Nafasi mpya za ajira Halmashauri za Mbeya na Tanga

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,763
4,587
Rejea mada hiyo hapo juu Kwa mujibu wa kibali cha Ajira mpya Kumb. Na. C8.170/369/01/96 cha tarehe 01 Decemba, 2014 tulichokipata tarehe 19/01/2015 toka kwa Katibu Mkuu Menejiment ya Utumishi wa Umma, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga anatangaza nafasi zifuatazo za Ajira kwa watanzania wote wenye sifa, na wenye umri wa miaka 18 hadi 45.

MTENDAJI WA MTAA DARAJA LA III TGS B.

SIFA ZA WAOMBAJI: .
Kwa mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Namba 1 wa mwaka 2013 kuhusu watendaji wa mitaa.
Waombaji wawe na Elimu ya kidato cha IV au VI,
waliohitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika mojawapo va fani zifuatazo:- Utawala, Sheria,
Elimu ya jamii (Sociology), Usimamizi wa Fedha (Financial Management), Maendeleo ya' jamii (Community Development) na Sayansi ya Sanaa (Social Work) kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo,. Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali



Mtendaji Wa Mtaa Daraja La II TGS C.

Waombaji wawe na Elimu ya kidato cha IV/VI
waliohitimu Stashahada katika. fani ya Uawala, Sheria, Elimu ya Jamii (Sociology), Usimamizi wa
Fedha (Finacial Management), Maendeleo ya Jamii (Community Development(, .na Sayansi ya Sanaa
(Social Work) kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.



Mkaguzi Wa Mji (Town/City Inspector)

SIFA ZA WAOMBAJI:
Waombaji wawe wamehitimu kidato cha sita.
Waombaji wawe wahitimu wa Shahada ya Sheria, Shahada va Utawala, usimamizi wa Fedha na Shahada ya Uchumi.



Fundi Sanifu Msaidizi Daraja La III Selemala

NGAZI YA MSHAHARA TGS A/B
Kwa mujibu wa Waraka wa maendeleo ya Utumishi
Namba 20 wa mwaka 2002, Nyongeza II: Kuhusu muundo wa Utumishi wa Mafundi Sanifu Technicians.

SIFA ZA WAOMBAJI:
Waombaji wawe wamehitimu kidato cha nne IV katika masomo ya Sayansi na ~ufuzu mafunzo ya
Ufundi katika fani ya Ufundi Seremala katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali au,
Waliomaliza kidato channe wenye Cheti cha majaribio ya Ufundi Seremala Hatua ya pili kutoka
Chuo cha Ufundi Seremala kinachotambuliwa na Serikali



Fundi Bomba Msaidizi Daraja III
NGAZI YA MSHAHARA TGS A/B
SIFA ZA WAOMBAJI:
Waombaji wawe wamemaliza kidato cha nne IV
katika masomo ya Sayansi na kufuzu mafunzo ya Ufundi katika fani ya Maji kutoka katika Chuo
kinachotambuliwa na Serikali au, Waliomaliza kidato cha nne wenve Cheti cha majaribio ya ufundi Bomba Hatua ya pili (Trade Test II) kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,



Fundi Msaidizi Daraja La II Umeme

NGAZI YA MSHAHARA TGS A/B

SIFA ZA WAOMBAJI:
Waombaji wawe wamemaliza kidato cha nne IV katika masomo ya Sayansi na kufuzu mafunzo ya Ufundi katika fani ya Umeme kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali au; Waliomaliza kidato cha nne wenye Cheti cha majaribio ya ufundi Umeme Hatua ya pili (Trade Test II) kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali.



Maafisa Maendeleo Ya Jamii Wasaidizi Daraja La III(x6) .

NGAZI YA MSHAHARA TGS B.

Kwa mujibu wa Waraka wa maendeleo ya Utumishi
Namba 7 wa mwaka 2002, na marekebisho yake ya tarehe 4 Agosti, 2008 katika Waraka Kumb. Na.
AC.62/260/01.

