Nachingwea-Shamba 17

Nachingwea-Shamba 17

atirbac

New Member
Joined
Jul 18, 2014
Posts
3
Reaction score
0
Translation of my earlier post:




ULIZO


Nachingwea-Shamba 17


Hamjambo? Mimi ni raia wa Msumbiji na ninafanya utafiti kuhusu asili ya Shamba 17 la Wilaya ya Nachingwea.


Ninaelewa kuwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia, Uingereza ilitenga Shamba 17, ikiwa moja ya mashamba 21 (au, 20 kulingana na vyanzo vingine), kwa wapiganaji wastaafu wa vita hivyo ambao wangependelea kushiriki miradi ya kilimo.


Ningependa kujua:


a) Maagizo kamili ya kikoloni kuhusu kuanzishwa kwa mashamba 21 (au 20) Wilaya ya Nachingwea.


b) Idadi ya askari waliokuwa kwenye mashamba hayo.


c) Kila shamba lilikuwa na ukubwa gani.


d) Aina ya kilimo, kanuni na masharti.


e) Ikichukuliwa maanani kwamba Shamba 17 lilipewa Frelimo na vikundi vingine vya ukombozi kutoka kusini mwa Afrika 1965, lilifungwa lini kama mradi wa kilimo?


f) Ilitokea nini kwa mashamba hayo?


Asanteni sana kwa msaada wenu katika jambo hili.
 
Back
Top Bottom