jMali
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 8,412
- 5,012
kila siku tunasikia "wazanzibari" wanadai hiki na kile, hususani kwenye katiba mpya, je wazanzibari ni kina nani hasa? Tuzingatie mifano kama: Rais ali hasan mwinyi kazaliwa bagamoyo lakini ni mzanzibari, Dr shein mzaliwa wa pemba ni mzanzibari, Mmasai, mchaga au "mbara" yoyote atayehamia zanzibar na kukaa miaka kadhaa naye anapewa uzanzibari (kama rais mwinyi).
Hivi mpemba aliyezaliwa bara na kukulia bara anaweza kuwa mzanzibari automatically tu kwa sababu babu yake alizaliwa zanzibar? au yeye atakuwa mbara?
Na je mbara aliyehamia zanzibar akawa mzanzibari (kisheria), akirudi bara na kuzaa watoto, hawa "wanyamwezi" nao watakuwa wazanzibari vile vile? Naomba tusaidiane.