Nafikia uamuzi wa kuvunja ndoa jamani!Naombeni ushauri wenu wenzangu!

mazoea ni mabaya sana sasa ndugu wanakuja ukumbini bila kadi walitegemea nini na harusi za siku hizi,pesa kwanza.....endelea kuvumilia yakikushinda nenda kwa baba paroko.....

Inategemea,ni mambo ya kawaida yanayotokea nafkiri busara ingetumika kwa paroko tulishaenda habadiliki
 
Dada meneno yako yanadhihirisha upendo ulio nao kwa mume wako, endelea hivyo hivyo usichoke mungu atakubariki mpendwa

Nashukuru kaka ni kweli nampenda sana ila napata mitihani sana,sasa ngoja tu nitulie kwa muda siku akijirekebisha haya.
 
Nakushukuru sana kwa kunisisitiza hilo kwani nilifika mahali nikakata tamaa kuliombea.

usikate tamaa dada....magumu yapo katika safari yoyote ya hapa duniani.......amini tumaini lipo kutoka kwa Mungu ....mana Mungu anayarahisisha magumu yote ukimtegemea yeye.......
 
Asante sana my dear mahipsi baby napata kitu kikubwa kupitia ushauri wenu nilikua nimekata tamaa kabisa.
 
Ndoa ndivyo zilivyo Dada. Amua kuvumilia uishi naye uonekane upo kwenye ndoa au amua kutoka kabisa. Life ndiyo hii hii hairudi tena.. Ukiishii kwa mateso ndani ya ndoa hata life span yako inakuwa fupi. Wengine walitoka wa kawa happy wengine wakapata shida zaidi ya walizozikimbia.
Wewe ndiye uliyevaa hivyo viatu, sisi hatujui ni jinsi gani vinakuumiza. Kazi kwako
 
Kuolewa na mume ambaye hana msimamo dhidi ya nduguze wanaotaka kuvuruga ndoa yake kwa namna moja au nyingine ni kazi kubwa sana. Endelea kuvumilia lakini yakikushinda funga virago vyako maana hata uvumilivu pia hufikia kikomo. Ukomo wa kuvumilia ukifika na kuamua kuendelea kuwemo ndani ya ndoa kama hii basi unaweza kupata mkanganyiko wa akili ambao unaweza kabisa kukuathiri kwa miaka mingi ijayo. Kila la heri.
 
ndelekio pole sana

Ninachoona hapa nyie wawili mna mitizamo miwili inayokinzana kuhsu maisha ya ndoa,. mmoja anaona kuwa umeolewa na ukoo mzima, wakati mmoja (wewe) ngependa ndoa yako muwe wewe na mumeo, muwe na maamuzi yenu na msiyumbishwe na ndugu wa upande wowote ule. Thats how I also live....

sasa kama mmeshafika hadi kanisani, hebu jaribu kujichunguza, kwa nini haipiti wiki kuna maugomvi? kumbuka ugomvi haupaswi kuwa sehemu ya maisha ya kila siku! huenda pengine umekuwa mbishi sana? sio mtii? unajibizana naye? Unaonaje ukianza kuwa mpole, msikivu, fanya kila atakachokuambia, bila kumbishia uone kama mwenyewe hatabadilika! hii ya kupelekana kanisani sijui kwa matron, inazidi kukuza tatizo. matatizo yenu mnayamalizia chumba cha kulala, hayatakiwi yafike sebuleni!

kwenye harusi hayo ya kutokuelewana kwenye sherehe ni ya kawaida, hayapaswi yabebwe hadi kwenye fungate na baadaye maisha yenyewe!
 
Last edited by a moderator:
Kwanza kabisa pole ila siku zote lazima mtu ujiandaye kwa maisha yajayo na mikikimikiki yake, hapo kuna suala dogo sana ambalo wote wawili mnalo na kuindoa hiyo tofauti yenu nikujishusha kwanza, maana fahari wawili hawakai zizi moja. kwa sababu siku ya harusi yenu kulitokea tatizo la kuzidisha watu upande wenu Bibi Harusi, hapo hukupaswa kumlaumu bwana Harusi wala familia yake, kwa sababu hawakuwa na kosa ila ilibidi uilaum familia yako, familia yako ilionyesha dharau. Bwana harusi naye anaona uko upande wa familia yako kwa sababu unaitetea naye lazima aitetee familia yake kwani haikufanya kosa lolote. Onyesha kuwa mpenda haki mkalishe mumeo kwa kumwambia kuwa sasa umejua kosa la familia yenu, na pia anzaneni maisha mapya yenu wawili , maana hapa naona wote mnategemea ndg zenu kuiongoza ndoa yenu
 
ndelekio pole sana

Ninachoona hapa nyie wawili mna mitizamo miwili inayokinzana kuhsu maisha ya ndoa,. mmoja anaona kuwa umeolewa na ukoo mzima, wakati mmoja (wewe) ngependa ndoa yako muwe wewe na mumeo, muwe na maamuzi yenu na msiyumbishwe na ndugu wa upande wowote ule. Thats how I also live....

sasa kama mmeshafika hadi kanisani, hebu jaribu kujichunguza, kwa nini haipiti wiki kuna maugomvi? kumbuka ugomvi haupaswi kuwa sehemu ya maisha ya kila siku! huenda pengine umekuwa mbishi sana? sio mtii? unajibizana naye? Unaonaje ukianza kuwa mpole, msikivu, fanya kila atakachokuambia, bila kumbishia uone kama mwenyewe hatabadilika! hii ya kupelekana kanisani sijui kwa matron, inazidi kukuza tatizo. matatizo yenu mnayamalizia chumba cha kulala, hayatakiwi yafike sebuleni!

kwenye harusi hayo ya kutokuelewana kwenye sherehe ni ya kawaida, hayapaswi yabebwe hadi kwenye fungate na baadaye maisha yenyewe!

Kaka heshima yako!!!!!!

Akisema mkubwa wadogo tunatingisha vichwa kukubali!!!!!

Hapo niongezee moja tu kaka mkubwa kwa ridhaa yako;ASIONGEZE MTOTO KATIKA HALI YA SINTOFAHAMU HIYO
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru kwa ushauri my dear ila jamani,mbona naona hatutafika?yani wiki haipiti hatujakwazana na nisiposolve mimi tutanuniana tuu,yani hadi kanisani tulishaenda lkn hakui wakati ana miaka 35.

Dada wakat mwingine kwenye ndoa unapoona mwenzio habadiliki basi inakubid wewe ubadilike for him.
Kwanza je wamtegemea mumeo kimapato 100%? If yes then its real hard kwa nitakachoenda kukushauri.kama humtegemei yeye kimapato basi fanya hivi,muheshimu kama mumeo,usimuonyeshe dharau yeyote,ila mu-ignore.usihangaike kununa au kukasirika pale anapokukosea,usipigizane naye kelele,wewe fanya mambo yako na mwanao kisha lala zako kimyaa! I tell u,hakuna kitu wanaume wanahangaika kama akiona hapapatikiwi au kunyenyekewa...itamgusa sana na atatafuta suluhu yeye.huwa tunasema unamuazibu kimya kimya.
Kama wewe huwa ni muongeaj sana anapokosea jamaa,basi jitahid akikikosea na ukijisikia kuropoka kunywa maji,usimeze yashikilie mdomon tu...try that na utanambia vile imesaidia.
 
Mimi ni mwanamke wa miaka 28,nilipendana na mpenzi wangu tukapata mtoto kabla ya ndoa na baada ya muda tukafunga ndoa,Sitaisahau siku ya ndoa yangu kwani ilikua siku mbaya maishani mwangu,upande wa mume wangu ulionesha dharau kwa upande wangu,kwani waliwazuia kuingia ukumbini kisa walizidi watu wawili.
Bora wangeniuliza kaka,niliwaoma watoe nafasi 30 kutokana na hali ilivyo cha kushangaza walitoa 20 na matusi juu,na waliokuja wote walikua ndugu wa karibu sana na walisafiri mbali tu.Mume wangu sikumjua vizuri coz kikazi tupo mbali kabisa so nilikua siishi naye.

ndelekio #8



Siku ya Harusi huwa si ajali na inaoneka ulikwisha pewa Kadi ya Watu 20 tu hao wengine 2 umewatoa wapi ! na kwani usimwarifu mwenza wako kabla ya kuja Ukumbini!

Yaani wewe kuzuiwa ndugu zako nje si kitu kidogo lakini unasahau kuwa shuguli za Harusi zinaenda na mahesabu na naunakuja na watu 2 extra alafu huoni kama ni kuharibu shughuli mzima?Acha hizo ulifaa kuwa wa kwanza ku- apologize!



Nakushauri uondoe hiyo sumu ya siku ya Ndoa ndani moyoni mwako na wa mwenza wako maana inaoneka wote kwa pamoja hiyo ishakuwa Sumu kaaeni chini musameheane!.


