My 20 laws of power

My 20 laws of power

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
12,314
Reaction score
18,146
1. Usikopeshe zaidi ya kile ambacho huwezi kukipoteza.

2. Yeyote anayekukopa kitu chukulia kuwa hatokulipa kabisa, ishi katika hali hiyo.

3. Juzuie kusema mambo yako binafsi unapokuwa na watu, utaweza kujizua kuwa mmbea wa kusema mambo ya wengine.

4. Kuwa bize na mambo unayoyataka na kupenda yatokee katika maisha yako,unapokuwa bize kupingana na usiyoyataka jua unapoteza energy yako katika kuyapinga,tumia energy hiyo katafuta unayoyataka.

5. Usipangie mahesabu pesa iliyo mikononi kwa mwingine hata kama ni yako.kilicho kwako ndio chako.

6. Unapodaiwa na mtu laki moja alafu mshahara wako ujao ni laki tano basi hakikisha unaelewa na unajiseti kiakili kuwa mshahara huo ni laki nne tu.

7. Kuwa mpole na mkarimu kwa watu wanaokuchukiza na kukukera ndio ustaarabu wa kweli kwako itakufanya uzidi kuheshimika na wala usitafute heshima kwa nguvu.

8. Usikubali kuchangia kuwasema wengine wasiokuwepo,kwani na wewe usipokuwepo wengine watakusema pia.

9. Lolote unalohisi kuwa unalihitaji katika maisha yako basi anza kulifanya sasa hivi japo kidogo kidogo.hakuna kitu baadae.muda ni sasa hivi.

10. Kumbuka kuwa ni bora kuajiriwa katika kazi unayoipenda kuliko kujiajiri katika biashara unayoichukia.

11. Hakuna kitu hakihitaji shukurani,hakikisha unashukuru katika kila jambo lako linalotokea ama unalofanyiwa

12. Usikosoe chochote ulicholetewa na mtu iwe zawadi ama ulimuagizia,sifia akiwepo na kosoa akiondoka tena ukiwa peke yako.

13. Kama mtu ana tabia ya kukukopa sana hakikisha usimdai pale tarehe ya malipo ikipita,hiyo itakufanya uwe na hoja ya kutokumkopesha tena akija kukukopa.

14. Weka akiba ya maneno.bora umtetee mtu muovu mbele za watu kuliko kumsema vibaya mbele za watu. Hutojutia kimya chako bali neno lako ndo hulijutia zaidi.

15. Maneno ya kejeli yanakufanya uwe vile unavyoyasema,maneno yako yanaamua uwe vipi, kuwa mtu chanya muda wote sema maneno mazuri.

16. Usimkejeli mtu mmoja ili uwafurahishe watu mia moja,watafurahi kwa sababu ya kukusitiri wewe ujione kama umewafurahisha kweli lakini nao umewahuzunisha.

17. Unapotaka kumfanyia ubaya mtu kwa sababu ya nafasi yako au cheo chako kumbuka kuwa hiyo sio mwisho wa kukutana nae.fikiria mbele.

18. Ukiwa haukuweza kuwa na demu mmoja wakati wa ubachela wako,basi ni ngumu kutulia na mke mmoja wakati wa ndoa yako.

Hakuna kutulia kwenye kuoa kama mtu hakutulia kwenye ubachela

19. Idadi ya wanaokusifia wakati upo nao ni ndogo kuliko idadi ya wanaokuponda wakati haupo,hayo ni maoni yao,kuwa bize na mambo yako.

20. Usimsaidie mtu huku unakilalamikia juu ya unachompa kwamba unakihitajia na kinakusaidia,atapokea shingo upande na hato appreciate msaada huo.
 
15.Maneno ya kejeli yanakufanya uwe vile unavyoyasema,maneno yako yanaamua uwe vipi, kuwa mtu chanya muda wote sema maneno mazuri.

huu ndio ugonjwa wetu walio wengi hapa JF, hadi tunakejeli chakula chetu mezani kabla ya kula!
 
