Modem inatumia tigo?? Itupe ina tabia mbaya.
On a serious note.
Taja aina ya modem na imei yake. Kwa uzoefu wangu ni rahisi sana ku-unlock zte modems online kushinda Huawei.
Ila kwakua hatuaminiani usitaje, nenda google search aina ya modem yako mfano "zte modem unlocker"
Ikija option ingia, aghalabu utakuta sehemu unaambiwa ingiza imei yako ili upewe passcodes za modem yako, utaingiza imei kisha utagewa hizo passcodes.
Utaweka laini ambayo haikutengenezwa kwa ajili ya huo mtandao, mfano utaweka ya Voda au Airtel, itakudai passcodes utaingiza zile ulizogewa, basi utakua umetatua tatizo.
Zingine siyo lazima uweke laini ya tofauti, kutegemea na aina ya modem.