My Ex Angel From GAS CITY

My Ex Angel From GAS CITY

msolopaganzi1954

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2018
Posts
763
Reaction score
379
.....Ndugu wana JF, leo nimejiona ni share kidogo True story ya maisha yangu ambayo nahitaji Ushauri au Masaada wa kitabibu.
..Nilijiunga Chuo kikuu (Udsm) 2008...nikiwa mwaka wa kwanza nilipata kitoga Cha mwaka wa Pili,
...Tulianza mapenzi motto Sana, kila Mara naenda Rum kwake nae anakuja Rum kwangu pale Mabibo Hostel, Koz yake ilikuwa miaka minne yangu miaka Mitatu. HIVYO kihesabu tulimaliza mwaka mmoja.
....Rafiki zake Wengi walikuwa Hawapendi urafiki wetu, Coz may b nilikuwa first year au sikuwa na mizigo.
..Akanishauri Nipange chumba Out of Campass, Ili kipindi cha Likizo tuwe Tunajichimbia maghetoni.. Nikafanya hivyo, nikapanga chumba karibu na Nyumbani kwetu, kwani Mimi wazazi wangu walijenga hapa Dar, na yeye Kwao Mtwara mjini karibu na Hospital ya Mkoa.
...Tulinunua vitu vya Chumbani pamoja mpaka Ghetto likakamilika mazima..Tukamaliza Chuo,tukarudi Ghetto, yeye alikataa kurudi kwao mtwara, Coz Maisha yalikuwa Tait Sana, So Tukawa tunaishi kwa Msaada wa wazazi wangu, kwani walimkubali Sana.
...Ghafla nikapigiwa simu na mwanangu mmoja, kuwa Gazeti LA mwanannchi kuna post za kazi zimetoka, nikanunua, nikakuta nafasi za Assistance Tortorial anaitajika Chuo kimoja cha Serikali tena kikubwa but nje ya Dar, na ni koz ya Yule manzi wangu, nikamshauri Aombe, mwanzo alisita but akaja kukubali, Akajaza Baada ya three weeks wakampigia Simu aende kufanya Interview?
.....Nauli sasa ikawa kimbembe, nikampanga Bi mkubwa akanipa,Bibie nikamsindikiza mpaka Ubungo akaenda, then akarudi, na Akawa kapata Kazi,
...Siku anayoondoka kwenda Kazini mkoa, Nakumbuka tuko Ubungo Terminal Mrembo Analia Sana, nami machozi yananilenga, but ananiambia anaendea kutengeneza mazingira,

Kumbuka Mimi hapo bado Sijapata kazi Rasmi, but nafanya za Kuunga unga Tu,
Mrembo baada ya kuondoka, Zikapita wiki, mwezi, akaanza kubadilika mazima, SMS ya asubuhi anakujibu Usiku, na anakuambia Ubize wa kazi, Mara apokei simu Mara anazima simu saa moja Usiku Mara Nikimtumia email Hajibu, ilimladi tu ilawa Chenga chenga, dah Nilivurugwa Sana mzee Baba,
...Jumamosi moja hivi Niko Leaders kwenye Bonanza Inaingia sms kwa simu yangu toka kwa mrembo wangu from Gas City,
Sikuamini, ananiambia Tuachane, Aoni FUTURE kwangu, na ameshapata Mtu WA Kumuoa.
Nilichoka Sana Nusura Nianguke Chini.
..Kweli akaolewa na Mwalimu mwenzie hapo chuoni, Wakazaa watoto wawili, baadae anakuja kugundua jamaa ana mke kwao na ana watoto 3,pia jamaa jamaa kamshawishi wamekopa pesa kupitia Account za mrembo wangu, alafu jamaa cha pombe mbaya,
....Nilibadilisha namba ya simu, sababu ya kuvurugwa, but Juzi Kati Mrembo Yule kanipigia Simu Uku analia na kuniomba msamaha kwa yote aliyonifanyia, na alikuwa Dar kwenye Seminar Flan Pale Landmark UBUNGO,
KIUKWELI sikumuelewa kabisa na wala Sikuenda Kama alivyotaka.

