Nachanganyikiwa naomba msaada...........


Jestina I think hio ipo zaidi kwenye category ya kujali ama upendo... Na hio ina play part both ways... Kutegemea na mazingara. Kwamba kama umemkuta nyumbani umerudi na umechoka sioni ubaya wa yeye kukupokea na maybe kukuvua koti hasa kama kweli unaelekea kulivua - na vice versa. Take note haya matendo sio onesided kua mwanamke tu ndio afanye.... kuweza kuendeleza vitu kama hivi inabidi pande zote mbili zionesha kujali. Kuna couples mimi nawafahamu... A guy anaweza iron nguo zake na mkewe jioni for work kesho yake huku mkewe yupo na responsibilities nyingine....
 
Depends labda anakupenda na hapendi akuone unasumbuka., mambo mengine madogo anaona anakuchosha bure, nadhani cha maana sababu its your nature and your character usiache kufanya unayofanya hususan mkiwa peke yenu (you know small things add a lot na siku ukipotea ataku-miss zaidi) ila labda sometimes anakuwa embarrassed kwa marafiki zake labda watadhani ni slave driver (anamtesa mama) if that the case labda mkiwa kwenye umati punguza kidogo au jaribu kumshauri hata hao marafiki zake wanaona wivu of how lucky he is.., anyway its minor things nina uhakika zaidi ya kukuonea huruma na kutokutaka kukusumbua he means well (its because he cares ndio maana hataki kukusumbua)

Ningemuona ningemshauri na yeye ajaribu kukufanyia hayo (ukiingia akupokee mizigo na siku ukisikia kiu akuletee maji)
 

Aksante sun wu............ nimelelewa hivyo, na mbaya zaidi kwa jinsi nimpendavyo najisikia tu kuwiwa kumuenzi kwa staili hiyo, iweje ghafla iwe rahisi kubadilika kisa mwenzi wangu haapreciate??!
 
MwanajamiiOne

kama umemsoma AshaDii, kasema heshima is given and earned, hadi umkubali mwanamme kuwa kichwa cha familia na lazima atakuwa amekidhi vigezo vya matarajio yako ya mwanamme unayemtaka.

Hiyo ya kuitwa toka jichoni kuna kumpa remote waweza ona kero, mie kwangu hewala, nachukulia kamiss kuona mgongo wangu nikiwa nimefunga kanga, anatafuta sababu ya kuniita.

Haya mambo ya yard na mile inategemea tu na nyie mipaka mliweka wapi, sidhani kama wanamme ni wabaya kiasi hicho afu kila siku tunaliliana tukae nao lol
 
Last edited by a moderator:

Si kila ulicholelewa nacho na kujuzwa basi ndiyo ukishikilie hivyo hivyo kama kilivyo. Wakati mwngine waweza kukifanyia mabadiliko ili kiendane na hali na mazingira uliyonayo. Ni kutumia common sense tu.

Hao waliokujuza hawapo kwenye huo uhusiano wako na huyo mtu wako. Kinachojalisha zaidi, kwa mtazamo wangu, ni wewe na huyo mtu wako kufanya mambo yenu jinsi ambavyo yanavyowapendezesha nyinyi wawili.

Mafunzo na malezi wakati mwingine hustahili kutupwa huko.
 

Uko sahihi kabisa BADILI TABIA, kama ambavyo wewe umeidefine heshima kwa mtazamo wako, mie nyongeza ya hayo uloyataja, naongezea.....yote ni heshima.
 

labda kama nimeolewa na mlemavu, other wise asahau huu mdebwedo sioni kama una uhalisia ndani yake.....:mad2:
 


I support you... mtu ambae anakuheshimu hawezi kukutoa jikoni eti uje umpe remote! Huo ni utumwa unless otherwise hapo alipo anaumwa ama kuna a delicate thing ameshika/fanya ambayo haitakiwi iwe disturbed. Na ikifika hio stage ni kwamba kakushika masikio ile mbaya... na he is not good for you aisee...
 

Aksante Bwan Chuchu umenifungua sikio ndugu yangu mwe..... kumbe ninayo kazi ya ziada..... yale mafundisho na hisia za kiada inabidi nizichambue tena eh!!
 
labda kama nimeolewa na mlemavu, other wise asahau huu mdebwedo sioni kama una uhalisia ndani yake.....:mad2:


lol.... I like this.... Knowing what you want katika mwenza before huja commit is the best thing... All the Best. Punguza basi huo mukari wa moto Jestina hadi naogopa sasa.
 
Kuna heshima hizi za kiafrika hasa maeneo fulani fulani zina raha yake bana.

Sio unamwita mume, kwa kushout kama waita kitoto kidogo lol

raha ya mwanamme aheshimike na aheshimiwe kama anastahili.

 

Tuko pamoja kongosho tena basi ukiitwa hufanyi kosa ati, warekebisha khanga kiunoni, nakuhakikisha anapata wasaa wa kutosha kuyaona majaaliwa ya mwenzi wake ati....tena ukishampa maji ya baridi wauliza kama anahitaji na ice cubes (but wauliza ilhal umempa ngongo ati)
 
Last edited by a moderator:

mwenzangu, ukianzisha jambo hakikisha unaliendeleza la sivyo utaonekana baadaye unamapungufu. Mf. halisi ni kuwa nilipooa kati ya miezi 2-5 baada ya ndoa nilikuwa natandika kitanda nikiwa wa mwisho kuamka na pia nilikuwa nafua nguo kumsaidia my wife, ghafla kwa kuamua nilianja kuacha kidogox2, eeeeh wife akaanza kununa na kuanza kujifungia chumbani nikagundua hiyo sababu.
 
Last edited by a moderator:
Kuna heshima hizi za kiafrika hasa maeneo fulani fulani zina raha yake bana.

Sio unamwita mume, kwa kushout kama waita kitoto kidogo lol

raha ya mwanamme aheshimike na aheshimiwe kama anastahili.

Kongosho i believe umenipata... Mimi I believe in heshima to my Man. Kile kipo ndani
ya uwezo wangu I will do mradi lililo nje ya uwezo wangu basi nitapotezea... na naamini
in being careful toka mwanzo na the type of Man upo nae... Mwanaume lazima awe wa
kuheshimika hata kwa wanaume wenzie bana!
 
Last edited by a moderator:
sasa mwj1 hapa ipo sababu ya mim kutoa ufafanuz kwa mtizamo wangu juu ya hili la heshima na "woga" hasa kwa wapendanao.....!nitakoment kwa kirefu zaidi kesho...!

hao wanaofanya heshima hao...izo za kimuonekano wapo wanaofanya kwa kulinda tu mahusiano...infact wanfanya tu kama mazoea labda kwa kuangalia histrory/backgrounds za kabila la mupenziwe....makabila mengine wanaume wanapenda kuabudiwa sana..kwa iyo ni swala la mwanamke mwenye focus kupretend tu.....!ingawa ni mbaya sana...



ndan ya hili neno heshima kuta kitu kingine kikubwa zaidi ya hili la kupigiana magoti...!

nitakoment kesho...!kutumia sim ninapata shida kidogo kuandika..
 
Dadaaa........... plz, kama ataka kuuona mgongo jamani haruhusiwi kuntoa jikoni? jamani hebu plz msinipangie namna ya kummiliki mwenzi wangu. Ni sawa na mie najihisi nimemmiss but yuko kwa jirani apiga story ndo nsimwite aje kuna mende chini ya uvungu?? pliz
 
Mwanajamii one, kwanza nianze kwa kukupongeza kwa jinsi ulivyo na heshima kwa mwenz wako.My dear asikudanganye mtu, Dr Ngaiza aliwahi kuandika kwenye journal ya gender wakati fulani kuwa "the woman hwealth is called upon mens head, wether that is a father or a spouse" mimi nakubaliana na hili kwa 100%. na ndiyo maana kwa mila zetu za kiafrika mwanaume ana heshima yake.

hata kama mtu atasema mimi siwez kufanya haya kwa mume wangu lakini ni busara sana kwa mtu kumuheshimu mumewe hasa kwa yale anayoyataka na anayoofikiri kuwa ynanamfurahisha mumewe. Mimi huwa napenda kuongelea uhalisia, bado mwanaume anahitaji heshima yake kama baba na kaka mume. kumbuka huyu ndiyo kichwa cha nyumba hapaswi kulinganishwa na mama ndani ya nyumba.

