Nafasi ya Vyuo vikuu katika Serikali ya Magufuli na Tanzania tunayoitaka

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,188
7,490
“Ifike mahali kila mtanzania licha ya tamaa zake za kimaumbile aseme hiki sikichukui kwa kuwa si stahili yangu na hiki sikifanyi kwa kuwa kwa hadhi na nafasi yangu si sitahili kukifanya licha ya kukitamani.Akili yake imtume hivyo hata kama hakuna mtu atakayemuona. Hata hivyo hilo litawezekana tu kama tutawekeza kwenye kubadili fikra za jamii ya kitanzania ambayo tayari imeathirika vibaya!”

Tatizo la Tanzania kwa zama hizi, si ukosefu wa utaalam bali kukosekana kwa uadilifu na uaminifu miongoni mwa waliowengi kutokana na kushindwa kudhibiti tamaa za mwili. Kwa kuwa tamaa katika hatua yake ya juu kabisa, humfanya mtu asitumie akili ya kichwani, wenye elimu kwa wasiokuwa na elimu wamekuwa wakileta maafa sawia.”

Mtu anaweza kufikiri tofauti kwamba shida ni ujuzi na utaalamu,pengine ni nene kwa mifano ili iwe rahisi kueleweka. Profesa mwenye Phd, analala na mwanafunzi wa kike ili amfaulishe, Dereva aliepewa lori la mafuta apeleke Zambia anauza mafuta njiani anachoma gari moto, fundi gari anadai kifaa kimeharibika inabidi kifungwe kingine halafu ukigeuka nyuma anakuambia tayari keshaweka kingine kumbe kapuliza vumbi kilichokuwepo. Cashier wa benki anakupa mil.3, anakupa chenji za elfu2, unahesbu unachoka unaacha kumbe kakuibia elfu 50. Au anaongea na majambazi wanakuua ukitoka nje, hiyo ndio Tanzania ya leo!. je tatizo ni utaalam?

Ni jambo la kutegemea sana kwamba pamoja na mambo mengine; kwa kuwa kazi ya vyuo vikuu ni kufanya “tafiti” “kufundisha” na “kushauri” kama malengo mahsusi, lengo kuu ni kuifanya jamii iwe na maisha bora leo na kesho zaidi ya ilivyokuwa jana na juzi kwa kufanya tafiti kutambua matatizo sugu yanayoikabili jamii yetu, kushauri wenye mamlaka juu ya nini cha kufanya na kuifundisha jamii nini cha kufanya.Sijui kwamba kwa nini tatizo hili hawakuliona mapema na kulishugulikia ipasavyo kama sehemu ya mchango wao katika maendeleo ya hatma njema ya nchi.

Kimsingi mabadiliko kwenye vitu ni muhimu, lakini mabadiliko ya msingi ni kwenye fikra za watu vinginevyo hata sheria haziwezi kufua dafu kama kuna tatizo kwenye fikra za watu. Tatizo kuu la watanzania wengi kwa sasa ni kuongozwa na tamaa badala ya fikira na hivyo kushindwa kutumia ujuzi walio nao kwa kujiendeleza na kuendeleza taifa lao, na tatizo hilo ni la kitaifa kiasi kwamba mtu akiwa muadilifu na muaminifu watu wanamshangaa kweli.

Pengine, jambo hili limekuwa halifanyiwi kazi kwa kuwa hapakuwa na wakulianzisha. Angalau Mh.Rais katanganza mkakati wa kurejesha uadilifu katika taifa hili. Kwa kuwa tatizo ni kubwa na lipo karibu kwa jamii nzima, ni mategemeo kuwa vyuo vyetu vikuu vitamuunga mkono katika hili kulingana na nafasi yao ili kuijenga Tanzania tunayoitaka.Ikumbukwe kuwa kila mtu ana nafasi yake katika hatima ya jamii ya mwanadamu na nchi hii kwa ujumla.

Vyuo vinapaswa vijenge ujuzi, maarifa na maadili vinginevyo kujenga ujuzi peke yake kutakuwa hakusaidii kujenga jamii bora na Tanzania tunayoitaka.
 
Pia ni vyema kujua kuwa suala la mabadiliko, maendeleo au kujenga jamii au nchi ya aina fulani si suala la watu wawili watatu bali ni suala la jamii nzima. Kila mtu kukaa akidhani kwamba kuna mtu fulani ambaye yupo mahali fulani ambaye ndiye mwenye jukumu la kuamua hatima na muelekeo wa nchi na jamii kwa ujumla peke yake ni kuamua kutokuwajibika. Jiulize wakati unajadili mwingine kufanya hili ama lile wewe umefanya lipi tayari!. Usomi hautakuwa na maana kama utakuwa ni kukariri mambo bila kuelewa majukumu stahiki ambayo mtu anatakiwa kutekeleza ili kuibadili jamii na nchi yake.Msomi ambaye kazi yake ni kulialia, kukaririsha watu mambo ya kwenye vitabu bila kuakisi maisha halisia, ni msomi asiye na maana.
 
Wasi wasi unaojitokeza ni kwamba, kwa kutegemea kwamba uadilifu utarejeshwa kwa sheria peke yake, mafanikio yatakuwa kidogo kwa kuwa wenye matatizo ni wengi kiasi kwamba kama kila kesi itafikishwa kwenye sheria, mahakama zitazidiwa na ni heri ya kinga kuliko tiba. Pia, kuna hatari ya baadhi ya watoa hukumu wakawa madhalimu kuliko wahukumiwa kitu ambacho nacho ni hatari sana.
 
Uadilifu hujengwa kuanzia shule za awali ambapo wa tanzania wanaziita shule za vidudu
 
Mtoto ajengewe misingi ya uadilifu toka anapoanza elimu, serikalin Wateuliwa wawe waadilifu haswaaa
 
Kwa nini maprof wa Tanzania mnamiacha prof P.L.O Lumumba ndio awe mchambuzi wa siasa za Tanzania?
 
Nafasi ya kuchambua mambo na kuyaweka dawa na hata kutoa ushauri na miongozo so jukumu LA Prof. Lumumba peke yake
 
Kuna watu watakuwa hawajakuelewa, umetumia lugha flani hivi naipenda sana. like hiyo mkuu

Huwezi kujenga uadilifu ulianza katika fikra kama jamii imegawanywa na makundi yaliyoneemeka hutumia nguvu zao na wazoepewa na watawala kuwatupa mbali waliochini.

Ni ngumu sana kama elimu haiepewi kipaumbele na ubabaishaji katika fani ya elimu kushamiri
 
Ni ngumu sana kuzungumzia uadilifu kwenye jamii ambayo ukipewa kazi serikalini ukaiba basi wewe ni mjanja na ukatoka masikini kwasababu uliamini unaitumikia vyema Serikali kiuadilifu basi wewe ni fala utasikia wanasema mtaani "jamaa alipewa kitengo lakini amekufa maskini"

Uadilifu unaanzia ngazi ya familia, kama baba anamshauri mwanae akasomee Procurement and Supply ili aje kuwa maisha mazuri usitegemee Taifa likaja kuwa na Uadilifu.
 
Vyuo vikuu viitishe mijadala kwa kutumia wataalam wazalendo kumshauri rais magufuli ili kwa pamoja tuweze kusonga mbele
 
Back
Top Bottom