Muungano kama yalivyo Mapinduzi ya Zanzibar ni michakato iliyoshirikisha MIKONO pengine na MIDOMO mingi lakini ROHO na VICHWA vya haya ni vichache,yaani nikimaanisha malengo ya watu kama NYERERE, KARUME,BABU,KAWAWA,na THABIT KOMBO,nikitaja wachache.Kwa miaka mingi utafiti, na majadiliano ya kisomi kuhusu muungano mara nyingi ikiepukwa kwa woga ama ukifanyika kwa upotoshaji.
Yafaa mwalimu uutafiti muungano upate vyanzo vya kutosha kuuelewa.Watoto wa kidato cha pili yawatosha kuujua kama mfano wa jitihada za bara hili kutafuta nguvu kubwa kiuchumi,kiulinzi,kisiasa na hata kiutamaduni,
Vyovyote utawasilisha kuwa umegundua muungano huu siyo wa kawaida,utagundua pia haujakamilika wala kuzeeka, pia utagundua kuwa hata wewe ulidanganywa shuleni pia lakini utawapa wanafunzi wajue ulikotoka ,ulipo sasa na mwelekeo!hiyo yatosha,maana mwalimu unatoa 25% wanafunzi wanatafuta 75%