Mzee Peter Kisumo: Mashindano ni Kitovu cha u-Bepari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee Peter Kisumo: Mashindano ni Kitovu cha u-Bepari

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Estmeed Reader, Apr 19, 2010.

 1. E

  Estmeed Reader Senior Member

  #1
  Apr 19, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna habari, iliyoandikwa na Daniel Mjema kutoka mjini Moshi (Mwananchi, 4/16/2010), yenye kichwa, Sheria ya DSE imechafua sifa ya nchi:

  MWENYAKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya simu ya Vodacom, Peter Kisumo amesema sheria mpya ya inayoyabana makampuni ya simu kujisajili Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE), imeichafua sura ya Tanzania.

  Kisumo, ambaye ni mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, aliliambia Mwananchi jana kuwa tayari wawekezaji wa kimataifa wameingiwa na hofu ya kuja nchini kuwekeza na wanaitaka serikali kuchukua hatua za haraka kujisafisha.

  nachoweka sharti kwa makampuni hayo kujisajili DSE kwa hisa za Watanzania, ni kibaya kwa kuwa kinakiuka hata masharti ya leseni ambayo Vodacom ilipewa wakati ikianza shughuli zake.

  Kisumo alisema serikali inapaswa ikumbuke kuwa wakati Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiingia madarakani, alibadili sera na kuruhusu makampuni binafsi kuwekeza nchini na iliwahakikishia kuwa hawataingiliwa ili mradi walipe kodi.

  “Sisi kama Vodacom Tanzania na Vodacom South Africa tulishaenda kwa rais tukamwambia kwamba kwa sheria hii wanahisa wanahofu kuwa umiliki wa mali yao unaingiliwa na tulieleza hilo kwa kamati ya Bunge,” alisema.

  Kisumo alifafanua kuwa leseni ya Vodacom ni ya miaka 25 na hakuna sehemu katika masharti ya leseni hiyo inayoeleza kuwa watatakiwa kujiunga na DSE na masharti hayo ndiyo yaliyowavutia Vodacom kuwekeza nchini.

  “Tunakubali kuwa masoko haya ya mitaji ni njia mojawapo ya njia za kuongeza mitaji kwa hiyo ilipaswa iwe ni hiyari kwenye kampuni kwenda kwenye soko hilo... kwanini unilazimishe nitakatafute mtaji DSE,” alihoji Kisumo.

  Alifafanua kuwa hapa nchini kuna kampuni karibu tano zinazotoa huduma ya simu za mikononi, kwa hiuyio kulazimisha zote ziingize hisa zake DSE ni wazi hata thamani ya hisa zitashuka kwa sababu zitafurisha soko kwa wakati mmoja.

  Kisumo, aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali ya awamu ya kwanza, alimpongeza Rais Kikwete kwa kukataa kusukumwa kusaini sheria kwa kuwa ingesababisha madhara makubwa kwa nchi katika suala la uwekezaji.

  “Ni jambo geni kabisa kwa Tanzania kwamba Bunge linapitisha sheria ambayo haijakamilika halafu rais anakataa kusaini na anaagiza yafanyike marekebisho na ikumbukwe wadau walipigia kelele sana kifungu hicho,” alisema.

  Mwenyekiti huyo wa Vodacom alisema hataki kuingilia namna serikali inavyofanya kazi yake hadi miswada ya sheria inakataliwa lakini akasema matukio hayo yanawatia shaka wananchi kuhusu umakini wa watendaji.

  Alisema ni jambo la ajabu sana kwamba serikali inatunga sheria mpya inayokinzana na masharti ya awali waliyopewa wawekezaji kabla ya kuwekeza nchini lakini serikali haitaki kujadiliana kwanza na wawekezaji hao.

  “Sheria ikitungwa hairudi nyuma, inatakiwa ianze kutumia kuanzia pale iliposainiwa na rais sasa uhalali wa sheria hii kuyabana makampuni ambayo yalipewa leseni miaka mitano iliyopita unatoka wapi,” alihoji Kisumo.

