JUkonga
Member
- Dec 30, 2015
- 14
- 13
Mh. Waitara (Mb) jioni hii akichangia hoja ya waziri wa fedha na mipango bungeni amejikita katika maeneo mawili, Elimu na Utawala bora.
Kwanza amewaambia CCM kuwa ni waongo na pia ni waoga. Amewaambia kuwa ili mipango wanayoizungumza itekelezeke ni lazima wang'oke madarakani kwakuwa wamechoka sana na ndio chanzo cha umasikini wa watanzania.
Akizungumzia uongo wa CCM ktk elimu, amesema kuwa CCM inawadanganya watanzania kwakuwa inafahamu kuwa hakuna elimu ya bure kama wanavyodai bali wazazi wanachangia elimu ya watoto wao na serikali inachangia.
Pia amewaambia CCM kuwa ni waoga sana na hawana hoja ndio sababu wanatumia jeshi la polisi hadi ndani ya ukumbi wa bunge badala ya kushindana kwa hoja kama ulivyo utamaduni wa mabunge yote duniani.
Pili amemalizia kwa kuwaambia CCM kuwa Maalim Seif alishinda uraisi wa Zanzibar katika uchaguzi wa October 25, 2015 na hata CCM wenyewe wanajua, watanzania wanajua, Afrika inajua na dunia inajua. Amewataka CCM kukubali matokeo hasa pale wanapokuwa wameshindwa.