Nafasi ya Umeya hapa nchini

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,662
Siku za hivi karibuni kumekuwa na mvutano mkubwa sana kuhusu nani awe Meya na nani asiwe Meya katika wale walio kuwa wakigombea nafasi hiyo kutoka CHADEMA NA CCM, imekuwa kawaida kuwa mtu akishinda umeya watu hushangilia na kuona wamepiga hatua kubwa sana ya kiuongozi!

Hasa kwa Jiji la Dar nafasi ya Umeya imeleta shida hadi Rais alipo lisemea ndo likawezekana! Kwa upande wangu kiukweli huwa nafuata mkumbo sijui Meya anakazi gani pale atakapo chaguliwa,sijui malipo yake i mean mshahara,Sijui hasara na faida yake pale atapokuwa ameshachaguliwa kifupi sijui chochote kuhusu umeya zaidi ya jinsi anavyo patikana

Lakini sio Mimi tukubali tukatae asilimia 90% ya wananchi wa Tanzania hawaijui nafasi ya umeya na hawajui hata kama ipo! Ingawa Ni Nafasi ambayo huleta Vurugu sana hadi kuja kuipata watu hutokwa na Mapovu! Sasa Najiuliza nafasi ambayo asimilia 90% ya wapiga kura hawaijui kwanini itupe shida na kuona kuwa ndo tumewin kila kitu kuwa na Meya? japo wengi wanasema hiyo Nafasi ipo kisiasa zaidi lakini bado pamoja na hilo sioni umuhimu wake kwa chama husika kama Wanachama wengi na wapiga kura wengi hawaijui hiyo nafasi kama ipo? wengi huja kuijiua kipindi cha kumpata meya zile vurugu vurugu kwenye magazeti mtu anajua kuwa ndo kuna nafasi hio!

Ni ukweli kuwa kwa wananchi walio wengi wanawajua,wenyeviti wao wa mitaa,madiwani,wabunge,mkuu wa wilaya na mkoa,Raisi na Waziri Mkuu! Tufurahie ushindi wa nafasi ya umeya lakini tukumbuke tuna kazi kubwa sana ya kuwaelimisha watanzania na wapiga kura wengi kuhusu hii nafasi ya Umeya ili wajue chama fulani kimepiga hatua! Lakini kama nafasi inafahamika pale kipindi cha kumpata na baada ya hapo humsikii tena meya mpaka baada ya miaka 5 basi tutaishia kushangilia afu uchaguzi mkuu ukifika kura zinakuwa chache na huenda Meya asirudi tena kwa Hasira za wananchi maana anakuwa bize hadi kuwasahau wapiga kura wake!

Hongereni sana CHADEMA kwa kuukwaa umeya jiji la Dar lakini kumbukeni Meya anakazi kubwa sana kuhakikisha anakuwa na waandishi wa habari wengi Kuliko Makonda na Magufuli ili wananchi wamjue kuwa kumbe kuna kiongozi fulani jiji la Dar kutoka CHADEMA! Lakini bila ya hivyo labda mpitie Dar yote mkiwatangazia wananchi na kuwapa elimu kuhusu Umeya!
 
Nina uhakika asilimia 99.9 ya Nyumbu hawajui kazi ya Meya

Hata huyu aliyechaguliwa pia hajui kazi yake!
 
Nina uhakika asilimia 99.9 ya Nyumbu hawajui kazi ya Meya

Hata huyu aliyechaguliwa pia hajui kazi yake!
Ni ukweli mkuu ni nafasi moja yenye utata sana na wengi hatuijui sijui Meya yupo chini ya nani Mfano Jiji la Dar Meya sijui yupo chini ya nani? mfano diwani tunajua wananchi ndo wanaweza kumuweka na kumtoa, mkuu wa mkoa tunajua yupo chini ya Rais sasa huyu meya hata akizingua sijui inakuwaje
 
Meya anasimamia vikao vya madiwani, ukusanywaji wa ushuru na na kupanga matumizi ya mkoa husika.
Nihayo tu ninayo yajua kuhusu kazi za Meya
 
Mayor wajibu wa
1.kusimamia shughuli zote za maendeleo ya jiji.

2.Ikiwemo kuhakikisha wanajiji wanapata huduma bora za afya, miundo mbinu bora,elimu bora

3. kuhakikisha mapato ya jiji yanatumika ipasavyo katika shughuli za maendeleo ya jiji.

4.Kuwajibisha watumishi wa uma wanaohujumu rasilima za jiji na kukwamisha maendeleo ya jiji.

nitawapatia majukumu zaidi ya Meya.

Kuhakikisha hadhi ya jiji inakuwa bora.
 
Back
Top Bottom