Habari za leo wanajamii wenzangu.
jana katika kipindi cha tutashinda cha mzee wa upako channel 10 nilimsikiliza mwanzo mpaka mwisho.kilikua ni maswali na majibu kuhusu huduma yake na mipango kiujumla maana anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa arusha.
katika maswali na majibu,mida ya saa 4:40 usiku aliulizwa swali kwamba analiongeleaje swala la dawa ya babu wa loliondo. kwanza akatolea mfano wa mfalme suleiman kwenye biblia na akasema tusiwe haraka kutoa maamuzi ya kukandia kitu au kusifia kitu,inabidi kukipa mda na kutafakari ndio mtu utamke.akaongeza kuwa kwa upande wake anaibariki dawa ya babu na atazidi kuiombea izidi kuwaponya watu,endapo tu haihusiani na ushirikina.kasema hajasikia masharti kuwa labda kainywe njia panda au rudi kinyumenyume au kupiga ramli,so iendelee kuponya watu.
pia aliongezea kuwa watanzania tusijiweke nyuma kiasi hichi.karibu dawa nyingi hata ulaya zinatengenezwa kwa mzizi. tusijiwekee fikra tu kwamba atakachovumbua mzungu ndio sahihi ila cha ngozi nyeusi ndio uongo.MUNGU ameamua kutukomboa tena kwa kupitia mwafrika. akasisitiza tunachoomba ni uzima wa wananchi maana afya ndio nguvu kazi na hitaji muhimu la wanadamu.sasa kama watu wanakunywa na kupona MUNGU na azidi kuibariki na hata huyo babu abarikiwe azidi kuponya watu alimalizia mchungaji.na pia anazidi kumuombea.atakua na mkutano arusha na amekaribisha watu waende kwa wingi kupata upako na waende loliondo kushushia dawa ya babu waponywe zaidi.maana dawa ya babu inatibu magonjwa matano ila yeye atakupa upako wa kibali kazini,kupata ajira,milango ya fedha,kuponywa mapepo,uwete na magonjwa mbalimbali.
kwa upande wangu niliridhishwa na uchambuzi alioutoa.
Ukisema hivyo unakosea Mungu ana vyombo vingi vingine vya chuma, bati, gold, almasi na babu ni moja kati ya chombo chake, si lazima mtu 1 upewe vipawa vyote na, ndo maana kuna walimu, wachungaji, wainjilisti na Manabii kila mtu ana kazi yake,Kweli babu ni chiboko, anatibu yale akina upako wameshindwa !
Ukisema hivyo unakosea Mungu ana vyombo vingi vingine vya chuma, bati, gold, almasi na babu ni moja kati ya chombo chake, si lazima mtu 1 upewe vipawa vyote na, ndo maana kuna walimu, wachungaji, wainjilisti na Manabii kila mtu ana kazi yake,
Ukisema hivyo unakosea Mungu ana vyombo vingi vingine vya chuma, bati, gold, almasi na babu ni moja kati ya chombo chake, si lazima mtu 1 upewe vipawa vyote na, ndo maana kuna walimu, wachungaji, wainjilisti na Manabii kila mtu ana kazi yake,
Kazi ya Mungu huwa haihitaji credit za wanadamu. Mwanadamu huwezi pima njia za Mungu, hutatofautiana na yule aliyetaka kukausha bahari kwa kikombe na kujaza maji yote kwe kishimo kidogo alichochimba. Acheni Mungu aitwe Mungu.
Babu ametumwa na CCM kula muda wa kuijadili Katiba,Dowans,Kiwira,IPTL na kashfa nyingine.Hana lolote.....msanii tu
mh! sidhani kama ni kweli, kwani wagonjwa waliotoka mahospitalini walikolazwa kwa muda mrefu ndo wadau wakuu wa majadiliano ya dowans na ....? by the way babu hajamwita mtu, wanamfata wenyewe na dawa yake sio ya kutibu kuongea na kuziba midomo bali inatibu magonjwa sugu tu 'kwa mujibu wake' hivyo watu kushindwa kujadili hoja kusihusishwe na babuBabu ametumwa na CCM kula muda wa kuijadili Katiba,Dowans,Kiwira,IPTL na kashfa nyingine.Hana lolote.....msanii tu
mzee wa upako kajitahidi kusema vyema.
waacheni wanaoamini kwa babu waende kwani la msingi ni kupona tu
Lusekelo mjanja...kaangalia upepo unakovuma nae akaelekea hukohuko, kwasasa ukitaka ulaaniwe wewe sema dawa ya babu ni kimeo!
Lusekelo is a sort opportunistic buddy! big up mzee wa upako...wewe ndio unajua jinsi ya kuendesha biashara ya dini kuliko Kakobe na Mwingira.