Mzee wa maajabu

Mzee wa maajabu

Tape measure

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2015
Posts
1,988
Reaction score
3,688
Ilikua juzi nipo maeneo ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza, nilienda kufuatilia zoezi la upimaji wa viwanja unaoendelea. Basi nikiwa na wenzangu wawili tukapanda kwenye gari aina ya corolla oldmodel manual kufika njiani tukakuta barabara imekatika hivyo wenzangu wakaendelea na safari kwenda kuonyesha viwanja vyao vilipo.

Nikabaki mimi na dereva tunawasubiri warudi kusudi na mimi niende nikaonyeshe eneo langu lipimwe katika kuwasubiri kulikua na miti ya miembe nikawa nimeenda kuyaangalia kama kuna yalioiva basi nikaanza kurusha vimiti kuyalenga yalianguka kiasi nikaendelea kwa muda kuyalenga bila kupata nililolitegemea.

Ghafla nikamuona mzee analima jirani na nulipokuwepo nikashtuka kwani kwa muda wote sikumuona mtu akilima katika eneo hilo wala kipindi anakuja sikumuona.

Nikamsalmia mzee akiwa kwa umbali wa mita kama 30 akaitika nikaendelea kurusha miti kugonga maembe dereva nilimwacha kwenye gari alikuwa bizy anapiga simu kwa watu wake nazani alikua na kifurushi.

Mara mzee akaniita boss naomba usogee kidogo nikamfuata huku nikiwaza akilini labda huyu mzee amezani na mimi ni land surveyor? Wakati na mimi nina shida any way nikaendelea kumfuata nisikie anachotaka kunieleza nikamkaribia akaniambia unajua hili shamba langu nimelilima kwa mda na mara kwa mara huwa naokoto pesa za zamani hapa akanionyesha pesa aliokota siku hiyo, ilikuwa ni coin ya 1912 ya Uingereza alikuwa pia na Tsh 20 na nyingine kama kumi na kitu ivi..

Wakati naendelea kumsikia gafla wale walioenda kuonyesha viwanja vyao wakarudi na mtaalam akawa ananifuata mimi kusudi niende kumuonesha eneo langu basi nikamwambia mzee nisubiri hapa endelea kulima nitarejea muda si mrefu akawa ananiuliza kwani hizi pesa watu wanazitaka kwa ajili ya kazi gani? Nikamjibu makubusho huku naondoka kuelekea kuonyeshaa mpimaji eneo langu

Nilipomaliza nikaachana na wapimaji nikarudi taratibu kwa mguu ilinichukua kama dakika 9 hivi kufika eneo lile ajabu mzee sikumkuta wala eneo nililoona mwanzoni limelimwa halikua na dalili ya kulimwa kabisa kwa siku hiyo.

Nyayo zangu zote za viatu nilipokanyaga wakati namfuata niliziona lakini cha ajabu sikuona unyayo wa mzee popote alipokanyaga. Niliuliza watu wa maeneo ya pale kama wanamfahamu mzee ambaye analima eneo lile kila mtu alisema hamfahamu,? Kwakuwa nyumba zilikua mbalimbali nilikaa pale kwa muda kuulizia kumjua yule mzee lakini sikupata dalili ya kumuona nilishindwa kumfananisha na matapeli wa mjini kwa kuwa eneo nililokutana nae nilikuta limebadilika halijalimwa na halina dalili ya mtu kuwapo katika eneo lile.

Nilipiga picha coin moja tu aliyoiokota siku ile na kuondoka nikitegemea kwa kuwa ndio alikua kafika basi ndani ya mda mfupi nitakaorudilazima nmkute wala sikuona umuhimu wa mimi kuchukua namba zake za simu.
Mpaka leo siamini kama kweli yule mzee alikua ni binadam kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushaona mauzauza halafu unakaa kusubiri?!
Kwahyo ulovyorudi hata coin hazikuwepo tena?!
 
Kama ni chai sawa ila kama ni kweli nimeshindwa kukuelewa, yaani unaulizwa issues ambazo unafaham mtiririko wake alafu unaleta hadithi duu...
🙄
 
Nako kuvamia mashamba ya watu na kuanza kutungua matunda si kuzuri! Alikuwa anakuonya kistaha kuwa wacha kuangusha embe hovyo, hapo ndipo anaokoteza visenti vyake mara nyingi kwa kuuza hayo matunda!
 
Back
Top Bottom