujasema unajiwekea kiasi gani pembeni, kama unazimaliza zote basi una tatizo inabidi ukawaone washauri wa masuala ya fedha [emoji848][emoji848]
 
Hivyo vishida vidogo vinatoa hela kwenye akaunti yako au huwa unatoa mwenyewe?! Tatizo lako ni kuwa huna financial discipline. Huna nidhamu ya fedha wala malengo na fedha zako.

Ni kawaida kuona mko ofisi moja mna mshahara Sawa ila mwingine amejenga na kununua gari wengine hawana chochote na wanabaki kujipa moyo fulani mwizi!
 
Sasa tukinunua wote magari nani atamuomba mwenzake lifti?

Anyway, ukitaka uendelee kwa mshahara, unatakiwa uukopee huo mshahara. Hapo hiyo hela unayopata ndo ununue hilo gari ama upandishe nyumba.

La sivyo utakuwa unazunguka duara tu
 
Kitu cha Kwanza kabisa..

Unakaa mbali sana na Kazini.

Unajua sehemu ya Boda Elfu 13 ni kama Ubungo hadi Kongowe ya Mbagala au zaidi.

Kwa mshahara wako unaweza pata nyumba sehemu ya jirani na kazini kwako let's say kazini Posta (assume unakaa Dar), unakaa apartment moja kali sana hapo Kigamboni. Nauli haizidi elfu 2 kwa boda siku nyingine unapanda kivuko the rest unatembea.

Cha pili,

Acha kufurahisha kila mtu. Yaani unajitia Yesu sana kila mwenye shida una mtatulia. Na mimi nina tatizo ili na ndio target yangu Feb nilitatue.

Tatu

Anza kutrack matumizi yako
. Tumia App mfano ya Money Manager unaipata Android na iOS. Una customize the way unavotaka. Itakuonesha ni wapi unatumia zaidi hela so wewe utaamua ufanyeje.

Ngoja nikuoneshe screenshot ya App kwangu mwezi January..

Screenshot_2021-01-29-08-12-11-230_com.realbyteapps.moneymanagerfree.jpg

Mimi ugonjwa wangu Giveaways najifanyaga Mwema sana nagawa sana misaada. February nabadilisha namba manina.

Bike na gari ni therapy. Nakaa jirani na kazini ila hivo vinanipa therapy ndio maana matumizi nayo makubwa.

Ila utaona no mavazi, no beers, sili vizuri, sina maendeleo. Am too f***d up sema atleast najua wapi nakosea.

Jaribu man mwezi Feb huu hafu tuone mzee baba. Achana na wanaosema tafuta kipato cha pili wewe hata ukiwa na Million 6 kwa mwezi wewe tatizo lako lipo pale pale.
 
Kitu cha Kwanza kabisa..

Unakaa mbali sana na Kazini.

Unajua sehemu ya Boda Elfu 13 ni kama Ubungo hadi Kongowe ya Mbagala au zaidi.

Kwa mshahara wako unaweza pata nyumba sehemu ya jirani na kazini kwako let's say kazini Posta (assume unakaa Dar), unakaa apartment moja kali sana hapo Kigamboni. Nauli haizidi elfu 2 kwa boda siku nyingine unapanda kivuko the rest unatembea.

Cha pili,

Acha kufurahisha kila mtu. Yaani unajitia Yesu sana kila mwenye shida una mtatulia. Na mimi nina tatizo ili na ndio target yangu Feb nilitatue.

Tatu

Anza kutrack matumizi yako
. Tumia App mfano ya Money Manager unaipata Android na iOS. Una customize the way unavotaka. Itakuonesha ni wapi unatumia zaidi hela so wewe utaamua ufanyeje.

Ngoja nikuoneshe screenshot ya App kwangu mwezi January..

View attachment 1688772

Mimi ugonjwa wangu Giveaways najifanyaga Mwema sana nagawa sana misaada. February nabadirisha namba manina.

Bike na gari ni therapy. Nakaa jirani na kazini ila ivo vinanipa therapy ndio maana matumizi nayo makubwa.

Ila utaona no mavazi, no beers, sili vizuri, sina maendeleo. Am too f***d up sema atleast najua wapi nakosea.

Jaribu man mwezi Feb huu hafu tuone mzee baba. Achana na wanaosema tafuta kipato cha pili wewe ata ukiwa na Million 6 kwa mwezi wewe tatizo lako lipo pale pale.

Nakubali kaka
 
Back
Top Bottom