Nafikiria Kuifunga Biashara yangu

proxy

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
1,468
1,329
Hello wanajamvi wenzangu naomba kuuliza hivi ukiwa na Leseni ya Biashara na Tin namba ,ikatokea unataka kuifunga Biashara ili ufanye mambo mengine ,je umiliki wa hivi vitu unakuwaje ,Leseni na Tin namba zitakuwa zimefungwa au zitaendelea kuwepo?
 
Andika barua ya kufunga biashara ipeleke tra....

Wataifanyia kazi kwa kuangalia kama una deni mf katika mwaka wa kodi 2018/2019 kama hujamaliza kulipa installment zako kulingana na kodi uliyokadiriwa inabidi uzilipe.

Then wataifunga na watakubadilishia tin kutoka ya biashara kuwa for non business use

Utapewa barua ya kuonesha ombi lako limekubaliwa itunze hiyo.
 
waandikie barua TRA ya kufunga biashara yako, ila hakikisha huna madeni ya nyuma ya kodi na kama yapo lipa,

hii itakusaidia kutoendelea kuhesabiwa kodi ilihali ulisha acha biashara.
 
Nipo sasa hivi nalipa Installment kama kawaida ,na kama nikitaka kuandika hiyo barua inatakiwa nisubiri mpaka mwaka uishe au naweza andika hata sasa hivi na wakalifanyia kazi?
Andika sasahivi haina shida kikubwa usiwe na deni
 
Kufunga biashara ni moja ya maamuzi ya busara......biashara haikupi faida ifunge usilazimishe kuonekana unafanya biashara fulani kumbe hupati kitu......maana ya biashara ni lazima kuwe na faida ndani yake.

Nilipofunga biashara ya duka la vifaa vya ujenzi leo hii naona nilifanya maamuzi sahihi na magumu pia maana wadau (wateja, marafiki, vibarua, mlinzi,tra walitaka niombe muda kidogo.....)walitaka niendelee.

Ushauri wangu kwako mkuu kama biashara haina faida IFUNGE usisubiri KUFILISIKA na MADENI juu.....

Karibu kwenye ufugaji.........
 
ulichofanya wewe ndicho hicho hicho nilichofanya mimi mkuu, wafanyabiashara wenzangu wananiambia ni bora yangu mie niliefunga biashara
 
JIWE akiisoma hii posti atasema huyu alikua mpigaji na mkwepa kodi sasa baada ya mianya kuzibwa kaamua kufunga biashara....

Mdau pole sana.
 
Kupitia swali lako na kutaka ufafanuzi juu ya kufunga biashara, umesaidia sana kupata elimu nini cha kufanya kabla ya kufunga biashara, wapumbavu wachache watahisi labda ulikuwa unakwepa kodi.
 
ulichofanya wewe ndicho hicho hicho nilichofanya mimi mkuu, wafanyabiashara wenzangu wananiambia ni bora yangu mie niliefunga biashara
Mkuu ulifanya cha maana unaweza kukomaa ukafa na tai shingoni kuna mwana wameuza nyumba yake kisa madeni biashara anaendesha kwa hasara.....mtaji ukipungua anakopa ku boost situations.
 
Ukimalizana na tra nenda Halmsahauri(Halmashauri ulipochukua leseni) pia ifunge leseni.....Japo Halmsahauri hawana nguvu kama tra coz tra ni country wise kaifunge tu hiyo leseni kama unayo.

Ikiwa utataka kurudi katika biashara hiyo, eneo hilo hilo ukataka kuifufua hiyo leseni lazima ukutane na deni.

NB: Mfumo wa Halmsahauri hauna nguvu sana......

Utaratibu ni kama ulivyofanya tra.
 
roho yang
Mkuu ulifanya cha maana unaweza kukomaa ukafa na tai shingoni kuna mwana wameuza nyumba yake kisa madeni biashara anaendesha kwa hasara.....mtaji ukipungua anakopa ku boost situations.
u inaniniuma sana mkuu, hadi namkumbuka rais wa awamu ya nne
 
roho yang

u inaniniuma sana mkuu, hadi namkumbuka rais wa awamu ya nne
Maisha lazima yaendelee ndugu hakuna namna yule bilionea aliyejipiga risasi mwaka jana baada ya shehena yake ya viroba kukamatwa biashara yake imeyumba zaidi, alimuacha mke wake,watoto.....

Nikipita ktk hilo duka najifunza mengi, kiuchumi nimeyumba ila najua kuna watu wanafurahi bado ninaishi furaha yao haijakoma kwasababu siingizi kipato kama mwanzo.

Japokuwa sometimes kuna vitu vinaumiza inabidi tujifunze na kuukubali ukweli kuna watu furaha yao mafanikio yanahitaji Uwepo wetu....

Chagua kuendelea maisha
 
Pole sana japo hujasema sababu za kufunga ila bila shaka ni huu upepo.
Wafanya biashara wanalia wahubiri kina Hivi punde kila siku wanadis kuajiriwa.

Ngoja nifanye tu kufata ule msemo, "za kuambiwa changanya na zako"
 
Back
Top Bottom