Mohamed Ismail
JF-Expert Member
- Mar 16, 2014
- 228
- 249
MY FUTURE WIFE
_______________________
Baada ya kutumia muda mwingi mchana katika kufanya mambo ya msingi na yasiyokuwa na msingi, inapofika muda wa kulala nakuwa nimechoka sana ambapo inabidi nilale usingizi wa pono. Kama kawaida yangu nina muda mwingi ila mambo machache. Nikilazimisha kuwa na mambo mengi na muda usitoshe najikuta hayo mambo yanakuwa siyo ya kwangu maana nimeingilia mambo ya watu.
Kama unavyojua kipindi hiki cha utandawazi ni bora ulale njaa kuliko kukosa bando la intaneti. Macho yangu yakiwa yamezidiwa uzito wa usingizi lakini bado nawasha kiswaswadu changu naingia mtandaoni kuangalia ulimwengu unavyoenda. Katikati ya kuperuzi bin kuperuzi mara paap! usingizi unanipitia na simu natupa huko.
Ndani ya dakika chache linanijizia jinamizi ninapambana nalo huku nikiweweseka. Ndani ya muda mchache uliojaa hofu na vitisho dhidi ya uhai wangu napata nguvu ya kushtuka nafumbua macho kuangalia adui sioni chochote. Nanyanyuka kitandani huku taa ikiwa bado imewaka. Akili inanijia najua hizi ni ndoto tu nasogea ukutani nazima taa ya chumbani na huku nakuta simu yangu ikiendelea kuangalia status za whatsapp pasipo mimi kujua chochote. Nazima data najiangusha kama gogo naendelea kufaidi starehe ya maskini isiyokuwa na gharama ambayo ni usingizi.
Ndani ya usingizi inanijia ndoto ya kukutana na my future wife. Sifanikiwi kuona sura yake bali naweza kuelezea wasifu wake. Kiukweli ni mwanamke ambaye kapendelewa kwa kila sifa ambayo mke wa mtu anastahili kuwa nayo. Nikiwa ndani ya ndoto naisikia sauti yake nzuri na nyororo imtoayo nyoka pangoni. Inapoingia masikioni mwangu nasisimika na kupagawa kama masai kapandisha morali.
Ninashtuka usingizini kumuangalia huyo anayetoa sauti hiyo najikuta nimekumbatia mto, ninakasirika ninaamua kujichagulia tusi ambalo halitaniudhi sana huku nikibaki najidharau. Baada ya hiyo ndoto usingizi unakata naanza kutafakari kama kawaida yangu. Mlimwengu mimi naanza kumuwazia My wife to be. Unaweza kubahatika kusoma ujumbe huu au usibahatike kusoma lakini naamini roho yako inasoma kile ninachokiandika hapa. Na wewe unayesoma ambaye siyo muhusika ebu nisaidie kusambaza ipate kumfikia.
Kwako mke wangu mtarajiwa najua unapitia mambo mengi mazuri na na mabaya na unaendelea kuyapitia ya walimwengu. Najua nakupa taarifa ambayo usingependa kuisikia huyo uliyenaye hatakuoa ila anakusaidia kuwa imara katika mahusiano yetu mimi na wewe. Umekuwa ukijiuliza labda una mkosi ndio maana huolewi la hasha Mwenyezimungu anakupenda anakusubirisha mpaka ukutane na mlimwengu mimi. Kuna watu najua roho inawauma kwanini mimi ndio nipendelewe huyu mwanamke aliyekamilika kila idara na afaaye kuwa mke wa mtu asubirishwe mpaka aonane na mimi. Bahati isiyo yako usiilalie mlango wazi wewe mbona umepewa hiyo nafasi lakini uliambulia kuitumia vibaya.
Laazizi , wa ubani wangu, mwanandani wangu, msiri wangu, nyongo mkalia ini na majina mengine mazuri yote nakuita. Usisononeke wala usimkufuru muumba yote yametokea kwa sababu tulikuwa hatuko pamoja ila najua si muda mwingi tutakuwa pamoja. Huna kasoro yeyote, huna tatizo lolote , huna ubaya wowote wewe umekamilika waswahili huku kwetu wasema waitwa full package wife. Wala usijione mdogo kama ni embe lilishakwiva linasubiri kuliwa hakuna haja ya kutumia chumvi tena kama ni ukakasi wote ulishakwisha.
Juzi siku ya Uhuru ulikuwa unajiuliza kwani hizi sherehe za nini?. Hukujua tu kwamba nchi hiii ni huru na sasahivi utapata uhuru wa kuwa na mlimwengu mimi. Ndio maana tunazidi kuliombea taifa hili lizidi kuwa na amani kama desturi yake. Ikishamwagika damu hata upendo huwezi kustawi .
Naomba nichukue nafasi hii adhimu kukuahidi kuwa nitakuheshimu, nitakupenda na nitakuwa tayari kukulinda kwa gharama yeyote. Kwangu mimi wewe ni wa thamani sana..... siko tayari kuchezea shilingi kwenye tundu la choo. Kuna hadithi moja nzuri ya mapenzi nilitamani nikusimulie hapa ila sitaweza hii itahitaji ufaragha kati yangu mimi na wewe na ikiwezekana nitakusimulia kwa kukunon'goneza masikioni mwako maana ni maamumu kwa ajili yako.
Naomba niishie hapa kwa leo. Ni mimi huyu huyu ambaye uliambiwa usipofunzwa na mama yako atakufunza.
#mlimwengumimi
Imeandikwa na
Mohamed Ismail Rwabukoba
Email: mohammedismail613@gmail.com
Phone no: 0762070361
11/12/2019