Nahisi maumivu chini ya kifua

Nahisi maumivu chini ya kifua

kingphisher

Senior Member
Joined
Nov 30, 2024
Posts
119
Reaction score
226
Wakuu, wataalamu. Nimeanza kuhisi maumivu makali sana maeneo ya chini ya kifua. Ni siku ya tano toka nimeanza kuiExperience. Nimekuwa nikitumia dawa za maumivu kutuliza maumivu.

Kama kuna anayejua dawa inayowesa kunisaidia anisaidie, maana hii hali nasikia wanasema huwa inatibiwa kienyeji, lakini hapa nipo Dar.

Bado natafuta hela ya kwenda hospitalini, ila kama kuna dawa naweza kutumia kwa muda basi naomba mniambia. Maumivu ni makali hasa muda wa usiku.

human-muscle-4933416 (2).jpg
 
View attachment 3515552
Umeandika kwa Hisia na maelezo yako yako bayana, hivyo sitarajii ukichukulia jambo kwa mzaha.

Bushdokta ni daktari wa mitishamba, hata hivyo ktk eneo hili tumewezeshwa kutambua maradhi yanayoweza kutibiwa kwa dawa na vipimo vya hospitali.

Maumivu yako ni eneo la Epigastrium yaani Chembe ya Moyo kwa lugha za kiswahili

Maumivu haya huashiria, Michubuko ktk njia ya Chakula Esophagus( Esophagistis), Gastric( Gastritis) na pia ni dalili za vidonda vya tumbo- Peptic Ulcer Disease.

Kama umri wako ni kuanzia miaka 40 kwenda Juu hakikisha

1. Unapima Blood Presha yako, BP
2. Kama presha iko juu hata kidogo tu pima Kipimo cha Moyo, ECG

Ikiwa Presha yako iko sawa basi Pima kipomo cha Maambukizi ya Bakteria wa Helicobacter Pylori ktk choo kikubwa, huyu bacteria husababisha michubuko, vidonda vya tumbo na acid nyingi.

Umesema umekuwa ukitumia dawa za maumivu kwa siku tano. Nakushauri uziache kuanzia leo kwani husababisha vidonda, michubuko na hata kuongeza maumivu zaidi.

Msisitizo; Kama una umri wa kuanzia 40 kwenda juu, nakuomba uende hospitali muda huu zingatia niliyoandika hapo juu. Na pengine kwrnye familia kuna ndugu wenye presha au maradhi ya moyo zingatia zaidi.

Kama umri sio ktk kiwango hicho, pata dawa za kupunguza acid tumboni za maji na vidonge then kesho nenda hospitali kwa H.Pylori testing.

Kuhusu matumizi ya mitishamba ni mpaka uwe umetimiza hayo juu, usipoteze muda na pesa zako
 
Maelezo ya Bush Dokta ni ya kuzingatia sana. Kwanza anza ni possibility ambayo ni ya hatari zaidi.
Kipimo cha moyo ni muhimu sana, ukishakuwa na uhakika kuwa huna tatizo la pressure/moyo, nenda kwenye kipimo cha vidonda vya tumbo na acid. Usisubiri mpaka upate hela, kama una ndugu, rafiki, kopa au waombe wakusaidie pesa ya kwenda kufanya vipimo. Maisha na afya, havina mbadala.
 
Kipimo cha moyo ni muhimu sana, ukishakuwa na uhakika kuwa huna tatizo la pressure/moyo, nenda kwente kipimo cha vidonda vya tumbo na acid. Usisubiri mpaka upate hela, kama una ndugu, rafiki, kopa au waombe wakusaidie pesa ya kwenda kufanya vipimo. Maisha na afya, havina mbadala.
 
Soon utapata vidonda vya tumbo. Wahi hospital kuvikanili watakupa ushauri mazuri tuu
 
Maelezo ya Bush Dokta ni ya kuzingatia sana. Kwanza anza ni possibility ambayo ni ya hatari zaidi.
Kipimo cha moyo ni muhimu sana, ukishakuwa na uhakika kuwa huna tatizo la pressure/moyo, nenda kwenye kipimo cha vidonda vya tumbo na acid. Usisubiri mpaka upate hela, kama una ndugu, rafiki, kopa au waombe wakusaidie pesa ya kwenda kufanya vipimo. Maisha na afya, havina mbadala.
Asante Hamatan kwa ufafanuzi mzuri zaidi.
 
Wakuu, wataalamu. Nimeanza kuhisi maumivu makali sana maeneo ya chini ya kifua. Ni siku ya tano toka nimeanza kuiExperience. Nimekuwa nikitumia dawa za maumivu kutuliza maumivu.