15. Maneno ya kejeli yanakufanya uwe vile unavyoyasema,maneno yako yanaamua uwe vipi, kuwa mtu chanya muda wote sema maneno mazuri.

huu ndio ugonjwa wetu walio wengi hapa JF, hadi tunakejeli chakula chetu mezani kabla ya kula!
mkuu ni hatari.

Tumezoea kuponda kila kitu..

Baada tutafute mazuri katika kila baya,sisi tunajikita kutafuta mabaya katika kila zuri.
 
1. Usikopeshe zaidi ya kile ambacho huwezi kukipoteza.

2. Yeyote anayekukopa kitu chukulia kuwa hatokulipa kabisa, ishi katika hali hiyo.

3. Juzuie kusema mambo yako binafsi unapokuwa na watu, utaweza kujizua kuwa mmbea wa kusema mambo ya wengine.

4. Kuwa bize na mambo unayoyataka na kupenda yatokee katika maisha yako,unapokuwa bize kupingana na usiyoyataka jua unapoteza energy yako katika kuyapinga,tumia energy hiyo katafuta unayoyataka.

5. Usipangie mahesabu pesa iliyo mikononi kwa mwingine hata kama ni yako.kilicho kwako ndio chako.

6. Unapodaiwa na mtu laki moja alafu mshahara wako ujao ni laki tano basi hakikisha unaelewa na unajiseti kiakili kuwa mshahara huo ni laki nne tu.

7. Kuwa mpole na mkarimu kwa watu wanaokuchukiza na kukukera ndio ustaarabu wa kweli kwako itakufanya uzidi kuheshimika na wala usitafute heshima kwa nguvu.

8. Usikubali kuchangia kuwasema wengine wasiokuwepo,kwani na wewe usipokuwepo wengine watakusema pia.

9. Lolote unalohisi kuwa unalihitaji katika maisha yako basi anza kulifanya sasa hivi japo kidogo kidogo.hakuna kitu baadae.muda ni sasa hivi.

10. Kumbuka kuwa ni bora kuajiriwa katika kazi unayoipenda kuliko kujiajiri katika biashara unayoichukia.

11. Hakuna kitu hakihitaji shukurani,hakikisha unashukuru katika kila jambo lako linalotokea ama unalofanyiwa

12. Usikosoe chochote ulicholetewa na mtu iwe zawadi ama ulimuagizia,sifia akiwepo na kosoa akiondoka tena ukiwa peke yako.

13. Kama mtu ana tabia ya kukukopa sana hakikisha usimdai pale tarehe ya malipo ikipita,hiyo itakufanya uwe na hoja ya kutokumkopesha tena akija kukukopa.

14. Weka akiba ya maneno.bora umtetee mtu muovu mbele za watu kuliko kumsema vibaya mbele za watu. Hutojutia kimya chako bali neno lako ndo hulijutia zaidi.

15. Maneno ya kejeli yanakufanya uwe vile unavyoyasema,maneno yako yanaamua uwe vipi, kuwa mtu chanya muda wote sema maneno mazuri.

16. Usimkejeli mtu mmoja ili uwafurahishe watu mia moja,watafurahi kwa sababu ya kukusitiri wewe ujione kama umewafurahisha kweli lakini nao umewahuzunisha.

17. Unapotaka kumfanyia ubaya mtu kwa sababu ya nafasi yako au cheo chako kumbuka kuwa hiyo sio mwisho wa kukutana nae.fikiria mbele.

18. Ukiwa haukuweza kuwa na demu mmoja wakati wa ubachela wako,basi jua kuwa ni ngumu kutulia na mke wako mmoja.

19. Idadi ya wanaokusifia wakati upo nao ni ndogo kuliko idadi ya wanaokuponda wakati haupo,hayo ni maoni yao,kuwa bize na mambo yako.

20. Usimsaidie mtu huku unakilalamikia juu ya unachompa kwamba unakihitajia na kinakusaidia,atapokea shingo upande na hato appreciate msaada huo.
18 inanigusa vizuri sana
 
"Fimbo iliyouwa nyoka huwa haiwekwi sebuleni "

Nilimsikia mchungaji mmoja akisema hivo nadhani kuna ujumbe fulani hapo
 
Back
Top Bottom