Sio siri watakuja hapa na Mapovu yao wanaomtetea Mbowe lakini ni dhahiri kushindwa vibaya kwenye uchaguzi wa kata ni matokeo ya kumuweka Zitto pembeni, na zaidi mtaona kwenye uchaguzi wa Urais na wabunge ujao, daftari kitu gani?mbona wengi waliowachagua zamani ndo wamepiga na leo?ina maana walikufa walioipenda CHADEMA peke yake?wa CCM wamebaki?ondoeni visingizio vya kitoto na mumuangukie Zitto. Huu ni mfano wa Ufanisi sifuri kwani gharama kubwa sana imetumika na huyo Mbowe lakini tumeambulia patupu. Hapo akili haikutumika bali kichwa peke yake na wengine wote mlifata, sasa tunadaiwa bela za chopa na uchaguzi tumeshindwa. Najua moderators wanaweza kuutoa uzi huu kwa sababu wanazozijua wao, lakini naomba muuache watu wachangie na msiuunganishe tafadhari.