Kama kuna anayejua dawa inayowesa kunisaidia anisaidie, maana hii hali nasikia wanasema huwa inatibiwa kienyeji, lakini hapa nipo Dar.

Bado natafuta hela ya kwenda hospitalini, ila kama kuna dawa naweza kutumia kwa muda basi naomba mniambia. Maumivu ni makali hasa muda wa usiku.

View attachment 3515552
Duh pole Sana mkuu, naona bush dokta kaelekeza nini ukifanye jaribu utakuwa poa
 
Maelezo ya Bush Dokta ni ya kuzingatia sana. Kwanza anza ni possibility ambayo ni ya hatari zaidi.
Kipimo cha moyo ni muhimu sana, ukishakuwa na uhakika kuwa huna tatizo la pressure/moyo, nenda kwenye kipimo cha vidonda vya tumbo na acid. Usisubiri mpaka upate hela, kama una ndugu, rafiki, kopa au waombe wakusaidie pesa ya kwenda kufanya vipimo. Maisha na afya, havina mbadala.
Mkuu umempa ushauri konki sana.
Maumivu kama hayo aliyapata mtu wangu wa karibu, tofauti kidogo yeye maumivu yalikuwa kushoto chini ya kifua.

Kilikuwa ni kichomi kilichomnyima raha sana.

Kwenda hospitali kuonana na daktari wa magonjwa ya ndani na kufanyiwa vipimo.

Tatizo likaonekana kwenye mishipa ya moyo pamoja na presha ya kupanda na akaanza dose siku hiyo hiyo.

Haya maumivu ya kifua si ya kusubiria mpaka mtu upate hela, ni hatari sana.
 
Mkuu umempa ushauri konki sana.
Maumivu kama hayo aliyyapata mtu wangu wa karibu, tofsuti kidogo yeye maumivu yalikuwa kushoto chini ya kifua.

Kilikuwa ni kichomi kilichomnyima raha sana.

Kwenda hospitali kuonana na daktari wa magonjwa ya ndani na kufanyiwa vipimo.

Tatizo likaonekana kwenye mishipa ya moyo pamoja na presha ya kupanda na akaanza dose siku hiyo hiyo.

Haya maumivu ya kifua si ya kusubiria mpaka mtu upate hela, ni hatari sana.
Sahihi kabisa
 
Wakuu, wataalamu. Nimeanza kuhisi maumivu makali sana maeneo ya chini ya kifua. Ni siku ya tano toka nimeanza kuiExperience. Nimekuwa nikitumia dawa za maumivu kutuliza maumivu.

Kama kuna anayejua dawa inayowesa kunisaidia anisaidie, maana hii hali nasikia wanasema huwa inatibiwa kienyeji, lakini hapa nipo Dar.

Bado natafuta hela ya kwenda hospitalini, ila kama kuna dawa naweza kutumia kwa muda basi naomba mniambia. Maumivu ni makali hasa muda wa usiku.

View attachment 3515552
Unafanya kosa kubwa kudhani kuwa watu wanaweza kugundua kinachokusumbua kwa kubuni. Pia unaweza kuambiwa dawa na ikawa haitibu ugonjwa unaokusumbua ukaishia kupoteza fedha. Jaribu kutumia dawa za kutuliza acid, ikiwa hakuna nafuu kesho nenda kwa dr.
 
Chini ya kifua dalili zavidonda vya tumbo zaman nilizan ni watu wazima ndo wanaumwa ila Kwa Sasa ni Kila mtu
 
Watu wazima kivipi mkuu ? Vidonda vya tumbo haviwapati watoto? Bacteria wa H.pylory hawachagui na wanaambukizwa kwa kasi sana
 
Ni ngumu kujua kinachokusumbua bila vipimo,

Hata stress husababisha hayo maumivu pia,relax mkuu ila fanya ukapate vipimo Hospitali kabla ya kutumia dawa yeyote ile,

Wishing you quick recovery.
 
Upo uwezekano kuwa unasumbukiwa na tumbo kwakuwa hapo kuna msukumo. Chunguza choo chako kama kina hali ya mucus/ kama mlenda au kamas*. Pia kama tumbo linaunguruma, kiungulia, uchungu mdomoni n.k
Kama ndivyo basi badili ulaji wako achana na wali maharagwe kabisa, chips na vyakula junks badala yake mboga za majani, matunda n.k
Punguza kula at least milo 2/day; mlo mmoja mkuu (maybe mchana) na light ( salad + matunda jioni sio usiku.
Acha sukari.
Itakusaidia kipindi unatafuta 🔍 💸 ulipoweka.
 
Back
Top Bottom