MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
Mtei amesema ili Watanzania wengi, wapate fursa ya kutoa mchango wao katika kuendeleza Taifa ni muhimu kuwepo mabadiliko ya Katiba ambayo yatawezesha kuundwa serikali ya mseto baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.
Anasema haiwezekani watu wanaungwa mkono na watu wengi, lakini baada tu ya uchaguzi wanakosa fursa ya kutoa mchango wao kwa maendeleo ya taifa.
“Mfano, Chadema tuna wafuasi wengi sana sio vizuri kuwaacha hivi hivi, baada ya uchaguzi ni muhimu wapate fursa kupitia muungano wa vyama kushiriki katika ujenzi wa taifa lao,” alisema.
Mtei alisema wakati Watanzania, wanamkumbuka Mwalimu ni muhimu pia kuendelea kushirikiana kwa pamoja kudumisha amani na utulivu katika taifa na kujitahidi kuondoa tofauti za kisiasa ili zisiwe chanzo cha vurugu.
Kuhusu Uongozi wa Rais Magufuli.
Mzee Mtei anasema Rais John Magufuli anafanya kazi nzuri katika kuimarisha uchumi na anapaswa kuungwa mkono, lakini kuna mapungufu kuhusu masuala ya demokrasia na uhuru wa watu.
“Rais anafanya kazi nzuri sana, uchumi unakwenda, lakini pia amerejesha nidhamu serikalini na sasa watendaji wa serikali wanatoa huduma nzuri kwa wananchi,” alisema.
Alisema angependa Rais Magufuli, kuungwa mkono katika mambo mazuri ambayo anafanya ingawa bado hajafikia uwezo wa Baba wa Taifa.
Mtei alisema hata hivyo, Rais anapaswa kuwashirikisha watu wengi katika uendeshaji wa nchi, kwani kuna makundi mengine wakiwepo wapinzani wamewekwa nyuma jambo ambalo sio zuri.
CHANZO: Gazeti la Mwananchi.