Nadhani ile hali ya kutokuwa karibu kati ya mtoto wa kike tangu mdogo na baba yake
huenda ikawa inachangia.
Utakuta mtoto wa kike akiwa tu hata na shida hata ya kawaida anaambiwa amwambie kwanza mama halafu mama ndio amwambie baba ukiuliza sana utaambiwa ndio tamaduni zetu,na pia ukali kupita kiasi kwa baba.
Matokeo yake hawapati nafasi ya kujenga yale mahusiano ya upendo wa baba na binti yake,matokeo yake wanaishia kuonana kama mwanamke na mwanamme.