Nahisi mtoto si wangu

MTINGIJOLI

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
1,455
1,473
Habari zenu wana JF,

Kuna binti nina mahusiano nae, ni (Bar tender) aliniambia ana ujazito na nimeukubali hadi sasa amejifungua, ila ghafla nimepatwa na hofu na sijui kwa nini,nahisi tu, huyu mtoto si damu yangu.
 
bar tender sio watu mkuu 100% ya bar tender ni washenzi kuliko unavyofikiri wanalal na mtu yeyeto ili mradi pesa ipo
 
We kama vepee nenda ukapime dna. Maana unaweza ukasema si wako, kumbe ni damu yako ni vile kafanana na bibi mzaa bibi ake
 
Swali la kizushi, Ulikula au hukula? Ulitumia kinga au hukutumia? Uliingiza kwenye tundu au uliingiza masikioni? Uliambiwa from the beginning au kukuambiwa? Kama maswali yote hayo unayo majibu yake basi usikimbie majukumu
 
Habari Zenu wana Jf, Kuna binti Nina Mahusiano nae, ni ( Bar tender ) Aliniambia ana Ujazito na Na nimeukubali hadi Sasa Amejifungua, Ila Ghafla nimepatwa na hofu na Sijui kwa nini, Nahisi tu, Huyu Mtoto Si Damu Yangu
acha kuhisi, ulitakiwa kujiridhisha tangu mimba, sio mtoto kazaliwa ndo unaaanza kukimbia majukumu, , laa humuamini mwenziwako kuna kipimo cha DNA TEST. nenda kapime uone utakavyoumbuka.
 
Kuna namna nyingi sana za kuweza kujua kwa awali either mtoto ni wako ama la, zamani kulia hakuna kuchek DNA lakini wazee waliweza kujua hapa mama alichepuka na walikuwa correct kwa asilimia kubwa tu..Mpaka sasa njia zile still zinatumika kuweza tambua kama mtoto ni wako ama la kwa kumuangalia mtoto sura, umbo lake, baadhi ya viungo vyake ikiwa ni pamoja na kucha, vidole, tembea yake, cheka yake nk...
Ila huko ni mbali maadamu wewe ulishiriki tendo na huyo mama bila tahadhari yeyote ya kujikinga na mimba na leo unaambia haya ndiyo matokeo ya kazi ile mliofanya na mama huyo wacha kuwaza mara mbili..Mara moja anza kuhudumia mtoto na kama ikija julikana si wako huko baadae hutakuwa na cha kujuta watoto ni baraka na wanahitaji msaada wa matunzo hata kama si wako..lakini ulishakuwa na ukaribu na mama yake tunza huyo mtoto..
 
These days wenye uhakika na nasaba ya mtoto ni wachache kuliko wasio na uhakika kuhusu uhalali wa mtoto,Lea tu.
 
Swali la kizushi, Ulikula au hukula? Ulitumia kinga au hukutumia? Uliingiza kwenye tundu au uliingiza masikioni? Uliambiwa from the beginning au kukuambiwa? Kama maswali yote hayo unayo majibu yake basi usikimbie majukumu

Nakimbiaje Majukumu? Mimi ndie Nilielea Mimba hadi Anajifungua, Na Huduma zote nilikua nampatia.
 
acha kuhisi, ulitakiwa kujiridhisha tangu mimba, sio mtoto kazaliwa ndo unaaanza kukimbia majukumu, , laa humuamini mwenziwako kuna kipimo cha DNA TEST. nenda kapime uone utakavyoumbuka.

Majibu yakiwa Mazuri ndio Furaha Yangu Mkuu, Siwezi Kukimbia Majukumu, Nahitaji sana Mtoto, Na Uwezo wa kumuhudumia Ninao, Ila awe kweli damu Yangu, Sio wa Kubambikiziwa
 
Kipimo cha kwanza uliingiliana nae lini kwa maana ya tarehe je zimeendana na tarehe ya kuzaliwa mtoto?
Kama ndio dalili yakwanza ni mwanao. Hiyo tu haitoshi mwangalie mtoto sura hasa miezi ya mwanzo lazima atakuwa na mwelekeo wa sura yako, head formation, sura, masikio. Kama hafanani bado haijalishi sio mwanao.

Kucha za vidole hazitakuangusha, hasa vidole gumba na kidole cha mwisho vya mkono na miguu ukichunguza vizuri huitaji dna.

Mwisho shukuru tu kwamba umepewa heshima ya kuitwa baba hata kama sio wako, umepewa heshima kubwa. Hakikisha kila kitu kipo kwa jina lako na toa angalizo ikitokea akaja mtu mwingine na kusema ni mwanae atalipa gharama kubwa.

Chukuo jukumu la kulea mpaka utakapoambiwa vinginevyo
 
Back
Top Bottom