Mzee wetu B.W. Mkapa, uko wapi? Unayaona haya?

Mzee wetu B.W. Mkapa, uko wapi? Unayaona haya?

Jumong S

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
7,427
Reaction score
10,749
Baba wa Taifa hili Mwl J. K Nyerere alikuchagua na kukuamini na hakika pamoja na mapungufu yako ulilitendea haki Taifa. Uchumi wetu ulipanda, uliinua uwekezaji, deni la Taifa lilipungua sana na ulikuwa hakika na maamuzi ya ki-uongozi.

Sasa ona, wale aliokuwa akiwakataa Baba wataifa kwa nia nzuri kuwa hawataweza kuwatetea masikini ndio wanagombania urithi wa Taifa hili. Sasa ni dhahiri, wenye pesa tusizojua wanazitoa wapi wanakusanyana viwanjani, wanapeana kampani huku wakionesha jeuri ya pesa ndio wanaelekea kutuchagulia viongozi wanyonge tusio na sauti.

Wamemuandaa kiongozi uliyempinga kwa niaba yetu ili akakikalie kit chako Ikulu. Je, mnyonge atapona? Viongozi mlioaminiwa na Mwalimu mko wapi? Hamuyaoni haya? Mbona mmekaa kimya?

TANZANIA INAHITAJI KIONGOZI MWENYE MENO MAKALI, ANAYEJITEGEMEA, ASIYEAMRIWA NA WENYE PESA.

Ndg Mkapa na wenzako mkikaa kimya mjue mtabeba dhambi hii.
 
Mkapa should act silently to put uncorruptible candidate with a vision to rise us up in presidential place
 
Huyu lazima ataelekea Butiama kesho nyie subirini mtaniambia tu ahahaaaa
 
Huyu lazima ataelekea Butiama kesho nyie subirini mtaniambia tu ahahaaaa

Hii nchi kwa sasa haina kiongozi mwenye moral authority ya kukemea maovu. Au kuzungumza watu wote wakamsikiliza. Wanaogopana. Kitendo cha Mkapa kuruhusu Kikwete awe rais ilikuwa kosa kubwa sana. Mwalimu alishatoa hint kwamba Kikwete hafai aliposema hajakomaa. Hii ilikuwa na maana zaidi. Kiufupi Kikwete hakustahili kuwa rais. Kwa sababu km mtu anasifa basi anazo tu, kukomaa gani tena? At 45km hujakomaa utakomaa tena lini? Watu wamekuwa marais wakiwa na miaka 30!!

Ilitegemewa kwamba baada ya Mkapa wa bara, zamu ingeenda Kwa Salim Ahmed Salim wa Zanzibar. Tamaa za Kikwete na kuchafuana kwa matumizi makubwa ya pesa ikampeleka ikulu. Udhaifu wake sasa umeiharibu nchi.

Lowasa anafuata njia ilelealiyoifuata kikwete. Nchi sasa hivi haina mwenyewe.
 
wenyewe ndiyo sisi bila sisi walipa kodi hakuna nchi tamareeeee


.
 
Back
Top Bottom