NACTE yakifungia chuo cha Mbeya Polytechnic!

NACTE yakifungia chuo cha Mbeya Polytechnic!

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,365
Reaction score
27,766
Akisoma uamuzi huo kwa niaba ya NACTE,Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla amesema kuwa taarifa kutoka NACTE zinaonesha kuwa chuo hichi kina mapungufu mengi ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya mifugo ambayo hayajathibitishwa na vyombo husika vya serikali.



Pia amesema kuwa chuo hicho kimekuwa kikidahili wanafunzi wasiokuwa na vigezo, akitolea mfano wanafunzi wanaosoma kozi ya mifugo ambapo kati ya wanafunzi 359 ni wanafunzi 89 pekee ndiyo wanaotambulika kuwa na vigezo husika.


Wakizungumza kwa uchungu baadhi ya wanafunzi wamelalamikia chuo hicho kwa kuwasababishia upotevu wa muda na gharama, ambapo baadhi yao walikuwa tayari wamehitimu na walikwenda chuoni hapo kufuatilia vyeti.“Mimi nimetoka mbali, nimekuja kufuatilia cheti change, sasa nina miezi miwili hapa, kila siku nazungushwa nazungushwa, kumbe walijua wanakuja kufungiwa, kwahiyo cheti change sipati, namuda nimepoteza, nimekaa hapa miaka mitatu halafu leo naambiwa miaka yangu mitatu haina maana tena, sikubali sikubali..” amesema mwanafunzi Catherene Buda huku akitokwa na machozi.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa chuo hicho Ellertoni Mwamasika, ameomba radhi na kusema kazi ya kuendesha chuo ni ngumu “Chuo kinawaomba radhi wote, ila mjue kuwa kazi hii ya kuendesha chuo ni ngumu”Hata hivyo serikali imesema wanafunzi wenye sifa watahamishiwa katika vyuo vingine huku ikimuagiza mmiliki wa chuo hicho kuwalipa wanafunzi gharama zao zote kabla hawajatoka chuoni hapo.


uploadfromtaptalk1465668380624.jpg
 
Hizi movie mpaka zikiisha tutakua tumeshakauka.....watoto wa wakulima mbona kazi tunayo. Akina Jesca wanaenjoy tu
 
Nasisi watanzania tunatakiwa tuamke na tuwe makini kwanini tunapenda slope aka kitonga. Vyuo vinavyotambulika na vilivyosajiliwa vinajulikana sasa kwanini tunajiunga na vyuo visivyo na sifa? Tuwe makini
 
Aiseee wamezuia bunge modern taarab live.. Naona kila wiki tunapata movie mpya... Haya napita tu...
 
Back
Top Bottom