NB:Najuha Mimi yamenikuta hivi, ila Naamini wanaume wenzangu yapo yaliyowakuta Kama hili au Zaidi ya Hili.
#Lakini Alikuwa Fundi Balaaah, Si Unajuha mambo ya Korosho City tena?
#Maamuzi Niliyofanya ni Sahihi au Nilikosea?
Thanks
 
Pole sana kiongozi... Huyo sio wa kumrudisha tena hakufai.... Fyekelea mbali kabisa...

Hospitali wakizaliwa watoto 10 basi 7 ni wa kike na 3 wakiume...

Asikuumize kichwa wanawake wapo wengi saaaanaaa
 
Mistake utakayoifanya ni kukubali kujirudisha kwa huyo dada

Dili na maisha yako, kama alivyokua akfanya na wewe mfanyie usipokee sim wala kujibu texts na emails atakazokutumia achana naye
 
Mistake utakayoifanya ni kukubali kujirudisha kwa huyo dada

Dili na maisha yako, kama alivyokua akfanya na wewe mfanyie usipokee sim wala kujibu texts na emails atakazokutumia achana naye
Madam hii story ya jamaa imesisimua saana kama ni ya kweli lakn..je inatufundisha nini?
 
Maamuzi sahihi kabisa tafuta wako. Mungu atakuandalia anayefanana na wewe
 
Kijana wa kiume msimamo,achana naye kabisa na ikiwezekana block namba yake,na mchane kuwa humtaki kwa sasa,watoto wawili amezaa na huyo bhana bado unakutaka nn mkuu,fyekelea mbali sana
 
Sijui kwa nini wanao ondoka kwa mbwembwe mwisho wa siku wana angukia pua.
Ule usemi wa "karma is a bitch" siyo mchezo wanasema malipo ni hapa hapa ulimwenguni mbinguni kulia manamba na kukatwa vibangala!
 
Hicho kichwa cha uzi tu kinaonyesha bado umekamatwa,hakuna cha kukushauri hapa ulishazama na utaendelea kuzama.
 
Naanza kupata ukakasi na degree za UDSM,kuandka kiswahili ni shida kiasi hicho,vipi kwa lugha ya malkia mkuu?
Inawezekana alichosema Dk.Shule kina ukweli ndani yake,kuna degree za boxer pia pale UD,ikiwemo ya mtoa mada.
Anyway pole sana mkuu,umefanya uamuz wa busara sana,na kamwe ucmpe second chance huyo msaliti,kama m2 ana watoto wawil means n muda mrefu umepta toka mmetengna,na ushazoea hali,move on with yo life nigga!
 
Hivi ni kweli huyu amesoma udsm miaka 3?

Halafu humu jf wanaume wote wanawake wao mafundi kitandani na wazuri.
Muhitimu wa UDSM Unajuha sana kuandika, ila sijahelewa hapo mwisho ulivyouliza maamuzi uliyochukua ni sahihi au ulikosea? maamuzi ya kumuacha aolewe au maamuzi ya kutokwenda kumuona Landmark au maamuzi gani?
 
Hivi ni kweli huyu amesoma udsm miaka 3?

Halafu humu jf wanaume wote wanawake wao mafundi kitandani na wazuri.
Lol, kwa mujibu wake ni muhitimu wa UD ngoja tuamini hilo.

Ukiona mtu anaanza kumsifia Ex wake ni mzuri kwa bed ujue bado amekamatika, hapo ushauri utakaomfaa ni 'follow your heart but take your brain with you'
 
Baada ya kuzaa watoto 2 nje ndo anakutafuta...Ila tuweke akiba ya maneno upo uwezekeno watarudiana hawa maana tumeona mtoa mada akimsifia kama ni fundi balaa!!
 
Sometimes wanawake bhana,yani wanakuua hivi hivi na pressure
 
Back
Top Bottom