Waterlemon
Senior Member
- Sep 2, 2016
- 143
- 199
Mzee mmoja (kwa jina tutamhifadhi) aliyekuwa akiishi huko visiwani Pemba alibahatika kuoa wake wanne…. (Aaah bwana usimsimange, wanaruhusiwa kuowa wake wanne!)
Tutasema kubahatika maana kuoa ni bahati na rehma, lakini ukimuuliza mwenyewe huyo mzee atakwambia ya kuwa alipata bahati mbaya ya kuoa mara nne. Alikuwa ni mzee mwerevu sana tena hodari katika kutafuta rizki. Siku zote alikuwa akijituma kuchapa kazi kwa bidii na kujitaftia rizki iliyo nzuri kwa kibiashara chake cha kuuza karafuu na mazao mengine pamoja na bidhaa kadhaa huku bara tena kwa njia halali na kuishughulikia familia yake inavyotakiwa. Lakini tatizo lake ni hilo moja tu, hamna hata mmoja katika hao wake zake wanne ambao wana maelewano mazuri. Kila siku ugomvi kwa kila mmoja. Kuparurana kwa hili au kwa lile siku nenda siku rudi! Alioa kuanzia wa kwanza akihisi huyu ndio the one, lakini kadri siku zilivyoenda maelewano yalizidi kupotea. Ndio maana akajiongezea wapili lakini yakawa ni yale yale… wa tatu, nae olaaaa…. mpaka huyo wa nne. Na wote wakawa headache baada ya headache…
Siku moja mida ya jioni baada ya kuparurana na wake zake, mzee akaamua kwenda zake pwani akanyooshe miguu na kupoteza mawazo. Akijieka nyumbani atarusha vibao buree, na yeye hapendi kupiga piga.
Katika kujitembeza kwake pwani, akaona kitu kinang’aa kimefunikwa na mchanga. Mzee akasogea karibu na kukifukua kile kitu kinachong’aa. Ilikuwa ni birika moja ya dhahabu, ndogo tu lakini yenye kupendeza sana. Tena inaonekana yenye thamani kubwa. Akaangalia huku na huku kuona kama kuna mtu karibu, pwani ilikuwa na watu wachache sana, tena kila mtu na shughuli zake.
Mzee akaona bahati iliyoje hii.. “ Birika hii nikiiuza nitapata pesa nyingi sana za kuwanunulia zawadi wake zangu. Au hata nikiiyeyusha nitapata dhababu kiasi cha kutosha cha kuwapatia jewellery wake zangu. Itawafurahisha sana hii yaani”… akajiwazia huku akichukua ile birika na kuitia chini ya shati alilovaa akiificha ili akasokomee nayo kwa sonara kisiri siri.
Vile anaharakisha kupiga hatua akimbie nayo, ile birika ikajisugua na ubavu wake ndani ya shati lake. Ghafla likatoka jini kubwa kutoka humo ndani ya birika. Jini likamsimamia mbele yake, kifua kimetuna, uso kaukunja kwa hasira, sharubu zinatikisika, mikono kaifunga kifuani kwa hamaki huku macho makali kamtolea yule mzee.
Jini: Ni nani huyu aliyethubutu kunisumbua mida hii kwa kunitoa kwenye makazi yangu. Nilikuwa nimejipumzisha na starehe zangu yaani, naangalia movie zangu za vituko vya mzee Majuto na kinywaji changu pembeni…
…(Jini likifoka kwa hamaki)…
…Nishachoshwa na viumbe nyie. Kila mara mkiniita huwa mna madai mengi tu. Hamtoshelezwi. Kila mara mnataka madai matatu matatu. Sababu ni wajibu wangu kutekeleza madai unayotaka na umenitoa kwenye starehe zangu, basi nitakutekelezea moja tu kati ya matakwa yako matatu. Haya Upesi, sema jambo unalotaka nikutekelezee…
Mzee (akitetemeka huku akifikiri kwa makini la kuomba): Ermmm… mie hufanya biashara zangu bara, lakini kusafiri kwa meli au kwa ndege siwezi. Hupata tabu sana. Sasa naomba unitengenezee daraja la kuvuka kutoka huku visiwani mpaka bara niwe naenda kwa gari au kwa pikipiki yangu. Itanirahisishia sana mheshimiwa Jini.
Jini (Kwa kufoka na hasira nyingi zaidi): WEWE U MZIMA KWELI? Nimesema omba jambo rahisi kutimiza. Unajua muda gani itanichukua kutengeneza hilo daraja. Kiasi gani cha sementi itakayotumika? Matofali na nondo zitakazochukua kuliimarisha hilo daraja? Na hiyo namna ya kuchimba misingi humo ndani ya bahari? Na nyaya za kulisimamisha hilo daraja? HAMNA SIFANYI HILO. Kazi kuomba mambo makubwa makubwa tu mnahisi yote hayo yanapatikana bure? SIWEZI HATA KIDOGO KUKUTIMIZIA HILO. ABADAN!... UPESI OMBA JENGINE. HILO SIKUFANYII ASILANI….
Mzee(akafikiria kidogo tu): Nimeoa wake wanne. Wake zangu kila siku wanasema siwapi huduma zinazostahili na siwajali pamoja ya mapenzi yote niliyonayo kwao. Basi naomba unipe uwezo wa kuwa nawafahamu uzuri wake zangu na niwe nafahamu yanayopita kwenye vichwa vyao na kujua wanayofikiri wakati wakinuna. Kujua kinachowasikitisha wakilia na kujua namna ya kuwafanya wawe na furaha.
Jini: Je unataka hilo daraja la kuvuka kwenda bara liwe na lami au kokoto?....