Kuhusu Rais kuingilia au kutoingilia sakata la uchaguzi Zanzibar kwa kisingizio cha kutoingilia maamuzi ya ZEC, kwa mazingira halisi yalivyo Zanzibar, nashawishika kusema amepotoka.
Haiingii akilini Rais unatenga pesa ya walipa kodi wa Tanzania wakiwemo Waunguja na Wapemba ukazitumia kumtuma Balozi Mahinga kwenda Burundi kusuluhisha mgogoro uliotokana na uvunjifu wa katiba wa kung'ang'ania madaraka na kuacha kutoa huduma kama hiyo kwa Wazanzibar.
Hapa Rais wangu mpendwa JPM hatusemi uende umtangaze Maalim Seifu au Ali M. Shein. Hatusemi ukasimamie uchaguzi urudiwe, la hasha. Tunachosema ni kwamba, nenda angalia mazingira yaliyofanya Jecha kufuta uchaguzi ni ya kisheria na kikatiba? Kama siyo, hata kama huna mamlaka ya kuingilia uamuzi wa Tume, lakini uamuzi huo ni kinyume cha sheria na Katiba, ndugu yangu, hapo hukwepi, unawajibika kuingilia kwa lengo la Kulinda, kutetea na kuhifadhi katiba kwa kushauri, kushawishi, kuelekeza na hata kuchukua hatua kwa waliokiuka sheria na Katiba.
Chukua mfano: Jecha ahesabu kura Zote Aziweke wazi, halafu amtangaze mwenye kura chache kuliko zote kuwa ndiye mshindi, kweli Magufuli utasema huna mamlaka ya kuingilia suala hilo? Au pamoja na kuto gombea akajitangaza yeye Jecha kuwa mshindi na kwamba yeye ndiye anastahili kuwa Rais, Magufuli kweli utakubali kuwa huna mamlaka ya kuingilia suala hilo? au akiamua kusema kuwa daftari la wapiga kura lote ni feki kweli Rais utakaa kimya kama unavyotuaminisha kwa msingi wa kuiacha tume ya uchaguzi kuwa huru?
Kama tutajitoa ufahamu kufuata dhana ya tume huru, tume huru bila kuzingatia katiba na sheria tutaishia aibu ya mwaka, na tutajuta kuzaliwa Tanzania.
Kama utang'ang'ania ushauri mbovu haya. tutaona!