Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,920
Kila kitu kina faida na hasira zake na ukweli huu utajidhihirisha katika utendaji wa serikali hii na hata katika bajeti iliyopitishwa leo.
Tunakoelekea serikali ndio itakuwa na hela huku wananchi wakiwa hawana kitu na hali hii teyari imeanza kujidhihirisha na hata mfanyabiasha Ahmed Shabiby ambae ni Mbunge wa Gairo kupitia CCM hivi karibuni alisema wazi Bungeni kuwa mtaani hali hivi sasa ni ngumu na akahoji nani asiejua ukweli huu?
Sasa najiuliza,serikali ikihodhi hela huku wananchi wake wakiwa hawana fedha ni nini kinafuata kama siyo kupunguza purchasing power ya wananchi hawa?
Purchasing power ya wananchi ikishuka bila shaka biashara nazo zitadorora,sasa biashsra zikidorora serikali itakusanya kodi kutoka wapi?
Kwa mfano,serikali inatarajia kukusanya kodi kutoka kwa wanywa bia huku tukitarajia bei ya bia kupanda kutokana na ongezeko la kodi.Sasa bia inapanda bei huku purchasing power ya mwananchi ikishuka,bia hii watamudu kuinunua wananchi wangapi?Mauzo ya bia yakishuka,kodi ya serikali itaongezeka au itapungua?
Purchasing power ya mwananchi ikishuka,huku juice,soda,sigara,n.k zikipanda bei baada ya kuongezewa kodi, mauzo ya bidhaa hizi yatashuka au yataongezeka?Mauzo yakishuka, mapato ya serikali, kwa maana ya kodi inayotokana na biashara hii, nayo siyatashuka?Yakishuka serikali haijaumia?
Mtumishi wa umma akikosa hela,mfanyabiashara bidhaa zake ataamuzia nani?Mfanyabiashara asipouza,serikali itapata wapi kodi?
Mfanyabiashara hana hela,mtumishi hana hela,nani atatutuma hela kwa mpesa,tigo pesa,n.k?Miamala hii ya mpesa,tigo pesa,n.k ikishuka, hayo makusanyo ya kodi mpya kutokana na tozo kwenye miamala hii itatoka wapi?
Mtumishi wa umma hana hela, mfanyabiashara biashara zimeyumba, watu hawa kwenye ATM watafuata nini?Safari za kwenda kwenye ATM zikipungua,kodi hiyo mpya ya transaction za ATM itatoka wapi?
Mfanyabiashara akiyumba,mtumishi akifulia,nani ataagiza gari kutoka nje ya nchi?uagizaji wa magari kutoka nje ukishuka,mapato ya kodi kutokana na uingizaji wa magari yatapanda au yatashuka?yakishuka,serikali ina faida au ina hasara?
Safari za watumishi wa umma za nje ya nchi zisizogharamiwa na serikali hazikuwa na faida kwa kuongeza mzunguko wa hela hapa nchini?
Kwa mfano,mtu akija na dola zake kutoka huko ughaibuni kwenye safari yake ya kikazi kisha akaamua kununua gari,tv,shamba,mifuko ya cement,n.k.Mtu huyo hajaongeza mzunguko wa hela?Mtu huyo hajachangia kodi ya serikali kupitia manunuzi haya?
Haya ni baadhi ya maswali ninayojiuliza na kama hatutachukua hatua mapema huku tukiwa hatuna hata viwanda,Bajeti hii iliyoongezeka kwa matrilioni huku tukitegemea ahadi za misaada na mikopo kutoka nchi wahisani,wahisani ambao wakati mwingine hawatimizi ahadi zao kwa wakati,Bajeti hii mwenzenu sijui.
NB:Msisahau kuwa serikali imepunguza PAYE kufikia single digit(hii si hela kidogo) na hapo hapo mtambue kuwa hilo punguzu la PAYE haliwezi kuongeza purchasing power ya mtumishi wa umma kwa kiwango cha kuleta tofauti na kwa bahati mbaya nyongeza ya mishahara safari hii nyongeza ambayo ingeweza ku-boost PAYE kwa upande wa serikali nayo haieleweki.
Hatari nyingine kubwa ni swala la VAT kwenye utalii.Hili swala linaweza kutupunguzia watalii na kuikosesha serikali mapato kwani watalii wengi wanaweza kutukimbia hasa wale wenye uwezo wa kati na ambao ndio wengi kulinganisha na wale wa wachache wa daraja la kwanza.