mkandaboy
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 257
- 89
Habari zenu wana JF? Naomba ku-share nanyi machungu ambayo TIGO wamekuwa wakinisababishia. Nimekuwa mteja mwaminifu wa kampuni hii tangu mwaka 2000 (enzi hizo ikiitwa BUZZ). Kiukweli nimefurahia sana huduma zao tangu wakati huo mpaka mwaka jana na sasa nafikiria kuchukua maamuzi magumu ya kuachana nao nihamie kwingine. Sababu kubwa ni hizi;
1. Wamekuwa wakinipora airtime kila mara ikitokea nimeongeza salio na sijalitumia kwa wakati huo. Kwa mfano naweza kuweka salio la sh 2,000/. Baada ya robo saa tu unakuta sh 500/ au zaidi imepungua, bila kupiga simu wala kutuma sms. Au napiga simu dakika nne tu wanachukua sh 1,000/. Ukipiga simu kuuliza wanaku-hold on hata robo saa na mwisho simu inakatika (au labda wanakata-sijui?).
2.Niliwahi ku-subscribe huduma ya kutumiwa ratiba na matokeo ya ligi mbalimbali za mpira wa miguu (mfano ya Uingereza, Uhispania). Huduma hiyo nimekuwa nikiipata vizuri. Imefikia wakati sasa nataka kujitoa kwa utaratibu ule ule walionielekeza wakati najiunga lakini wananing'ang'ania mno. Kila nikituma sms ya kujitoa wanaipokea lakini hawatekelezi ombi langu. Nikiwapigia simu yale yale ya kusubirishwa robo saa bila msaada.
Vipi wana JF wenzangu nanyi mmeshakutana na madhila kama hayo yangu? Kiukweli kabisa nafikiria kuachana na kampuni hii...