Mzee Makamba apingwa Bumbuli

Mzee Makamba apingwa Bumbuli

mghoshimgima

Member
Joined
Sep 20, 2014
Posts
6
Reaction score
0
Kwa muda mrefu kumekuwa na mzozo kati ya mzee Yusuph Makamba na viongozi wa BAKWATA wilaya ya Lushoto kwa kuwa mzee Makamba hautambui uongozi wa BAKWATA wilaya hiyo.

Mzee Makamba alianzisha taasisi yake ya dini bila ridhaa ya BAKWATA wilaya ya Lushoto lakini akafanikiwa kuisajiri bila kushirikisha wilaya ya Lushoto na kumekuwa na mizozo mikubwa ambayo mingine ilibidi hata polisi kuingilia kati baada ya dalili za machafuko, leo hii huko nyumbani kwa mzee Makamba, Mahezangulu waislamu wamegawanyika na taasisi yake imechukua mali zote za waislamu ambazo mzee Makamba aliwahi kuzichangia na kuziweka chini ya taasisi yake.

Baada ya kuona BAKWATA wilaya ya Lushoto haimuungi mkono, mzee Makamba amepigania chinichini kupata BAKWATA wilaya ya Bumbuli, maana sasa Bumbuli ni halmashauri ndani ya wilaya ya Lushoto, lakini nia yake kulazimisha iwepo BAKWATA wilaya ya Lushoto, baada ya kutumia njia zake akafanikiwa kupata usajiri kinyuma na utaratibu unaotakiwa na yeye mwenyewe kuteua viongozi wa
BAKWATA hiyo.

Tofauti na matarajio yake, alipoitisha mkutano wa viongozi wa bakwata na masheikh ndani ya bumbuli, viongozi wale waliipinga na kumuambia hawatambui utaratibu huo na shekh wa mkoa wa Tanga aliyetumwa kuongea nao alishangaa alipoambiwa ukweli na kuona msimamo wa waislamu wale, na kwakuwa yeye alitumwa na mzee Makamba akawaambia viongozi wale waandike barua ya kupinga ndio viongozi wale wa kata 14 kati ya 16 ndani ya bumbuli walipo sign kupinga mpango huo wa mzee makamba.

Itakumbukwa pia mzee makamba amemshitaki mwenyekiti wa
BAKWATA wilaya na kumdai fidia ya mil 20 kwa kuwa alimpinga hadharani.

Barua ya waislamu imeambatanishwa.

Huu ni muendelezo wa upinzani anaoupata mzee makamba na mwanae ndani ya jimbo la Bumbuli.


attachment.php
 

Attachments

  • bumbuli.jpg
    bumbuli.jpg
    21.6 KB · Views: 1,982
Sredi nyingine mmm,,,,,!!!!!!kazi kweli kweli
 
Ngoja nimuulize mzee makamba kama n kweli.Msizalilishe uislamu bhana!
 
January mwambie baba yako wakati wake umepita awapishe vijana
 
kwani mzee makamba ni muislamu? anaitaka pepo bila kuitolea jasho! aende zake akafuge nguruwe huko.
 
Huyo Mzee ndiye alieanzisha udini hapa Dar es Salaam na alanike yeye na kizazi chake kutumia dini kwa manufaa yake binafsi na wanawe pepo hilo
 
Sijaelewa, familia hii ya Makamba wanaotaka kutawala siasa ya Tanzania kupitia CCM, wamekuja kwenye dini tena. Ni shiiida
 
Family ya Makamba iliota makubwa mapema mno, warudie unyenyekevu ili wawe na harufu nzuri kama zamani
 
Kwa mwenye kumbukumbu nzuri, hivi January Makamba ni mkristo au muislamu? Nasikia huyu mzee ana wake 2, bimkubwa ni mkristo while bimdogo ni muislam, kwa ane jua please!
 
January ni mkristo ila anaficha sana watu wasijue... Kupata support ya waislamu...
Mama yake pia ni mkristo
Mzee makamba ni muislamu wa jima...
 
Naona team Membe mmeanza kutunga tunga uongo! Wiki mbili zilizopita mlikuja na ka heading fulani hivi mkitaka kumchonganisha Mzee Makamba na Mh.Wakawashtukia sasa mmekuja kwa mwanvuli wa Bakwata.Poleni sana.
 
Si akawaambie Boko haram au ISIS waje wamsaidie? Wazee wengine bana, halafu akipingwa anasema kadharirishwa na vijana hawana adabu.
Yaani misaada yake ndo iwatese waislamu wengine? Au anataka watu wajue na yeye bado yupo?
Hivi ni mshia au Sunni, au ahamadiya? Kama mi mshia dawa yake ni ISIS!!!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom