Nafasi za Kazi, Halmashauri ya Jiji Arusha

Nafasi za Kazi, Halmashauri ya Jiji Arusha

karibukwetusingida

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Posts
290
Reaction score
138
NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA - 8/25/2014

Kutoka Mwananchi 25 August

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wakufanya kazi kwa mkataba kwa
masharti yaliyoainishwa kama ifuatavyo:-

Mtunza Bohari: Nafasi (1)


Sifa za waombaji:

  • Awe na stashahada ugavi
  • Ama cheti cha form IV na form VI
  • Awe na passport 3
  • Awe na Barua ya U dhamini

Majukumu


  • Kutunza ghala la vifaa
  • Kupokea vifaa vipya vitakavyoletwa
  • na wazabuni mbalimbali
  • Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji wengine
  • Kuandaa hati za kupokelea vifaa
  • Kufungua na kutunza "Bin Card"kwa kila kifaa kilichopo ghalani

Watakaofaulu usaili watalipwa mshahara utakaokuwa umeainishwa kwenye mkataba ya ajira hii.

Afisa Manunuzi Msaidizi Nafasi (2)


Sifa za mwaombaji:


  • Awe na stashahada ya manunuzi au ugavi
  • Ama cheti cha form IV au form VI
  • Awe na passport size 3
  • Awe na Barua ya Udhamini

Majukumu


  • Kuaandaa mpango wa manunuzi na kukusanya takwimu za vifaa vinavyohitajika
  • Kukusanya na kutunza takwimu za utendaji za wazabuni mbalimbali
  • Kusimamia utunzaji wa maghala na hati
  • Kusimamia upokeaji,utunzaji na usambazaji wa vifaa ghalani
  • Kuhesabu na kutoa taarifa ya thamani ya vifaa vilivyomo ghalani kila mwisho wa mwaka

Afisa Mtendaji wa Kata II: Nafasi (12)


Sifa za mwombaji


  • Awe na Shahada ya moja ya fani zifuatazo:
  • Uongoziwa Utumishi, Rasilimali watu, Sosholojia, Sheria na fani nyingine zinazofana na hizo
  • Awe na Cheti cha fomu N na VI
  • Wasifu wake (CV)
  • Barua ya Uthamini
  • Passport size 3

Majukumu


  • Kuandaa mpango kazi wa maendeleo wa Kata na kuwasilisha kwa Mkurugenzi wa halmashauri
  • Mhamasishaji wa umma katika mikakati ya uzalishaji mali ili kuondoa njaa na umaskijni
  • Kutafasri na kusimamia utekelezaji wa sera,sheria ,kanuni na miongozo ya serikali
  • Kupanga mikakati ya kuzuia na kukabili majanga katika kata

Afisa Usalama nafasi (2)

Majukumu ya kazi

  • Kusimamia mifumo ya ulinzi na usalama katika maeneo na mali za Halmashauri
  • Kuripoti katika sehemu husika kuhusiana na hali yeyote ya wizi
  • Kushughulikia matatizo ya watu yanayohusiana na ulinzi na usalama kama kuandika taarifa zao na kuzipeleka sehemu husika
  • Kusimamia uingiaji wa wageni na magari katika majengo ya Halmashauri
  • Kufanya ukaguzi kwenye vituo vya ulinzi
  • Kutekeleza majukumu yote kama atakavyokuwa amepangiwa na mkuu wake wa kazi

Sifa za Mwombaji


  • Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha nne au cha sita.
  • Awe mstaafu wa Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania au Jeshi la kujenga Taifa
  • Mwenye uzoefu wa kutumia silaha za mota
  • Umri usiozidi miaka 40 isipokuwa kwa wastaafu wa jeshi la polisi/ Jeshi la Wananchi (JWTZ) na awe amepitia mafunzo ya masuala ya Usalama (security)
  • Awe hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la jinai ndani na nje ya kazi alizowahi kuzifanya.
  • Awe na vyeti sahihi vya Elimu yake
  • Awe na vyeti/cheti/barua ya kustaafu kwake na asiwe alifukuzwa kazi.
  • Aeleze ana mke/mume na watoto wangapi, wako wapi na wanafanya nini.
  • Awe raia wa Tanzania.

Waombaji wote waliokidhi vigezo watume maombi yao kwa:-

MKURUGENZI WA JIJI
S.L.P.3013, ARUSHA

MWISHO WA KUTUMA MAOMBI NI SIKU 14 TOKA TAREHE YA KUTANGAZWA KWA NAFASI HIZI KWENYE GAZETI HUSIKA.

IMETOLEWA NA:
J.A.R.IDD
Mkurugenzi wa Jiji Arusha
 
ahsante ila naumia kusoma kutokana mpangilio ngoja ninunue gazeti la mwanainchi
 
Asante kwa isu ila kwa yeyote anayejua tujulishane,hapo anaposema Mthamini maana yake ni nn? Au ni ka nilvyoelewa mdhamini?
 
Barua ya uthamini ndio ipi hio na inatoka kwa nani?

kuna bint kaniuliza hii uthamini ni kitu gani nlikua sijaelewa nlivogoogle nikakutana nayo huku JF kama kuna mtu anajua maana yake awasiadie vijana hawa jaman wasikosee..binafsi nilidhani ni udhamini kumbe sio?
 
Kwa kweli neno "Barua ya mthamini" imefanya watu waumize vichwa hata me nimegoogle nikauliza mwisho nimepata jibu ambalo yeyote aweza kulisahihisha,
1. Barua ya Uthamini ni RECOMENDATION LETTER au INTRODUCTION LETTER, ambayo mtu anaweza kuipata kwa Afisa mtendaji wa wa mtaa au kata yake au Kiongozi wake wa Chama n.k

Yeyote anaweza kunisahihisha
 
barua ya mdhamini inaandikwa na nani, referees au mtendaji kata
 
barua ya mdhamini inaandikwa na nani, referees au mtendaji kata

Kama ni mdhamini,inaandikwa na mdhamini wako mmoja kati ya wale 3 na sio mtendaji kata .mtendaji kata anaandika barua ya utambulisho kua wewe ni mkazi wa eneo fulani
 
Kwa kweli neno "Barua ya mthamini" imefanya watu waumize vichwa hata me nimegoogle nikauliza mwisho nimepata jibu ambalo yeyote aweza kulisahihisha,
1. Barua ya Uthamini ni RECOMENDATION LETTER au INTRODUCTION LETTER, ambayo mtu anaweza kuipata kwa Afisa mtendaji wa wa mtaa au kata yake au Kiongozi wake wa Chama n.k

Yeyote anaweza kunisahihisha

Barua inayotakiwa ni ya Mdhamini na si Mthamini...... Yaani mtu ambaye atakuwa kama referee au mdhamini.....
 
Back
Top Bottom