GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Nimeona nichukue fursa hii adhimu kabisa kuwataja Mashujaa wangu wa kutukuka kabisa kwa mwaka huu unaoisha leo lakini pia nitawataja wale ambao pia naona kwa mwaka huu hawajawa Mashujaa wangu nikiwa na matumaini kuwa kwa wale Mashujaa wangu wataongeza bidii ili wazidi kunifurahisha na wale wasio Mashujaa wangu basi watajirekebisha ili mwakani 2017 watende Kazi zao vizuri na kwa ufanisi.
HEROES wangu kwa mwaka 2016 ni hawa wafuatao:
Hata Wewe Member najua kwa mwaka huu unao Heroes na Non Heroes wako hivyo si vibaya basi na Wewe ukatiririka nao hapa ili tuuage mwaka vizuri ila hakikisha tu wanakuwa Watatu katika kila upande.
OMBI.
Tafadhali mnapowataja hapa hao Heroes wenu Watatu na Non Heroes wenu Watatu naomba MSITUKANE na tuwe na lugha ya staha zaidi na hata kama unapiga dongo basi liwe na Kidiplomasia zaidi ila tusifanye Character Assassination nitawashkuruni sana mkilizingatia hilo.
Zaidi ya hapo sina mengi zaidi ya kusema tu GENTAMYCINE nawatakieni Members wote wa JF Kheri ya Mwaka mpya wa 2017 na naomba uwe wa fanaka na matarajio yenu yafikiwe huku mkipata baraka nyingi za Mwenyezi Mungu ILA nichukue pia nafasi hii kuwaomba radhi / msamaha wale Members wote ambao labda kwa namna moja au nyingine niliwakwaza na wakajisikia vibaya. Yachukulieni tu yale yote kama changamoto kwenu kwani kuna muda mwingine nakuwa ' mtundu mtundu ' ili tu kuweza kuchangamsha ' Jamvi ' lakini sikuwa na nia mbaya na msisahau hata katika Familia lazima kuwe na Mtoto mmoja ' mtundu ' ili Nyumba ichangamke.
Nawapendeni nyote na mbarikiwe sana akhsanteni.

- Rais Dkt. John Magufuli...ameonyesha uthubutu wa Kiuongozi na Kiuwajibikaji.
- Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa...ni Mtu mvumilivu, makini na mwenye dira.
- JF Co Founder and MD Maxence Melo...ni Shujaa wa kweli na mfano wa kuigwa na wengi.
- Waziri Mwigulu Nchemba...sidhani kama mpaka sasa anajua anachokifanya.
- Mchezaji wa Yanga Amis Tambwe...alinisababisha nivunje kiti Taifa kwa kutufunga Simba.
- Waziri Jumanne Maghembe...katupotezea Faru John wetu na bado anatuzuga tu Watanzania.