Kwa wadada wa siku hizi huwa wanaona kama kumuheshimu mume ni ulimbukeni lakini si kweli, ukitaka kuamini tizama familia ambazo baba anaheshimiwa, hata kama ni mbaya lakini bado upendo wake kwa mkewe na familia huwa unakuwepo.

Heshima si tu kwamba inaonyesha unyenyekevu kwa mwenzi wako bali pia inaonyesha upendo. Ninavyoamini mimi huwezi kumuheshimu mtu kama humpendi, na heshima humfanya mtu anayeonyesha kupunguza makosa. Mathalani kama unamuheshimu sana mwenzi wako ni ukweli kuwa kuna makosa mengi ambayo hutoyafanya kwasababu tu utakuwa na hofu juu yake. Hali hii humfanya yule anayeheshimiwa kujenga imani zaid kwa anayeionyesha heshima.

kamwe usilogwe kuharibu penzi lako kwa kutokumuheshimu mumeo. Wapo wanaume wengine ambao huwa wakiheshimiwa hawaoni kama n kitu cha maana, hili lisikukatishe tamaa hata kidogo, wewe timiza wajibu wako kwa kuendelea kuheshimu ipo siku ataelewa tu. Kwani napenda kukuhakikishia ipo siku atakuta yuko tofauti sana na mwenzie asiye heshimiwa na mkewe. katika dini imeandikwa mke mwema mumewe hujulikana malangoni penye watu. maana yake hata kama akiwa mbele za watu atajulikana tu kuwa mkewe anaheshima.

mwisho endelea kummvua viatu, kumwosha miguu wakati anakunywwa kahawa jioni, kumvua koti hata kumvalisha nguo. Ringa na mumeo bwana halafu utaona jinsi utakavyoifaidi ndoa yako. Mimi huwa naamin san kwenye dhana kuwa maisha ya amani yenye upendo heshima na kujaliana huwa yanakuwa na siku nyingi za kuishi kuliko yenye ugomvi, nidham mbovu na mengine ya kufanana na hayo.

Mpe mumeo nafasi yake kama baba ambaye utamuheshimu, kwa kila kitu. usichoke kuonyesha upendo wako kwa njia zote. Tena ogopa sana siku hizi watu wamekazana kuwaloga wanaume wakiamin ndio watakuwa wazuri kumbe ni uongo mtupu, dawa ya mwanaume ni upendo, heshima, na nyama nzuri ya ulimi. kamwe usimkarikie mumeo mbele za watu wala kumbishia mbele za watu hakika hiyo ni sumu na itakugharimu sana kwenye ndoa yako.
 
Nimekuelewa suppose hakuna kupretend.........its a genuine heshima Tuanzie hapo coz hata mie siamini katika nidhamuya uoga. kwa faida ya nani sasa?
 

AshaDii nakugongea a100 likes
 


Hivi vitu haviendi black and white.... Kuna vitu katika situation zote ambazo zahitaji kusoma nyakati za alama (or is it alama za nyakati?); kama umeishi na mwenza wako kwa mda mrefu... hajawahi hata siku moja niita toka mbali (lets say nje or another room) kuja mchukulia kitu ambacho kipo karibu nae.... akifanya hivo kwa siku moja na hajawahi wala hana hio tabia, akanitoa jikoni kuja niomba remote kua nimpe... kwa kweli sitakwazika na nitampatia... na kumuuliza kama everything is alright or just tired.

Hivo MJ1 akikuita ili akuone... kuna utofauti wa uombaji.... na the way ata react ukishafika hapo. In other words uhakikishe mboga ina maji ya kutosha isije tu ikaungua.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…