Naamini kuwa Tanzania yaweza epuka yaliyotokea Kenya ktk uchaguzi 2007 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naamini kuwa Tanzania yaweza epuka yaliyotokea Kenya ktk uchaguzi 2007

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwadada, Dec 1, 2011.

 1. M

  Mwadada Senior Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Tanzania ipo ktk mchakato wa kupata katiba mpya,hii ni moja ya fursa kubwa sana kwa mh. J.Kikwete kuandikwa vema zaidi ktk historia ya taifa hili, ikiwa atahakikisha na kuruhusu zoezi zima la upatikanaji wa katiba mpya linaenda kwa kuzingatia maoni toka kwa wadau wote toka ktk kada mbalimbali nchini,kwa uhuru na usawa na haki.

  Kuna baadhi ya wadau wanadhani hili ni swala la wanasiasa tu,na zaidi baadhi ya vyama vikubwa tu. Baadhi ya wanasiasa au wengi wao wanaliona swala la katiba mpya kuwa ni fursa ya kwenda ikulu na wengine kwao ni fursa mbaya ya kupoteza madaraka. Yote hayo yaweza kuwa sawa, lakini katiba mpya inapaswa pamoja na kuweka mazingira sawa kwa vyama vya siasa kushinda au kushindwa kwenye chaguzi mbalimbali. Pia raslimali za taifa hili ni muhimu kupewa kipaumbele ktk kuzitunza na kuzitumia.

  Maadili na uadilifu kupewa mkazo ktk taifa. Ni wazi kuwa serikali yetu haina dini,lakini sidhani kuwa serikali inapaswa isiwe na maadili. Ni wazi kuwa taifa letu pamoja na serikali yake vinakabiliwa na changamoto nyingi sana,nadhani badala ya kuendelea kulalamika au kulaumu ni wakati wa kutenda. Nadhani Siku zote umadhubuti wa serikali unatokana na jinsi serikali inavyokabiliana vema na kwa ufanisi na changamoto inazo kabiliana nazo,na hata zilizo mbele yake. Hapa ndipo ninafikiri kuwa ktk changamoto kubwa ambazo mh. rais na serikali yake zinawakabili ni swala zima la katiba mpya kwa taifa hili. Ambayo pamoja na mambo mengine kwayo twaweza pata serikali tatu,moja au kuendelea na mbili.

  Yawezekana zoezi la kupata katiba mpya likaenda kwa wakati itakuwa ni vema ilmladi katiba itoke kwa watanzania. Lakini pia yawezekana zoezi likachukua muda mrefu kinyume na matarajio,pia ni vema ilmladi mwisho ipatikane katiba inayotoka kwa wananchi kwa ajili yao na taifa.

  Ikitokea zoezi limeshindwa kukamilika kwa wakati ni vema kwa mh.rais kuhakikisha tume huru ya uchaguzi inaundwa,itakayo kuwa wazi na kufuata haki kwa pande zote ktk uchaguzi ujao 2015 ili kujenga imani kwa wadau wote. Hii yaweza saidia sana taifa letu kupita vyema ktk kipindi chenye changamoto kubwa kwa taifa na kuepuka yaliyotokea kwa jirani zetu Kenya.

  Hili la katiba mpya linahusu wananchi wote wa Tanzania kwani ndiyo mstakbali wao pamoja na watoto na raslimali za taifa kwa ujumla,hili ni zaidi ya vyama vya siasa,basi ni vema watanzania toka ktk kada mbalimbali wahusike na kuafikiana ktk hatua zote za mchakato hii itasaidia kupatikana kwa katiba itakayo heshimika zaidi kwa wananchi wote ambao ndio wadau wakubwa ktk zoezi zima.

  Ikumbukwe kuwa amani ni matokeo ya mambo makuu manne ya kimsingi ambayo ni Ukweli, Uhuru,Haki na Mshikamano. Haya yote yanabebwa na neno moja kuu 'UPENDO'. Mungu wabariki viongozi wangu wa Tanzania waweze kutafsiri vema alama za nyakati na waweze kuamua wakati wote kwa hekima yako. Mungu tubariki wananchi wa Tanzania ili nasi hekima yako ituongoze.
  Ni mtazamo wangu wana jf,naomba kusahihishwa/ kukosolewa ili nipate kujifunza zaidi,asanteni.
   
Loading...