Steph Curry
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 5,939
- 4,706
Habari zenu wana bodi...
Uzi huu unaweza usiwahusu watu wengi humu ila baadhi unatuhusu na pia nimeandika kufikisha ujumbe kwa Mzee wangu na Role Model wangu Mzee Mengi.. Siko hapa personally kumshambulia ila niko personally kufikisha ujumbe kwake kupitia njia hii niliyoiamua...
Kwanza kabisa kuhusu ushiriki wa Mzee wetu kwa maendeleo ya Watanzania, hapa tunakupongeza sana kwakuwa tunaona ukisaidia jamii mbalimbali zenye mahitaji. Lakini hapa pia tunaona jamii yako ya wachagga hasa wamachame ni kama umewasahau, ni kweli wachagga hasa wamachame hawahitaji msaada wowote mkubwa kwakuwa jamii hiyo inajiweza ila Mzee hata ukiamua kusaidia mambo madogo madogo utakuwa umefanya vyema kwa ndugu zako. Hapa binafsi nina visa viwili vya kuelezea ambavyo kama nilidanganywa basi naweza nikapata ukweli kutoka kwako au kama ndivyo basi inawakosea sana ndugu zako..
Kisa cha kwanza, ni miaka ya 2008/9 uliahidi kutoa ng'ombe wa kisasa mmoja kwa kila kaya kuanzia pale Makoa mpaka kijiji cha mwisho kabisa cha Nkweshoo vijiji hivyo maarufu vinafahamika kama MACHAME CENTRAL, ukawaambia waandae mabanda ya kisasa na wenye ng'ombe juu ya watano waanze kuuza na kupunguza mifugo yao ili kumu'accomodate ng'ombe huyo utakayemtoa. Kila kaya ilichangishwa mchango wa elfu kumi (10,000) na nakumbuka kwa kijiji changu pesa alipewa Mama Paul Muro. Baada ya wanakijiji kutoa hiyo michango mkaleta habari ya maji ambayo wanakijiji wanayatumia bure kwenye mabomba yao mkataka muuziwe ile chemichemi nyie muwe ndio wamiliki ndipo mtatoa hao ng'ombe. Wanakijiji wote wa Machame Central kwa umoja wao walikataa na mkawarudishia pesa zao. Inavyosemekana ni kwamba Mzee ulikuwa unataka maji hayo wanayotumia ndugu zako bure uyapeleke kule hospital ya Moyo ya Mutie Mengi ilipokuwa inajengwa..
Kisa cha pili, ni hili suala la kujenga barabara ya rami kuunganisha vijiji vyote vya Machame Central kuanzia pale Makoa mpaka kule Nkweshoo. Kwanza ni aibu kwako Mzee wangu pamoja na matajiri wenzako wa huko kupita kwenye barabara ya mbovu kama ile mkiwa na magari yenu ya kifahari. Mdogo wako kila siku anapita barabara hiyo asubuhi na jioni akienda na kutoka kazini. Mmefanya busara sana kuanzisha mchakato kwa kuijenga ile barabara ukizingatia pia na Mkuu wa Kanisa la KKKT anatoka huko Machame Central kutakuwa na ushawishi wa hali ya juu kuijenga barabara hiyo ambayo mnasema mwezi wa nane ndiyo mtaanza mchakato wa ujenzi baada ya kukamilisha michango. Ila cha kusikitisha nimesikia Mzee wangu Mengi umetoa Million 40 wakati matajiri wadogo tu wasiofahamika wametoa mpaka million 50 kila mmoja.. Mzee wangu kwa jina ambalo unalo na marafiki na ushawishi hatukutegemea kama utatoa kiasi hicho, ingawa nimesikia umesema hapo ni kwa kuanzia tu basi Mzee tunaomba kweli huko mbeleni ujiguse tena usikae kimya. Mzee kumbuka tu shida uliyopata ulipoenda kuzika mtoto wako mpendwa Mutie, na tunajua kila mwaka lazima uende kusalimia na unapita hiyo barabara, hebu tufunge mkanda kujenga hii barabara wakati huu na tuache blah blah.. Hili la barabara pia hatutegemei mtakuja baadae kuwaambia wanakijiji ili kujenga barabara hii basi mtupe kitu fulani.. Tunategemea hili mnalifanya kizalendo kabisa..
Wito kwa wote kutoka Machame Central, tutoe michango yetu kwa wakati ili kufanikisha hili jambo ili tunapoenda December tukute angalau barabara imejengwa.. Mzee Mengi kwa hili tunaomba ujitoe haswa kulifanikisha maana hatujui kwanini kwako barabara sio kipaumbele. Hata hapo ITV barabara ya kuja ofisini kwako ni mbovu sana na Mzee wala hujigusi kuirekebisha..