Aisee kuna haja ya kufanya utalii wa ndani kwnye huu mkoa wa Manyara,niliwahi kupita njia ya Singida kwenda Arusha nikitokea Mwanza kile kipindi barabara ni ya vumbi na tulitumia siku 3 kutoka Singida hadi Arusha kupitia Babati,sasa nataka nijipange niende,Babati,Mbulu,Hanang,Kiteto(huku sikupendi kuna ukora sana,wamasai wa Kiteto wao jibu ni sime tu),kwa Ole Sendeka(Simanjiro) nako kuna Wamasai wakora ,huko nako jibu ni sime tu,halafu Ngorongoro na Karatu ,nadhani nikiwa na 3m itatosha,huu mkoa unaonekana una mambo mengi ya kuvutia lakini washika dau wamelala usingizi wa pono.