Mzee Fumbuka kaandika haya someni kuhusu Nyerere

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,804
8,797
Asanteni sana marafiki kwa kutenga muda na kunitumia salamu za heri na fanaka nilipokuwa natimiza umri wa miaka 67 hapo jana. Shukrani sana!

Niliwahi kusema miaka mingi iliyopita kwamba, yalikuwa ni makosa makubwa sana Nyerere kuwa Rais wa Tanganyika na baadaye Tanzania. Matatizo makubwa ya msingi yanayotusumbua hadi leo, yaliasisiwa na Nyerere! Umasikini wetu, ujinga tulionao, Katiba mbovu tuliyonayo, CCM yenyewe, sera ya serikali mbili, sera ya kofia mbili kwa kichwa kimoja, nk mwasisi wake ni Nyerere!

Mapema kabisa, Miungu [ninaamini katika mizimu], ilimtuma Sajenti Ilogi [askari jeshi-kambi ya Colito, sasa Lugalo] kumpindua Nyerere usiku wa kuamkia tarehe 20/Januari/1964 ili nafasi yake ichukuliwe na Oscar Kambona!

Licha ya salamu nyingi za pongezi kutoka kwa marais mbalimbali wa Afrika na kwingineko duniani za kumpongeza Kambona kwa kumpindua Nyerere ambaye hadi wakati huo alikwa ni kibaraka wa mabeberu na adui nambari moja wa umoja wa Afrika [maneno ya hayati Kwame Nkurumah], hata hivyo, Kambona aliisaliti Tanganyika [na Afrika kwa ujumla] kwa kitendo chake cha kukataa kuwa Rais wa Jamhuri ya Tanganyika baada ya Nyerere kupinduliwa!

Laana ya usaliti huo, haikumwacha salama Kambona, ilimwandama na kujikuta akilazimika kukimbilia uhamishoni!

Kuna sokomoko linaendelea huko nyumbani, kuhusu utata wa mkataba wa uwekezaji katika bandari za Tanzania [Zanzibar haimo!!!] na maeneo mengine ya kimkakati. Kwamba, ubovu wa vipengele vingi vya makubaliano [mkataba] baina ya DPW na Tanzania, unaufanya mkataba huo kuwa wa hovyo kuliko mikataba yote iliyowahi kuingiwa na serikali ya CCM!

Mkataba mbovu kuliko mikataba yote tuliyonayo, ni ule mkataba unaoitwa wa Tanganyika na Zanzibar ulioua taifa huru la Tanganyika na kuasisi kitu kinachoitwa Tanzania! Huu ndiyo mkataba wa hovyo kabisa kuliko mikataba yote!

Inawezekana kabisa kwamba, kama Oscar Kambona angetii amri ya Miungu na kukubali kuwa Rais wa Tanganyika pengine haya ya DPW [na mikataba mingine ya hovyo] yasingetukuta. Sababu ni rahisi, Kambona aliamini katika demokrasia, haki, usawa na uhuru. Nyerere aliamini katika udikteta, ubabe, ubinafsi, uroho wa madaraka, pombe na bangi!
FB_IMG_1690483278431.jpg
 
Back
Top Bottom