SIFA ZA WAOMBAJI:
Waombaji wawe wamehitimu kidato cha nne IV waliofuzu mafunzo ya cheti kwenye fani ya maendeleo ya jamii katika Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vya (Buhare, Rungemba) au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.



Katibu Mahususi Daraja La III (x3)



SIFA ZA WAOMBAJI:
Kwa mujibu wa waraka wa maendeleo ya Utumishi Namba 9 wa mwaka 2002 nyongeza VI: Kuhusu muundo wa Utumishi wa Makatibu Mahususi
(a) Waombaji wawe wamehitimu kidato cha nne IV waliohudhuria mafunzo ya Uhazili na kufaulu mtihani wa Hatua ya Tatu, wawe wamefaulu somo la Hati Mkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya Computer kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata Cheti katika Program za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher

Msaidizi Wa Kumbukumbu Daraja La II(X3)
NGAZI YA MSHAHARA TGS B
SIFA ZA WAOMBAJI:
Kwa mujibu wa Waraka wa maendeleo ya Utumishi Namba 9 wa mwaka 2002 Nyongeza Namba V kuhusu muundo wa Utumishi wa Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la II (Records Management Assistant II) Waombaji wawe wamehitimu kidato cha nne/sita wenye cheti cha Utunzaji wa Kumbukumbu katika moja wapo ya fani za Afya, Masjala na Ardhi.

KAZI YA AUXILIARY POLICE NAFASI ISHIRINI (20)

SIFA ZA WAOMBAJI:
WaombaJi wawe wamehitimu kidato cha nne waliohudhuria mafunzo ya:-
Auxiliary police kwa miezi isiyopungua sita toka Chuo cha Polisi Moshi.
Waliohitimu mafunzo ya JKT na kupata Cheti cha mafunzo ya JKT.
'Waliohitimu mafunzo ya mgambo na kupata cheti cha Mgambo.
Wawe wamefaulu angalau masomo matatu ya kidato cha nne.

APPLICATION INSTRUCTIONS:


Maombi yote yaambatane na vivuli vya vyeti vya masomo na mafunzo. -
Muda wa kuleta maombi ni ndani ya siku 21 kuanzia tarehe ya Tangazo hili, siku ya mwisho ya kupokea
maombi ni tarehe 16 Februari, 2015 saa 9.30 Alasiri.
Waombaji wote waweke namba zao za simu kwenye barua za maombi, majibuyatatolewa kwa njia ya
simu kwa wote watakaoitwa kwenye Usaili.
Waombaji wenye anuani za Barua Pepe (E-mail) na Fax waweke pia namba za simu katika barua zao
za rnaornbi, zitakazotumika kuwapatia majibu ya kuitwa kwenye usaili.
Waombaji waweke pia picha moja ya Passport Size iliyopigwa hivi karibuni katika barua zao za maombi
ya kazi.
Tuma kwa
MKURUGENZI
HALMASHAURI YA
S.L.P. 178
TANGA



==================
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA
SIMU: 025 - 2502280
FAX: 025 - 2500128
MKURUGENZI MTENDAJI:
Barua pepe: mbeyaded@yahoo.com


S.L.P 599
MBEYA
TANZANIA


YAH: TANGAZO LA KAZI


Kwa mujibu wa kibali chenye kumb. Na. CB.170/364/01/9/47 cha tarehe 24 Octoba, 2014 kutoka kwa katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Manajimenti ya Utumishi wa Umma na kibnali mbadala cha Ajira kumb. Na. CB 170/364/01/G/51 cha tarehe 29/12/2014 kutoka manajement ya utumishi wa Umma

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mbeya anawatangazia nafasi za kaiz Watanzania wenye sifa za uwezo wa kujaza nafasi kama ifuatavyo

KATIBU MAHSUSI – NAFASI 6

SIFA
Kuajiliwa Wahitimu wa Kidato cha IV walioudhulia mafunzo ya uhadhiri na kufaulu mtihani wa hatua ya tatu. Wawe wamefaulu somo la Hitimisho ya Kiswahili na kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya kompyuta kutok chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft office, Internet and Publisher

MAJUKUMU
Katibu mahsusi daraja la III atapangiwa kazi kazika Typing Pool au chini ya katibu Mahsusi mwingine mwenye cheo cha juu kumzidi kwenye ofisi ya Mkuu wa sehemu ya kitengo

i. Kuchapa barua, taarifa ya nyaraka za kawaida
ii. Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa
iii. Kusaidia utunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake na ratiba za kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake wakati unaohitajika
iv. Kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada, nyaraka au kitu chochote inachohitajika katika shughuli za kikazi hapo ofisin
v. Kusaidia kufikisha maelekezo kwa mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia kumharifu kuhusu taarifa zozote anzokuwa amepewa na wasaidizi hao
vi. Kusaidia kupokea majarada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika
vii. Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msaidizi wake wa kazi
NGAZI YA MSHAHARA
Mshahara ni kwa mujibu wa viwango vya mshahara serikalini yaani TGS B (345,000 X 9,300 hadi 428,700) kwa mwezi na mwajiriwa katika kada hii ataanza na 345,000/= kwa mwezi
============

MCHAPA HATI II- NAFASI I

SIFA
Kuajiliwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita waliofauru mtihani wa uhaziri hatua ya 2 kutoka chuo cha Watumishi wa Umma na ujuzi wa Kompyuta hatua ya I na II toka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali

MAJUKUMU
i. Kuchapa taarifa za uhamini na Hati za faida
ii. Kuchapa Nyaraka na Hati za kumiliki ardhi

NGAZI YA MSHAHARA
Mshahara ni kwa mujibu wa viwango vya mshahara serikalini yaani TGS B (345,000 X 9,300 hadi 428,700) kwa mwezi na mwajiriwa katika kada hii ataanza na 345,000/= kwa mwezi
================

DEREVA DARAJA LA II - NAFASI 1

SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Kuajiliwa wenye Cheti cha Mtihani wa kidato cha Nne (IV) wenye leseni daraja la "C" ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali, wenye cheti cha Majaribio ya ufundi daraja la II

KAZI YA KUFANYA
i. Kuendesha magari ya abiria na malori
ii. Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo
iii. Kufanya matengenezo madogomadogo katika gari
iv. Kutunza na kuandika daftari la safari "Log - book" kwa safari zote

Mshahara ni kwa mujibu wa viwango vya mishahara serikalini yaani TGOS A2 9271,200 X 6,200 hadi 370,400) kwa mwezi na mwajiliwa katika kada hii ataanza na 271,200/= kwa mwezi

MASHARTI KWA UJUMLA
1. Mwombaji awe Raia wa Tanzania na awe tayari kufanya kazi sehemu yoyote kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya
2. Mwombaji awe na umri usiozidi miaka 45 na awe hajawahi kupatikana na kosa lolote la jinai au kufungwa jela
3. Maombi yote yaambatanishe maelezo binafsi yanayojitoshereza (Detailed CV)
4. Maombi yote yaambatanae na nakara za vyeti vya taaluma, vyeti vya elimu (IV - VI ), cheti cha kuzaliwa na picha mbili za rangi za hivi karibuni (Passport size) na iandikwe jina nyuma)
5. Testimonials "Provisional Result" Statement or results" hati ya matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULT SLIPS) HAVITAKUBALIWA
6. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TSU na NECTA)
7. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawataruhusiwa kuomba isipokuwa kama wanakibali cha katibu mkuu kiongozi
8. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 10 Februari 2015 saa 9:30 Alasiri
9. Maombi yaandikwe kwa mkono na mwombaji mwenewe na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo

MKURUGENZI MTENDAJI (W)
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA
S.L.P 599
MBEYA

Upendo Sanga
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA

Source: Nipashe 28th January 2015
==========
 
Watu wote ninaowafaham ambao wameaply hakuna aliyeitwa till now. Nimestuka kidogo kusikia written interview next week. Tommorow nitacheki na mtu ambae yupo pale ili aweze kunithibitishia hili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom