Nadharia ya USHINDI ktk siasa.

Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
10,490
13,551
Ni CCM tu ktk nchi hii ndicho chama chenye kuweza kujivunia hii nadharia ya ushindi.

Ni CCM ndicho chama pekee kinachoongoza kwa misimamo ya kisiasa, hakiingiliwi na makundi, na kinawazalendo waliotayari kuitumikia nchi yao.

Ukija upinzani, hapajawahi tokea kuwa na chama chenye nadharia ya ushindi. Mfano, chama kilichokufa 2015 chama cha wafu wa chadem kilijaribu, ila mwisho kikaangukia pua na hatimaye kupelekea kuzikwa rasmi 2015. Moja ya ajenda yao hiki chama marehemu/hayati chadema ilikuwa mabadiliko. Hasa walipigia kelele rushwa, uzembe, ufisadi, na mikataba mibovu ya wawekezaji. Walienda mbali zaidi kusema kwenye madini tunaibiwa. Ila watanzania wakawang'amua, wakawatosa 2015. Hivyo nadharia ya ushindi kwao ikashindwa vibaya mno.

Sasa tupo kwenye ushindani mwingine, masalia ya huyu hayati chadema wamekomaa wakimkingia kifua mwizi ACACIA, na CCM na Watanzania wamesimama kidete kusema hata kama mikataba ilisainiwa, lakini imekeukwa kwa kuacha kiwango kikubwa cha madini ndani ya mchanga, hivyo ni lazima pawe na uwajibikaji wa kusema kweli. Watanzania wanasema muwekazaji amekuwa akidanganya, hivyo alipe ule udanganyifu, ila masalia ya hayati chadema wanasema muache mwizi aendelee kuiba.

Kama ilivyokuwa 2015, lazima CCM na watanzania tushinde kwa sababu tumezoea ushindi, na hatujawahi kushindwa!
 
Nakuunga mkono japo siipendi CCM ila sijaona chama cha upinzani chenye uwezo wa kushika hatamu
 
Back
Top Bottom