Nafundisha Lugha ya Kichina

Nafundisha Lugha ya Kichina

Qj_

Senior Member
Joined
Feb 16, 2017
Posts
157
Reaction score
155
(haya maneno mda mwingi tunayatumia unapokutana na mtu)

Hujambo
nĭ hăo 你好

Habari ya asubuhi
zăo shang hăo 早上好

Habari ya mchana
xià wŭ hăo 下午好

Habari ya jioni
wăn shàng hăo 晚上好

Usiku mwema
wăn shàng hăo 晚上好

Jina lako ni nani?
nĭ de míng zi shì shén me 你的名字是什么?

Jina langu ni ___
wǒ jiào ___ 我叫___

Samahani, sijakusikia
duì bù qǐ ,wǒ méi tīng jiàn 对不起,我没听见

Unaishi wapi?
nǐ zhù zài nǎ lǐ ? 你住在哪里?

Unatoka wapi?
nĭ cóng nă lĭ lái 你从哪里来?

Habari gani?
nĭ hăo ma 你好吗?

Nzuri, asante
wŏ hĕn hăo xiè xie 我很好,谢谢

Na wewe?
nĭ ne 你呢?

Vizuri kukutana na wewe
hĕn gāo xìng jiàn dào nĭ 很高兴见到你

Vizuri kukuona
hĕn gāo xìng jiàn dào nĭ 很高兴见到你

Uwe na siku njema
zhù nĭ yú kuài 祝你愉快

Tutaonana baadaye
dāi huì jiàn 待会见

Tutaonana kesho
míng tiān jiàn 明天见

Kwaheri
zài jiàn 再见


kama una swali lolote kuhusiana na lugha yakichina piga cm 0764531080/0718632536 tuma sms ya kawaida au WhatsApp

Frank,B.
tryphonefrank@gmail.com
0764531080/0718632536
mwalimu wa lugha ya kichina
 
unapatikana wapi na ada zako zikoje.unafundisha kwa mda gani.mimi nipo ars
 
😅 nimejitahidi kusoma hayo maneno lkn mwe! Tuwaachie wenye lugha.
 
Kusoma hayo maneno lazima shingo ikakamae kama umebeba kitu kizito.
 
欢迎大家



你们好!nǐmen hǎo!Habari zenu!

Lugha ya kichina (hanyu 汉语/zhongwen中文) ni lugha inayo zungumzwa na watu billion 1.2 sawa na asilimia 16% ya watu wote duniani , lugha ya kichina ni lugha ambayo ina mkangayiko mkubwa sana hasa kwenye matamshi, hichi kitu ndio kinaifanya lugha ya kichina kuwa ngumu sana kwa watu wanao jifunza lugha hii, kwa mfano unaweza kukuta mtu anaye tokea Beijing na mtu anaye tokea jimbo la kusini mwa china wasielewane kutokana na matamshi yao ya maneno ya kichina, hii ni kwasababu lahaja ya Beijing inatofautiana na lahaja hasa ya majimbo yaliyopo kusini mwa nchi ya China. Kutokana na kwamba lahaja ya lugha ya kichina inatofautiana kutoka jimbo mmoja hadi jimbo jingine, hii hali ikawa inasababisha mkanganyiko miongoni mwa wazungumzaji wa lugha ya kichina.

Kutokana na mkangayiko wa kila maeneo hasa majimbo kua na lahaja zao hivyo kulikua na mvutano mkubwa wa lahaja ipi itumike kwa nchi nzima ya China, hivyo basi serikali ya China mnamo mwaka 1949 ikaamua kutumia Beijing dialect (lahaja ya Beijing) hapa ndio tukapata kitu kinacho itwa Mandarin Chinese (mandarin Kichina) au pia watu wengine wanapenda kuiita ‘’mandarin’’ hii ndio lugha ya yaifa ya China, Taiwan pia ni mmoja kati ya lugha nne rasmi za taifa la Singapore , lakini pia Mandarin ni moja ya lugha rasmi kati ya lugha sita za umoja wa mataifa. Lakini Hong kong na Macao wanatumia lugha yao inaitwa Cantonese(hii inaendana na kichina lakini inatoafouti kubwa kwenye upande wa matamshi, lakini pia mandarin kwa sasa watu wengi wanaongea hiyo lugha kwasasabau Macau na hongkong pamoja na kutumia lugha yao inayo itwa Cantonese lakini Mandarin ni lugha ambayo inafudishwa mashuleni.

Hong kong na Macao Kichina wanacho ongea kinaitwa Cantonese mfano watu wanaotokea china mainland neno historia (史)linatamkwa kama shǐ lakini kwa Lugha ya Cantonese linatamkwa sí, hivyo kwa wale mliokua mnazani watu wa hong kong na macau wanatumia lugha moja na watu wa China bara siokweli kwa maana mtu ambaye anatokea Beijing akaenda hong kong hawezi elewana na mtu (namaanisha kutakua na Lugha gongana) labda kama akutane na mtu anayejua kuongea Mandarin/puntonghua (kinchina kinacho ongewa na watu wa china bara ‘’mainland’’)

Kwa wale ambao wanataka kujifunza kichina kwa lengo la kwenda China kusoma au kufanya biashara basi inatakiwa ujifunze mandarin chinese ‘’Putonghua ‘’. Kwa wale wanao taka kupata full schoraship ya kusoma degree au masters kwa kutumia Chinese government scholarship, lazima uwe umefaulu HSK4 (hii ni mitihani ya kupima ustadi wa kuongea, kusoma, kusisikiliza na kuongea lugha ya kichina, hii mitihani unaweza fanyia kwenye tahasisi za lugha ya kichina zilizopo kwenye vyuo kama UDSM, UDOM n.k) hii mitihani inafanana na mitihani ya lugha kiingereza kama vile TOEFL au IELTS.

Mitihani ya lugha ya kichina (hanyu shuiping kaoshi 汉语水平考试 HSK) ina hatua/ngazi (level) sita (6)

HSK1(hii level ina jumla ya misamiati 150 ya lugha kichina)

HSK2 (hii level ina misamiati 300 ya lugha kichina)

HSK3(hii level ina jumla ya misamiati 600 ya lugha kichina)

HSK4(hii level ina jumla ya misamiati 1200 ya lugha kichina)

HSK5(hii level ina jumla ya misamiati 2500 ya lugha kichina)

HSK6(hii level ina jumla ya misamiati 5000 nakuendelea ya lugha kichina)

Hiyo mitihani imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni kusikiliza(tingli听力), kusoma(yuedu阅读) na kuandika(xiezuo写作) lugha ya kichina , pia kuna mtihani wa kuongea lugha ya kichina ambao unaitwa HSKK (hanyu shuiping kaoshi kouyu 汉语水平考试口语)

Lugha ya maadishi ya kichina wanatumia hanzi (汉子)kwasababu kwenye lugha ya kichina hatutumii alfabeti. Kwa kufuata mfumo wa kijifunza lugha ya kichina kwa wageni ‘’foreigner’’ inatakiwa ujue hanzi 300 kwa hatua ya chini (beginer level). Hivyo kwa wale mnao taka kuanza kujifunza lugha ya kichina mnatakiwa mlifahamu hilo, kwenye kaundika hanzi kunachangamoto kubwa hivyo jitahidi uwe unafanya mazoezi ya kuandika mara kwa mara vinginevyo hutaweza kuandika Chinese character kwa ufasaha mkubwa.

Lakini kwenye spoken Laguage wachina wanakitu kinaitwa Tone (shengdiao声调), hii ndio hutumia kutofautisha maneno (hapa ndio ulipo ugumu wa kuongea lugha ya kichina ), Lugha ya kichina ina tone(toni) nne (4) lakini kwa sehemu ya maeneo ya kusini mwa china wanatumia tone 6 hadi 12, lakini Mandarin Chinese (Putonghua 普通话) kuna tone 4 ambazo ni toni ya kwanza,toni ya pili , toni ya tatu na toni ya 4

Mfano wa toni nne za lugha ya kichina

1.Mā 2.Má 3.Mǎ 4.Mà

Katika kutamka hayo maneno inabidi uwe makini sana kwasababu ukikosea tu tone basi unakua ume maanisha kitu kingine kabisa

Kwa leo tutaanza kwa kujifunza salamu za lugha ya kichina

Habari – Nǎ hǎo 你好!

Habari za asubuhi – zǎoshàng hǎo 早上好!

Habari za mchana – zhōngwǔ hǎo中午好!

Habari za usiku – xiàwǔ hǎo 下午好!

Kama una swali lolote comment hapo chini na mimi nitakujibu.

Pia kwa wale wanaotaka kujifunza kichina au kikorea nina online class kwa bei nafuu kabisa

Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi au kama unataka mafunzo binafsi ya lugha ya kichina wasiliana nami.

tryphonefrank@gmail.com

0764531080

Frank, B.R.

郝铭
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom