Nafasi za kazi Halmashauri ya wilaya ya Ngara

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,438
1,387
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA WILAYA YA NGARA



Unapojibu tafadhali taja:


Kumb. Na. EB.89/286/02/19 12/04/2021
YAH: TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara anawatangazia nafasi za kazi Wananchi wote wa Tanzania wenye sifa za kuajiriwa kama inavyoonekana hapa chini:-

Mtendaji wa Kijiji Daraja la III nafasi 02

Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II nafasi 01


1.1 Sifa za kuajiriwa – Mtendaji wa Kijiji Daraja la III - Mwombaji anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:-
  1. Mwenye elimu ya Kidato cha Nne (K.IV) au sita (K.VI).
  2. Mhitimu wa Mafunzo ya Astashahada/ Cheti katika moja ya fani za
  3. Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii, Mipango na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinacho tambuliwa na Serikali.

1.2 Majukumu ya Mtendaji wa Kijiji Daraja la III - Mwombaji atakayefaulu/ atakayekidhi vigezo na kuajiriwa atatekeleza majukumu yafuatayo:-

  1. Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
  2. Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na Mali zao; na kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
  3. Kuratibu na Kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji.
  4. Katibu wa Mikutano/Vikao na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
  5. Kutafsiri na Kusimamia Sera, Kanuni, Taratibu na Sheria za Nchi.
  6. Kuandaa Taarifa za Utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha Wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali pamoja na kipato binafsi.
  7. Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji.
  8. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji.
  9. Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalamu waliopo katika Kijiji.
  10. Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya Wananchi.
  11. Kusimamia utungaji wa Sheria ndogondogo za Kijiji.
  12. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.

1.3 Mshahara – Ngazi ya mshahara itakuwa ni TGS/B/1


2.1 Sifa za kuajiriwa- Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II Mwombaji anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:-
  1. Mwenye elimu ya Kidato cha Nne (K.IV) au sita (K.VI).
  2. Awe na cheti cha Astashahada ( Technician Certificate-NTA LEVEL 5) cha utunzaji wa kumbukumbu katika mojawapo ya fani za Afya, Masijala, Mahakama au Ardhi. kutoka Chuo cha kinachotambuliwa na Serikali.

2.2 Majukumu ya Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II – Mwombaji atakayefaulu/ atakayekidhi vigezo na kuajiriwa atatekeleza majukumu yafuatayo:-

  1. Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/Mafaili yanayohitajika na wasomaji.
  2. Kuthibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/Nyaraka.
  3. Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/Nyaraka katika makundi kulingana na somo husika (Classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya Ofisi.
  4. Kuweka/kupanga kumbukumbu, Nyaraka katika reki (Fail racks/cabinets) katika masijala/vyumba vya kuifadhia kumbukumbu.
  5. Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka n.k) katika mafaili.
  6. Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.

2.3 Mshahara – Ngazi ya mshahara itakuwa ni TGS/B/1


MASHARTI YA JUMLA KWA MWOMBAJI:-


  1. Awe ni Raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 45
  2. Awe Mtanzania Me/Ke mwenye akili timamu
  3. Barua za mwombaji ziambatishwe pamoja na Vivuli (Photocopies) vya vyeti vya taaluma, ujuzi, kuzaliwa na picha mbili (2) (Passport size) za rangi za hivi karibuni bila kusahau maelezo binafsi (CV) yanayojitosheleza yakionyesha anuani kamili za Wadhamini watatu (3). Namba ya simu ya Mwombaji ni muhimu na iandikwe katika barua ya maombi ya Kazi chini ya anuani yake.
  4. Waombaji waliosomea nje ya nchi waambatishe uthibitisho wa Vyeti vyao kutoka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).
  5. Maombi yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili/Kiingereza.
  6. Kwa waombaji ambao tayari wameisha ajiriwa/ walishawahi kufanya kazi Serikalini na kuacha kazi, wafanyakazi wanaotoka kuhama kada wanashauriwa kuzingatia utaratibu wa uhamisho au kurejea katika Utumishi wa Umma baada ya kuacha kazi kama ilivyoelekezwa katika Waraka Na. CCB.228/271/01 wa tarehe 07/08/2012.
  7. Awe hajawahi kutiwa hatiani kwa makosa ya Jinai.

Hati za matokeo ya kidato cha Nne na Sita (Statement of Results) hazitapokelewa.

Maombi yote yatumwe kwa anuani ifuatayo:-

Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Ngara,
S.L.P. 30,
NGARA.


Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 25/04/2021 saa 9:30 alasiri.

LIMETOLEWA NA;
MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA NGARA

S.L.P 30, Ngara, Simu:028 2226016, Nukushi:028 2226152, Barua pepe:ded@ngaradc.go.tz, Tovuti: www.ngaradc.go.tz
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom