NAANZA KUAMINI UHUSIKA WA SERIKALI TUKIO LA KUTEKWA ROMA NA WENZIE

CHOCKSTIC

JF-Expert Member
May 16, 2011
474
254
Ni takribani miezi miwili sasa inakatika huku kukiwa na ukimya wa kushangaza kutoka vyombo vya usalama kuhusu kilichowatokea ROMA na wenzie,mimi kama raia wa nchi hii imeumizwa na kusikitishwa sana na ukimya huu kuliko hata tukio lenyewe la utekaji,haiwezekani raia wanatekwa wanaenda kuteswa vibaya halafu tukio hilo lipite kama hakujatokea kitu inasikitisha sana.

Nimesikitishwa pia na kimya cha waziri wa habari kwa jinsi picha yake inavyonijia siku akiwa kwenye press conference ya ROMA akionekana kana kwamba ana uchungu na ameguswa sana na tukio hilo kumbe alikuwa anatuachezea bongo muvi,inasikitisha sana
Hata mkuu wa mkoa aliyehakikisha vyombo vya dola vinafannya juu chini kuhakikisha ndugu zetu watanzania wenzetu wanapatikana wakiwa wazima nae pia hana hata habari kama vile hili jambo halikumgusa,KWELI!?

vyombo vya usalama viko kimya,mwezi wa pili huu unakaribia lakini hakuna findings wala update yoyote mpaka sasa,hii inaleta picha mbaya kwamba raia sasa hatuko salama ndani ya nchi yetu kama ni kweli watu wanaweza wakafanya mambo ya kutisha kiasi hicho halafu wakapotelea GIZANI.huu ni muendelezo wa matukio ambayo serikali haiyapatii ufumbuzi kama matukio yanayotokea huko KIBITI,tukio la kupotea BEN SANANE,matukio haya yanaichafua serikali kwamba imeshindwa kuchukua hatua au serikali inapuuzia UHAI wa RAIA wake na pia inapuuzia haki ya sisi wananchi kujulishwa kuhusu usalama wetu.kwa hali hii halafu anatokea mtu anakuhubiria kuhusu UZALENDO,kweli!?
 
Watekwaji nafikiri kuna maneno waliyokuwa wakiulizwa na kuambiwa na watekaji wakati wakiwa wametekwa na wakisurubiwa lakini cha ajabu hawajayasema ni wazi watekwaji wanajua wazi walitekwa na nani ka kwa sababu zipi.
 
Ngoja utekwe wewe ndipo utajua ukirudi kule huwezi kusimulia kilichpkupata. Ndio maana ukaitwa utekwaji yaani unapotezewa Uhuru wako wote katika maisha yako.kuna mengi nyuma ya paziwa huyajui
 
Huyu si alikua anaimba yuko tayari kufa!!!
Kumbe alizani kifo ni kusinzia eeh!!!
Nasikia wanamgogoro na mkewe karibu wataachana kisa hawezi tena mapenzi na mkewe
 
Huyu si alikua anaimba yuko tayari kufa!!!
Kumbe alizani kifo ni kusinzia eeh!!!
Nasikia wanamgogoro na mkewe karibu wataachana kisa hawezi tena mapenzi na mkewe
mada imejikita kujua vyombo vya usalama vimefikia wapi kuhusu tukio hili la utekaji?
 
Ishu ni kwamba serikali hufanya kazi kwa zimamoto na si weledi.
Ingekua tukio kama la Kibiti wangeshakuja na majina na kusema tumewaua majambazi kadhaa...

Sasa hapa hawana uwezo wa kuzima moto inabidi wakae kimya tu.
 
Pole kunawatu huwa mnaelewa polepole wanaitwaga slow learner...wapo wengine mpaka mwakani watakuwa bado kuelewa!
 
Back
Top Bottom