Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Imefika wakati sasa tuwe wakweli na tufungue macho, pamoja na juhudi na michango yake mingi aliyoitoa baba wa taifa letu Mwl.Nyerere nafikiri sasa pia umefika wakati wa kumpumzisha na kuanza kuwaenzi wazee wetu wengine ambao binafsi ninaweza kusema kwamba Mlm.Nyerere pia alipokea kijiti ktk kwao kama akina Mirambo, Mkwawa, Isike, Kinjikitile "Bokelo" Ngwale na wengineo ambao walianzisha mapambano dhidi ya udhalimu wa Kikoloni!
Hivyo basi kwa kuwa tayari tuna kumbukumbu za kutosha kuhusu Mwl.Nyerere ningependelea sasa tuanze pia na kuwaenzi hawa wengine kwa mfano binafsi sikupendezwa na daraja jipya kuitwa Nyerere angalau lingeitwa Kinjikitile, Mirambo au hata Mkwawa!