Kiukweli unawezaona ni jambo dogo lakini liliniuma sana kwani nilianza kuwasoma ndugu wa mume,nililia sana,baadae waliwaruhusu kuingia ukumbini wakati nao walishakasirika na kutaka kuondoka,baadae walitumia busara wakaingia,kiukweli wazazi wangu walikerwa sana na kitendo hicho,then upande wa mume haukuona kama ni kosa wala hawakutafuta suluhu na hata hawakuwakaribisha kwao kama ilivyo desturi yetu.
Nilivumilia kwakuwa nilikua nampenda sana mume wangu,na niliwaza mwanangu ataishije.Ila mume wangu naye aliwatetea ndugu zake,tulipohitilafiana alikua ananisema na nduguze.



Ushauri unautoa kwa ndugu zako au !
Maana mlolongo wa mgogoro chanzo toka ya siku ya Harusi kwa mujibu wa maelezo yako na inaonekana Ndugu zako wanaendelea kukujaza pumba!
Na mbaya zaidi inaonekana kila kukijitokeza matatizo wewe/wanawake wengi midomo yao haina breki(Jamani wale wenye midomo misafi naomba radhi) kazi ni kuanzisha mashambulizi kwa yaliyopitwa hata miaka mitano, hali kama hiyo usitegemee binadamu wenye kufikiri atakuelewa sawa sawa. Kwa hiyo angalia kama kuna hiyo tabia achana nayo kabisa ni sumu katika maisha ya wawili.


Tatizo kubwa tangu tufunge ndoa ni migogoro daily,sijawahi kuona furaha ya ndoa,ila nimegundua mume wangu ni mtu asiyejitegemea kimawazo(anategemea ndugu),hana msimamo,anaamuliwa mambo yake ya familia na ndugu zake,hawezi kabisa kusolve issue au conflict ndogo zinazotokea ktk family,ni mbinafsi sana na hana mawazo ya kiutu uzima.Nilijaribu sana kumshauri mambo mengi lkn anarudia yaleyale,jamani ninampenda sana mume wangu hana tabia za wanawake lkn mbona naona nashindwa?


Dada ndugu zako/wazazi waharibu nyumba yako au familia yako anza kuchukua hatua!

Mzazi wangu m1 amefikia hatua ya kuniambia nikienda kwa huyo mwanaume mimi sio mwanae lakini yote ni sababu ya madharau ya huko kwao'naombeni mnishauri,nivunje ndoa?Kama hujaelewa mahali uliza plz.
 
hapo hautasolve kwa kuvunja ndoa mumeo ka ni mtoto wa mwisho ndivyo walivyo. cha kufanya simama kwenye nafasi yako sawa sawa yeye mwenyewe atajiobea aibu.

pia mambo madogo usimuulize kwa sababu awezi kukusaidia.
 
Nafkiri hujanielewa vizuri lkn nilishayaeleza yote unayoniponda nayo ila amini maswala ya ndoa ni magumu mno,na hapa nipo njia panda.

Ukweli mgumu, ndoa matatizo mengi kuwa makubwa uanzishwa mara nyingi na matatizo madogo.

Umesema mwenyewe siku ipi ndoani ilikuwa mbaya sasa unazani sijakuelewa?

Ukweli hautaki kukubali familia yako ilichemsha na umekuwa na chuki nao since, unazani kama wamejua na kukusoma watakuachia?

Kama umechoka nenda ukale maisha unayotaka ya u single mother, kama ungekuwa na matatizo makubwa rohoni zaidi la siku ya ndoa ungemwagiga kirahisi humu wakati unaeleza ila ndio hivyo.
 
Mpaka unatia huruma ndugu yng vp mlshajarbu kuwatumia watu wazma waheshima kwaajl ya kutafuta resolution dadaa
 
Asante rafiki lakini ni ngumu sana,yeye hana ushirikiano wwt,mnayaongea kesho ni yaleyale,kiukweli nimekata tamaa ingawa naumia.

Ndoa za waswahili bana kwa hiyo walibebana wawili kwani kadi za mwaliko mlipewa ngapi? Kwa nn hamkulipia 2 kama wanavyo fanya wenzenu acha uswahili ndo maana ndoa inakushinda.
 
ndelekio fanya ufanyalo,mshawishi mumeo iwezekanavyo kwanza wazazi wako waende kwao kama ilivyo desturi. Sababu umeshaisoma familia na mumeo, tumia busara. Ndoa ziko hivyo.

Wewe ni mpambanaji, nakuaminia
 
Last edited by a moderator:
Nilifikiri umenyimwa dudu!!!! mbona unalalamika upuuzi shosti hebu nisogee pembeni unantia' joto mie
 
Back
Top Bottom