mnasikitisha sana, anaetaka kutokwenda awaulize walimu waliopangiwa mwaka jana wakakataa wanavyosota kutafta kazi kwenye vijishule vya kijinga wanalipwa mshahara 150,000 na headmaster. Tena wanajuta kweli kweli? Si bora uende utatafuta uhamisho baadae? Acheni utoto mtaa ni mgumu hasa nyie wanaume utaoa au umeoa mkeo na watoto utawalisha mawe? Kisa upo town bila kazi. Kwanza huko bush life is easy, unaweza kufanya kazi kwa malengo ukasave pesa ukawa na maisha yako mazuri, ukajenga, ukasomesha na kufungua miradi. Watu wengine hambebeki hata kwa mbeleko ya chuma. Kumbuka usichezee kazi chezea mshahara, majuto ni mjukuu.