  Kisumo alisema picha iliyoanza kujengeka kwa wawekezaji ni kwamba Tanzania ni nchi ambayo ni kigeugeu kwamba inawaahidi wawekezaji mazingira mazuri, lakini baada ya muda inabadilika kama kinyonga.


  Kuna kisa cha Microsoft kupelekwa mahakamani huko Ulaya Magharibi (hivi majuzi) kutokana na kile kiitwacho “unfair business competition”, kwa mmiliki wa “operating system” za komputa kuwazuia wakinzania wengine wasinufaike. Microsoft ilibidi kutii amri. Mashindano ndicho kitovu cha u-bepari!

  Mzee Peter Kisumo amezua, kama hilo la Microsoft! Sijui hili lilitoka moyoni mwake, yaani, ndiye “progenitor” (kalizalisha yeye mwenyewe binafsi) ama anatumiwa tu na wanyonyaji wakuu wa kampuni ya Vodacom, na wengineo wenye dhamira ya ku-“monopolize” biashara hiyo ya simu?

  Mimi si bepari. Lakini yafaa sana Mzee Kisumo na hao wenzake watambue yafuatayo:
  Ø Kulingana na tamko la babu wa u-bepari wa Ulaya Magharibi, Adam Smith, mashindano hayo eti ni nafuu kwa mlaji: bei ya bidhaa na huduma itateremka! Inakuwa ni kama kuvuja kwa pakacha, nafuu kwa mchukuzi!
  Ø u-bepari unajikita katika mashindano, kama hayo Mzee Kisumo anayokataa. Adam Smith u-bepari unajikita katika mashindano ya soko huria (“the magic of the market”! Unayeshindwa, hutupa ndani taulo na kuwaachia washindi.
  Ø Sasa Mzee Kisumo anatwambia kuwa “monopoly” ni kitu kizuri. Si ajabu, kuna siku atatwambia pia kuwa “oligopoly” ni kitu kizuri sana: Ya samaki mkubwa kumumeza samaki mdogo, kupitia “mergers”!
  Ø Mwisho, hawa wazee wetu waliolea Ujamaa wa enzi za Nyerere leo hii wameona mwanga wa u-bepari (mithili ya Bwana Robert McNamara wa Marekani hapo baadaye kukana vita ya Vietnam na kumbe yeye ndiye alikuwa mpikaji wa sera za vita hiyo)!
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Hawa wazee wanatumiwa tu. Sidhani Kisumo ana hata hisa moja katika Vodacom. Lakini anaweza kufungua milango ya ofisi nyeti. Kumbuka kabla ya hapo Mwenyekiti wa Vodacom alikuwa Pius Msekwa wakati huo bado ni Spika wa Bunge. Watu walipohoji kuhusu kuwepo mgongano wa maslahi akawakebehi kuwa wana "wivu wa kike". Hizi ndizo ishara za nchi kushikwa na mafisadi.
   
 3. P

  Preacher JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kampuni kuuza hisa zake kupitia DSE (soko la hisa la Dar es Salaam) - ina maana waTZ nao wawe wana hisa na kupata faida kwenye kampuni hiyo pale ifanyapo biashara - sasa shida ya Mzee wetu huyu ni nini??? Kampuni iko Tanzania, inafanya faida - badala ya kufagilia wananchi wakanufaika - anapinga. Mie naona ifuatavyo:

  1. Hana elimu ya kutosha kuhusu Stock Exchanges wala money markets
  2. Anadhania kila kitu ni siasa (kutetea kwa vile ni mwenyekiti) - asijali as long as ni mwenyekiti - posho yake ipo pale pale pamoja na zawadi anazopewa kama mwenyekiti.

  Tunasubiri kwa hamu makampuni yajiunge - tununue hisa nasi tuinuke kiuchumi ingalau kwa kidogo.
   
 4. N

  Namdawa Member

  #4
  Apr 23, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nadhani kuna umuhimu wa kwenda ndani zaidi na kuona lipi la kumfaidia mtanzania na sio mgeni lakini tuwe na udadisi yakinifu ili tujue lipi la kushika na sio kurupuka tu
   
Loading...