Mzee wa miaka 65 ampa mimba mwanafunzi wa miaka 16

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamtafuta mzee wa umri wa miaka 65 Dominick Kweka wa kijiji cha Kisereni wilayani Hai kwa tuhuma za kumbaka msichana wa miaka 16 ambaye ni mtoto wa dada yake (Mjomba) na kumpa ujauzito ambao sasa una umri wa miezi sita.

Akizungumza na ITV kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Bw Wilbrod Mutafungwa amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa juhudi za kumsaka zinaendelea ili afikishwe katika vyombo vya sheria.

Bw Mutafungwa amesema, jeshi la polisi katika mkoa huo halitavumilia kuona vitendo vya ubakaji vikiendelea kutokea kwa watu wa aina hiyo ambao wanakatisha maandalizi ya maisha bora ya wanafunzi wasichana.

Msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Nkuu amesema, mjomba wake huyo alimbaka nyumbani kwake wakati alimpopelekea sola kwa ajili ya kuichaji ili apate nafasi nzuri ya kujisomea nyakati za usiku na ameiomba serikali aendelee na masomo baada ya kujifungua.

Baba mzazi wa msichana huyo Bw Kilasauko Nyuki ameiomba serikali imchukulie hatua kali za kisheria mzee huyo mwenye makazi katika kijiji hicho na majiji ya Arusha na Dar es Salaam ambaye inadaiwa ametoroka baada ya tukio hilo.

Chanzo: ITV
 
Mzee wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Nkuu Kisereny mwenye umri wa miaka 65 amempa ujauzito binti mwenye umri wa miaka 16 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Nkuu iliyopo maeneo ya Machame wilaya ya Hai.

Hali hiyo imezua taharuki baada ya wananchi wenye hasira kali, hususani wazee kujitoa kumtafuta mtuhumiwa, huku wakidai kuwa wamechoshwa na vitendo vyake vya kuwarubuni mabinti wadogo kwa kuwapatia vizawadi vidogovidogo.

Chanzo: Mwananchi
Jina la Mzee!!
 
Haaaaaaa Asante kwa taarifa ya kutosha kuhusu viongozi wa dini wa kwanza kufika kanisan wanakaa kwenye viti vya heshima kumbe wanachunguza wengine na watoto. Lakini hii taarifa yako mpaka utaje cheo cha MTU mmmmhh
 
Jamaa apigwe mvua ya ya miaka 30 jela fasta hamna uchunguzi wala nini ili kupisha kazi nyingne za kiutendaji ktk mahakama zetu! 95 arudi kulea mtoto wake atamkuta akiwa na miaka 30+!!
 
Huyo akikamatwa nae apewe ujauzito tu......mtoto wa miaka 16 ni mjukuu wke kamharibia maisha
 
Mzee wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Nkuu Kisereny mwenye umri wa miaka 65 amempa ujauzito binti mwenye umri wa miaka 16 ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Nkuu iliyopo maeneo ya Machame wilaya ya Hai.

Hali hiyo imezua taharuki baada ya wananchi wenye hasira kali, hususani wazee kujitoa kumtafuta mtuhumiwa, huku wakidai kuwa wamechoshwa na vitendo vyake vya kuwarubuni mabinti wadogo kwa kuwapatia vizawadi vidogovidogo.

Chanzo: Mwananchi
Mchungaji wa kondoo anapokula kondoo wake.......
 
najiuliza why umeandka mzee wa kanisa kkt,na si kuandka jina lake au kusema tu mzee mmoja.
 
Jamaa apigwe mvua ya ya miaka 30 jela fasta hamna uchunguzi wala nini ili kupisha kazi nyingne za kiutendaji ktk mahakama zetu! 95 arudi kulea mtoto wake atamkuta akiwa na miaka 30+!!
akifungwa mtoto atalelewa na nani?
 
Back
Top Bottom