Naandaa mashtaka dhidi ya viongozi waandamizi kwa kosa la kulea uzembe katika mambo ya msingi, ukiwemo umeme

Daisam

JF-Expert Member
May 23, 2016
2,626
3,141
Nchi hii kwa sasa inapita katika kipindi kigumu sana kutokana na uhaba wa umeme.

Uhaba huu wa umeme kwa asilimia kubwa huwa ni wa kutengenezwa tu na baadhi ya mafisadi.

Tatizo kubwa hapo ni kwamba, wanakuwepo mafisadi wanaotengeneza tatizo kwa maslahi yao na kwa upande mwingine wanakuwepo viongozi/wenye MAMLAKA ambao ni waoga/wazembe wa kutowachulia hatua kali wale wanaohujumu umeme.

Itakumbukwa wakati ule wa awamu ya 5, JPM alitamka maneno machache tu"sitaki mgao wa umeme katika Nchi hii". Kauli hii ilitekelezwa kwa zaidi ya 98%. Hatukuwa tena na uhaba wa umeme wa kutengenezwa.

Sasa basi, kwa sababu tatizo hili kwa asilimia kubwa linatokana na uzembe wa baadhi ya viongozi kutochukua hatua madhubuti kukomesha tatizo hili, tunaunda kikosi cha wanasheria ili kuandaa mashtaka dhidi ya hao viongozi wazembe kushindwa kutatua tatizo la umeme linaloikumba Nchi yetu kwa sasa.

Mashtaka hayo yataambatana na kuiomba mahakama kuwaamuru waliosababisha tatizo kuwalipa FIDIA Watanzania wote walioathiriwa na kutopatikana kwa umeme.

Madhara ya kutokuwepo kwa umeme ni pamoja na:

1. Mafundi welding kukosa kazi.

2. Vyakula vya biashara (samaki wabichi, nyama pamoja na madawa na bidhaa mbalimbali) kuharibika kwenye Friji. Madhara ni mengi mno.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom