Mzee Lowassa atakumbwa na upepo wa UKAWA

Mzee Lowassa atakumbwa na upepo wa UKAWA

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,981
Reaction score
17,380
Alisababisha mvurugiko wa sasa ndani ya CUF na Chadema wakati anaachiwa kugombea Urais kwa tiketi ya UKAWA hatua ambayo ilisababisha LIpumba na Slaa kutimkia kusikojulikana. Kuondoka kwake UKAWA na kurudi CCM ni sawa na kuwapiga kisu mgongoni wale wote waliompigia kura 2015.

Kurudi CCM ni haki na hiari yake, lakini hakuna haki bila ya wajibu, wajibu wake kwa wale waliompigia kura UKAWA ni upi wakati anatimiza haki yake ya kurudi CCM?

Mzee wetu nadhani anastahili kuwalipa wale wote waliovuja jasho na damu zao kwaajili yake mwaka 2015 vinginevyo watamuadhibu vibaya sana kisiasa, kijamii na kibiashara. Akumbuke kuwa upinzani sio CUF na Chadema bali ni itikadi ya watu wanaotafuta tofauti kwenye siasa. Yaani hata uwape tende na halua bureee majumbani mwao ni bure kwao, watataka mabadiliko. Hivyo hakuna mtu mmoja peke yake anayeweza kuzima fikra zao hizo za kutaka mabadiliko. Mtu anaweza kuwachelewesha watu hao kwa muda tu hadi muda fulani lakini sio kumudu kuwazuia kabisa milele. Hivyo mzee wetu Lowassa amefanikiwa tu kuingia kwenye historia ya orodha ya watu waliojaribu kuchelewesha mabadiliko ya watu hao kama vile wale waliofanikisha kuwachelewesha akina Mzee Nyerere, Kenyatta, Obotte, Nkrumah, Lumumba, nk kupata Uhuru wa nchi zao lakini wakashindwa kuwazuia kabisa milele wasipate Uhuru.

Binadamu wana tabia ya kupenda mabadiliko kuanzia ngazi ya mtu binafsi, familia, jamii, taifa na dunia. Waliyatafuta mabadiliko tangu enzi ya zana za mawe za kale hadi zama za leo, tangu zama za ujima hadi zama hizi za ujamaa na ubepari, tangu usafiri wa kutembea kwa miguu hadi kusafiri kwa ndege, ni mabadiliko, mabadiliko, mabadiliko kwa kwenda mbele, hakuna anayeweza kuyazuia, chamzingi ni kuyawekea groves (njia rasmi, pana na sahihi) yatakamopitia kuelekea kule yanakoelekea ili yasisababishe madhara kwa wanajamii wanaopakana nayo. Kule Venezuela walishindwa kuyawekea groves hivi sasa yanakaribia kutaka kupitia popote kwenda yanakokwenda.

Upepo wa wapenda mabadiliko ukikukumba huamki tena labda upelekewe mbeleko ya kubebewa.

Dalili kubwa za watu wanaokumbwa na upepo wa wanamageuzi ni:

1. Kuwa na hofu kila wakati
2. Biashara zako zinasuasua
3. Utalindwalindwa kila wakati
4. Unaweza kupata sonona
5. Heshima kwenye jamii inapungua kidogo au sana kuliko zamani
6. Usingizi unapotea
7. Jamii inakutupa mkono kwenye mambo yako
8.
9.
 
#Amani_Na_Upendo utakapokuwa #Msingi_Wa_Upinzani_Wetu (Sisi Wenye Damu Za Upinzani) ndipo tutauondoa #ulumumba .
 
Sera ya manunuzi ya wapinzani imehama toka kwa wabunge kwenda kwa viongozi maarufu .
 
Inavyoonekana wale wanaopenda utofauti wa mambo ni wengi kuliko wanaojitokeza, ndio maana kila aliyewadhihaki hasimami kwa miguu yake tena bila kupata mbeleko fulani.
 
Back
Top Bottom